Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kiongozi wa ACT Wazalendo.,Zitto Kabwe, amefungua kesi ya Kikatiba dhidi ya mosi; Sheria ya Ukaguzi namba 11 ya mwaka 2008 kukiuka Katiba na pili Uteuzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) uliofanywa na Rais Magufuli kuwa kinyume na masharti ya Katiba.
Kesi hiyo ya Kikatiba namba 1 ya mwaka 2020 ambayo Ndugu Zitto anawakilishwa na Wakili Nyaronyo Kicheere, imefunguliwa Masjala Kuu ya Dar Es Salaam na imepangiwa Majaji Mlacha, Masoud na Masabo.
Zitto anaiomba Mahakama kutamka kuwa kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi No.11/2008 inaenda kinyume na Katiba kwa kukiuka Ibara ya 144(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kupingana na kifungu 62(a) cha Sheria ya Ukaguzi ambacho kinaendana na Katiba.
Aidha Zitto anaiomba Mahakama kutamka pia kuwa uamuzi wa Rais Magufuli wa kumwondoa Ofisini Prof. Assad ulikuwa kinyume na Katiba kwani Prof. Assad hakuwa ametimiza miaka 65 ya kisheria wala miaka 60 ya Kikatiba. Pia uteuzi wa Bwana Kicheere hukufuata Katiba ufutwe.
Zitto Kabwe anasema baada ya kutafakari kwa kina ameonelea kuwa uvunjifu wa Katiba uliofanywa na Rais Magufuli haupaswi kukaliwa kimya. Kama Mtanzania, kwa miaka 8 aliyehudumu ktk Kamati za Bunge za Uwajibikaji, itakuwa dhambi kutotaka tafsiri ya Mahakama kuhusu uteuzi wa CAG.
"Nalifanya hili kulinda ma CAG wajao kwani tukiacha Katiba ikichezewa Ofisi ya CAG inayopaswa kuwa Huru KIKATIBA itakuwa dhaifu mno na kuhatarisha usimamizi bora wa Fedha za Umma. Kwa maoni yangu CAG akishateuliwa haondokeki mpaka afikie umri wa kustaafu kisheria." Zitto Kabwe.
Shauri hili la Zitto Kabwe litaitwa kwa mara ya kwanza Januari 28, 2020 saa 3 Asubuhi, ambapo Wajibu shauri ni Rais Magufuli kupitia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, CAG Mussa Assad na Bw. Charles Kicheere.
Imetolewa na;
Suphian Juma, Afisa Habari, ACT Wazalendo.
Jan 25, 2020.