Zitto afungua kesi ya kikatiba kupinga uteuzi wa CAG mpya

Asad kastaafu juzi tuu njaa imeanza kuuma na anatuma vijana wake ili wafanye jitihada wamrudishe kazini? umri!!! baba umri !!!baba

ALIIMBA MR.EBO
Njaa inauma...... chunga usichinje njau...........njaa inauma.........
Alikuwa akiwaachia upinzani wale ruzuku watakavyo Sijui walikuwa wakimgawia ?

.CAG mpya eneo la ruzuku kula nao sahani moja Hawa akina Zitto Kabwe aliyekuwa akificha madhambi yao profesa Assad kaondoka.Peleka special audit please haraka
 
Anamtishia nyau CAG mpya asifanye special audit ya matumizi ya pesa za ACT wazalendo

CAG mpya nenda kagua miaka ya nyuma upya ikiwezekana Rudi hata Saba nyuma .Tuma kikosi kazi.Hilo.ni tishio la kutaka umuogope ukae mbali na ulaji ruzuku wake
Hujaacha majungu?
 
Naomba unitajie Majina ya CAG mpya na Majina ya Mwanasheria wa Zitto huyo anaemuwakilisha labda sijaelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na umefutiwa zaidi ya moja... Kuna nyingine umeniqoute kabla sijajibu ikafutwa... Hii inaonyesha hujatulia hata... Kiufupi una mihemko ya kisiasa... Sijaona hoja uliyojenga hata moja... Yaani unafanya kama ninyi mnavyosutana... Achana na siasa,you are an adult but it seems you're still a kid in politics.

Sijaandika kitu kibaya kikafutwa! Hata hyo comment yangu bado naiona! Ww ndo uache mihemko mkuu!
 
Are you trying to scare him?

Taking risk in anything positive in life is part and parcel of any successful person!!

By the way, whether be it a lost or win battle; the precedence must be recorded for a future generation...!!
I concur
 
Naomba unitajie Majina ya CAG mpya na Majina ya Mwanasheria wa Zitto huyo anaemuwakilisha labda sijaelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mleta mada kajichanganya muda mrefu alikuwa hayuko mtandaoni baada ya chadema kumpiga chini kwenye chaguzi zao za ndani naona kapost mbio.mbio.akiwa na hang over ya frustration kichwani za kupigwa chini na chadema chaguzi zao za ndani

Hizi post anaonyesha wazi kahamia ACT wazalendo hayuko Tena chadema.Kaandika Akiwa na misongo ya mawazo msamehe bure
 
Chadema mkuje huku
Mleta mada salary Slip alikuwa mwanachama wenu katimkia ACT wazalendo baada ya kupigwa chini chaguzi zenu za ndani.Alikuwa kinara wenu humu Jamii forums kuwatetea kwa nguvu zote .Kupigwa chini tu kwenye chaguzi zenu kaehuka
 
Kiongozi wa ACT Wazalendo.,Zitto Kabwe, amefungua kesi ya Kikatiba dhidi ya mosi; Sheria ya Ukaguzi namba 11 ya mwaka 2008 kukiuka Katiba na pili Uteuzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) uliofanywa na Rais Magufuli kuwa kinyume na masharti ya Katiba.
EPIFBLXWAAAxXjv.jpg

Kesi hiyo ya Kikatiba namba 1 ya mwaka 2020 ambayo Ndugu Zitto anawakilishwa na Wakili Nyaronyo Kicheere, imefunguliwa Masjala Kuu ya Dar Es Salaam na imepangiwa Majaji Mlacha, Masoud na Masabo.

Zitto anaiomba Mahakama kutamka kuwa kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi No.11/2008 inaenda kinyume na Katiba kwa kukiuka Ibara ya 144(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kupingana na kifungu 62(a) cha Sheria ya Ukaguzi ambacho kinaendana na Katiba.

Aidha Zitto anaiomba Mahakama kutamka pia kuwa uamuzi wa Rais Magufuli wa kumwondoa Ofisini Prof. Assad ulikuwa kinyume na Katiba kwani Prof. Assad hakuwa ametimiza miaka 65 ya kisheria wala miaka 60 ya Kikatiba. Pia uteuzi wa Bwana Kicheere hukufuata Katiba ufutwe.

Zitto Kabwe anasema baada ya kutafakari kwa kina ameonelea kuwa uvunjifu wa Katiba uliofanywa na Rais Magufuli haupaswi kukaliwa kimya. Kama Mtanzania, kwa miaka 8 aliyehudumu ktk Kamati za Bunge za Uwajibikaji, itakuwa dhambi kutotaka tafsiri ya Mahakama kuhusu uteuzi wa CAG.

"Nalifanya hili kulinda ma CAG wajao kwani tukiacha Katiba ikichezewa Ofisi ya CAG inayopaswa kuwa Huru KIKATIBA itakuwa dhaifu mno na kuhatarisha usimamizi bora wa Fedha za Umma. Kwa maoni yangu CAG akishateuliwa haondokeki mpaka afikie umri wa kustaafu kisheria." Zitto Kabwe.

Shauri hili la Zitto Kabwe litaitwa kwa mara ya kwanza Januari 28, 2020 saa 3 Asubuhi, ambapo Wajibu shauri ni Rais Magufuli kupitia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, CAG Mussa Assad na Bw. Charles Kicheere.

Imetolewa na;
Suphian Juma, Afisa Habari, ACT Wazalendo.
Jan 25, 2020.
Kwa mtu yeyote yule ambaye ni makini na mwenye kujali, kamwe hawezi kuacha katiba ikikiukwa kwa makusudi na wale ambao wamepata madaraka kupitia kitiba hiyo hiyo. Mh. Zito ni lazima aungwe mkono, kwa kuwa ameonyesha njia.

Ni funzo jipya kwa vyama vyote vya upinzani, ili kufufua ari mpya na kuunga mkono jitihada za Marehemu Mtikila (Mola amrehemu) ktk kila eneo ambalo linaonyesha kwa dhahiri kuchezewa ama kukiukwa kwa makusudi na serikali kuendana masharti yaliyopo ndani katiba yetu. Kunung'unika tu pasipo kuchukua hatua stahiki huwa haisaidii kitu chochote. Kudos Hon. Zitto Zuberi Kabwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijaandika kitu kibaya kikafutwa! Hata hyo comment yangu bado naiona! Ww ndo uache mihemko mkuu!
Ipo wapi ile post yako uliyoniqoute halafu mwisho ukaishia na emoji za kusonya...ilete..,nilimqoute mtu mwingine wewe sijui hukupendezwa nayo ukanijibu violently mod wakaifuta...ilete kama bado unaiona... Act kama unaelewa unachofanya.... Wewe unakuwa kama wale vijana wa bodaboda ambao wakiona bendera ya chama chao wanatoka na wazimu...Jibu mtu kiutashi wewe.... Sijui hayo majazba mnayatolea wapi sababu hata kiongozi wenu mkuu hayupo hivyo...Tatizo mnachanganywa na hao wanaogombea uwenyekiti serikali za mitaa na nyie mnajiona wajaaanja.
 
Ccm imechokwa jua hvyo!
 
Kiongozi wa ACT Wazalendo.,Zitto Kabwe, amefungua kesi ya Kikatiba dhidi ya mosi; Sheria ya Ukaguzi namba 11 ya mwaka 2008 kukiuka Katiba na pili Uteuzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) uliofanywa na Rais Magufuli kuwa kinyume na masharti ya Katiba.
EPIFBLXWAAAxXjv.jpg

Kesi hiyo ya Kikatiba namba 1 ya mwaka 2020 ambayo Ndugu Zitto anawakilishwa na Wakili Nyaronyo Kicheere, imefunguliwa Masjala Kuu ya Dar Es Salaam na imepangiwa Majaji Mlacha, Masoud na Masabo.

Zitto anaiomba Mahakama kutamka kuwa kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi No.11/2008 inaenda kinyume na Katiba kwa kukiuka Ibara ya 144(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kupingana na kifungu 62(a) cha Sheria ya Ukaguzi ambacho kinaendana na Katiba.

Aidha Zitto anaiomba Mahakama kutamka pia kuwa uamuzi wa Rais Magufuli wa kumwondoa Ofisini Prof. Assad ulikuwa kinyume na Katiba kwani Prof. Assad hakuwa ametimiza miaka 65 ya kisheria wala miaka 60 ya Kikatiba. Pia uteuzi wa Bwana Kicheere hukufuata Katiba ufutwe.

Zitto Kabwe anasema baada ya kutafakari kwa kina ameonelea kuwa uvunjifu wa Katiba uliofanywa na Rais Magufuli haupaswi kukaliwa kimya. Kama Mtanzania, kwa miaka 8 aliyehudumu ktk Kamati za Bunge za Uwajibikaji, itakuwa dhambi kutotaka tafsiri ya Mahakama kuhusu uteuzi wa CAG.

"Nalifanya hili kulinda ma CAG wajao kwani tukiacha Katiba ikichezewa Ofisi ya CAG inayopaswa kuwa Huru KIKATIBA itakuwa dhaifu mno na kuhatarisha usimamizi bora wa Fedha za Umma. Kwa maoni yangu CAG akishateuliwa haondokeki mpaka afikie umri wa kustaafu kisheria." Zitto Kabwe.

Shauri hili la Zitto Kabwe litaitwa kwa mara ya kwanza Januari 28, 2020 saa 3 Asubuhi, ambapo Wajibu shauri ni Rais Magufuli kupitia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, CAG Mussa Assad na Bw. Charles Kicheere.

Imetolewa na;
Suphian Juma, Afisa Habari, ACT Wazalendo.
Jan 25, 2020.
Zitto ni mdini sana!
 
Back
Top Bottom