Anachokifanya Zito ni sahihi sana. Hata kama hukumu wengi wanaona inajulikana lakini ni vema mashauri kama haya yakiwepo maana yanatunza kumbukumbu sahihi za historia ya Taifa letu.
Matukio haya yataeleza jinsi uvunjifu wa katiba ulovyoweza kufanyika wakati fulabu, jinsi watu walivyopinga kwa njia mbalimbali, na jinsi mfumo wa mahakama ulivyoshindwa kutimiza wajibu wake.
Hongera sana Zito. Kesi za namna hii zilistahili kuwa nyingi. Kila tukio ambalo watu wanasema katiba ilivunjwa, na hasa na viongozi, ni vema kufungua kesi, hata kama mahakama isiposimamia ukweli, kumbukumbu itakuwa imewekwa.