Halafu pia maswali yafuatayo:
1. Je Zitto anataka kumpigia kampeni huyo Kafulila kwa kuwa tu ni rafiki yake?
2. Utaratibu wa kuomba nafasi ya kugombea ukoje NCCR? kwani Kafulila ni mgombea tayari? Si kuna mchakato au?
3. Zitto kabwe kafanya research gani kuonyesha kuwa Kafulila anakubalika kwenye jimbo? au kwa kuwa tu yeye anamtaka?
4.Kwa akili ile ya Kafulila na maneno yale aliyosema siku anaondoka Chadema je ni kweli Kafulila ni kiongozi wa maana? wa kupiganiwa kuwa mbunge?
5. Kwa nini kama Zitto ana mapenzi na Chadema asiwaombe NCCR wawaachie jimbo Chadema badala ya yeye kusema eti anamuunga mkono mgombea wa NCCR!! wa Chadema je? au kwa kuwa ni rafiki? je NCCR na Chadema Zitto anapenda chama gani?
6. Ina maana Zitto anaweka mbele urafiki kuliko chama? je ana tofauti gani na Kikwete?
7. Kwa nini Zitto asikubali tu kuwa Kafulila sasa yuko NCCR na kwamba urafiki wao unaendelea lakini wanaamini itikadi tofauti?
8. Kafulila amekwenda NCCR kwa ajili ya kupewa nafasi ya kugombea ubunge? Je akishindwa kwenye uchaguzi ndani ya NCCR hatima yake itakuaje? manake mind you sio lazima agombee yeye! na je akishindwa kwenye uchaguzi mkuu atafanya nini? atabaki NCCR?
9. Je Zitto haoni kwamaba natumia issue ya Kafulila kutaka tu kupimana ubavu na viongozi ndani ya Chadema?
10. kwa hiyo kampeni zikianza huko kigoma Zitto atakuwa jukwaa gani NCCR au Chadema?
11. Je Zitto anatambua kuwa suala zima hapa si la Kafulila na Zitto bali ni Chadema na NCCR? Yani it is not about individuals it is about the party , the team teamwork?
12.Chadema for now will be better without Zitto than with him.BUT please msimfukuze..msifanye kosa walilofanya wabunge wa CCM la kumfukuza Zitto bungeni na hatimaye kumpa public symphathy ya bure kabisa ambayo ndio inamlinda hadi leo japo imeshuka sana kwa sasa.
maswali mazuri,
1. Umeonyesha NCCR na Chadema hawawezi kuweka mgombea mmoja jimbo moja? si wote wapinzani?
2. Umeonyesha kuwa hata NCCR kumkaribisha Kafulila kwa lengo la kugombea ubunge nao hawajafanya assignment yao vizuri
3. Nilishasema kuondoka kwa watu kama akina Kafulila na Kupiga domo ubaya waliofanyiwa ndani ya Chadema ni ujinga na utoto!
4. with that crazy passion still Nccr wanamchukua kama mtu wao
5. Zitto naye kusema(sijathibitisha) kuwa anampigia kampeni chadema-kawa individual zaidi yuko kivyake!this is serious case
6.Umeonyesha pamoja na kupiga kelele kote huko kwa zito bado chama chake hakijamchukulia hatua mpaka leo hii!!!-Kwa nini JK hawachukulii hatua watu wa chini? si kwa sababu naye ni fisadi? this is serious kwa naibu katibu mkuu wa chama ku-act kama Zitto! inanyesha chama chote kimeoza na atakayemgusa Zitto lazima ajiulize mara mbili!!!
7. Mwisho nasikitika kama siyo kukupa pole kuwa uko biased na sio mkweli kusema Zitto alipewa sympathy na wananchi alipofukuzwa bungeni-Please kua kidogo na uwe mkweli, hata kama zama zile ulikuwa unampenda kiri kwa lile alilolifanya acha sanaa na chuki hapa
8. Nashangaa unatoa solution ya ajabu kabisa pamoja na maswali yako mazuri kuwa Zitto abaki chamani, at the sama time unalaumu anaweka urafiki kuliko chama, hii solution ni nzuri? na inakisaidiaje chama?
Maoni yangu.
1. Kama chama cha chadema wanaona Zito kawakosea na yuko kinyume nao, solution ni kumfukuza-Ukimfukuza unaleta sense ya chama kama watu na sio chama kama individual!
2. Chadema kutomchukulia hatua zito, kunaonyesha kuna udhaifu wa chadema kama chama, humo ndani inaonyesha kuna makundi makundi na pengine wanaona wakimfukuza Zitto basi kuna kuvunja chama! kesho atatokea Zito mwingine na kumchukulia hatua itakuwa haiwezekani kwani kuna wengine hawachukuliwi hatua!
3. Inaonyesha pengine haya yote unayoyasema na kujadili humu, uongozi unaona kama mnamzushia Zitto kwa hiyo Zitto ni safi kabisa, japo Lukule unatoka povu humu
4. Kumpa uongozi mkubwa kama huo Zitto na kuonyesha utovu wa nidhamu(kama unavyomuona wewe!) kunaonyesha chama kizima hakina nidhamu, intelligence, wala hakiwachunguzi watu kabla ya kuwapa uongozi, hatari yake ni kuwa kesho kama kuna pandikizi la CCM litaingia na kukiharibu chama na kutokomea, hii ni hatari na si kitu cha kuchezewa mkuu!
5. Naona kuna haja ya vyama vya upinzani kuwa na special contract na viongozi wake kama akina kafulila, na katika contract ieleze kabisa ni mwiko kusema ubaya wa chama kupitia media, kama wasiporidhika na utendaji wondoke kimyakimya-upo hapo?
nimetoa point sita,
wewe unasemaje ishu ya kafulila kutoka chadema na kwenda nccr kisa anataka ubunge unafikiri anataka nini?-ulaji au sio
kwa nini leo mimi nisihitimishe kuwa vyama vyote hivi vya upinzani wanatafuta kula??
1. Kwa nini mtu anang'ang'ania kuwa lazima we mwenyekiti wa chama? refer Mrema, Mbowe n.k
2. Kwa nini hamna demokrasia ndani ya hivi vyama?( refer uchaguzi wa chadema)
3. Kwa nini NCCR kama wanamoyo na nia moja na Chadema kwa nini walimkaribisha Kafulila? wao ni safi kuliko chadema? (refer kafulila kuhamia NCCR), je kitendo kile watu wa kawaida si wanaona usanii fulani na kutoa conclusion kuwa hivi vyama kuna haja ya kivumulika mpaka kwenye mifupa yao???
hold on...
Zito, chadema, mbowe wenu , slaa....nccr, mrema...cuf, name it..... I real doubt naona hakuna seriousness katika vyama na watu, kiasi cha kusema why dont we think another option! utasema na kuvitetea hivi vyama mpaka unatoka mvi nyeupe kwapani wapi!!!
kisaikolojia Zitto amekuwa kwenye weak point kiasi cha kumtupia lawama zote kumbe tatizo si yeye , chama makini, chenye watu wakali na walio serious na swala linaloitwa upinzani, Zito asingepiga kelele zake hizo, siku ya pili alitakiwa awe amekwisha jiuzulu,! mbona naona ishu zile zile za CCM chadema, am I blind???
ebu tujiangalie tena