WanaJF!
Binafsi nina amini katika 'uongozi' na sio hali ya taasisi, hii ni kwa kumaanisha kuwa endapo akipatikana kiongozi bora, basi hata taasisi iwe hoi namna gani itanyooka tu na kuwa yenye tija na yenye manufaa makubwa kwa umma.
Nina yasema haya kwa kutambua kuwa hivi karibuni una tarajiwa kufanyika uchaguzi wa ndani ya CHADEMA ambao umekuwa ukifanyika kwa kila baada ya miaka mitano, hivyo mimi kama mwananchi mpenda amani, haki na usawa, nimeona nitoe yaliyo moyoni kuhusu uchaguzi huo.
Zitto ni kijana ambae amehusika kwa kiasi kikubwa katika haya mabadiliko tunayo yaona hivi sasa kwa CHADEMA na taifa kwa ujumla wake, ni kijana ambae amejitoa kuhakikisha haki ina tolewa, usawa una kuwepo na sheria zinafuatwa, na hayo amekuwa akihakikisha yanafanywa na kuonekana kufanyika.
Zitto ndiye amekuwa tanuru la vuguvugu lenye kutoa hamasa na ujasili kwa vijana kuamka na kuhoji juu ya mambo mbalimbali yanayogusa mstakabali wa taifa letu, kwani itakumbukwa vijana wengi walijiunga na CHADEMA kwa kuvutiwa na ushawishi wa Zitto, uwezo wa kujenga hoja na uzalendo wake.
Aidha, itakumbukwa kuwa Zitto ndiye aliye ifyeka njia na kuwaandalia mazingira ya kuaminiwa na wananchi hawa wabunge wapya wa CHADEMA, kwani ni Zitto ndiye aliyekuwa akiibua mambo mbalimbali ya kifisadi serikalini, hii ilijenga imani kuwa ya wananchi kwa kijana huyu na kupelekea CHADEMA kujulikana nchini.
CHADEMA (nikiwa na maana ya wanachama) kama itajivika ujasiri na kukataa hali ya kuendeshwa na kikundi cha watu wachache na ikathubutu kumpa ridhaa ndugu Zitto nafasi ya uenyekiti wa chama hicho, binafsi nitatoa kura zangu kuanzia ya urais, ubunge mpaka udiwani kwa CHADEMA bila kujali ni nani aliye simamishwa kugombea nafasi hizo (soma aya ya kwanza).
ANGALIZO: USHABIKI WA ITIKADI ZA KISIASA NI KIKWAZO KWA MAENDELEO YA NCHI.

Last edited by a moderator: