Zitto akiwa mwenyekiti; naahidi kuipa CHADEMA kura zangu zote!

Zitto akiwa mwenyekiti; naahidi kuipa CHADEMA kura zangu zote!

Umelonga mzee!!! sasa hivi hakuna kiongozi anayekubalika kama Zito hapa Tanzania. Kumbuka mada zake matukio yake mengi huongea kwa ajili ya nchi na watu wake hajali Kigoma peke yake. Kumbuka alipotofautiana na viongozi wenzake Chadema kwa kumsifia Kikwete kwamba ndiye raisi wa kwanza Tanzania kujenga barabara ya lami Kigoma kabla ya hapo hakukuwa na lami mkoa mzima wa Kigoma ukiachia km 2 tu za mkoloni.Hii inaonyesha jinsi asivyojali hata maslahi ya chama inapokuja swala la ukweli na Utanzania.NAWAASENI WATANZANIA MKITAKA MABADILIKO YA KWELI SIMAMENI KIDETE HUYU KIJANA TUMSIMIKE VINGINEVYO HAYA MATATIZO YA KILA KITU MTOTO WA BABA KAKA,SHEMEJI KABILA FULANI UKOO FULANI, DINI FULANI AMETOA KITU KIDOGO KUWA KIONGOZI AU KUPEWA MAMLAKA FULANI HAYATOISHA. TUNAKOELEKEA SASA HIVI TUNAKWENDA KUCHAPANA KWANI UVUMILIVU UNAELEKEA MWISHO. MAJESHI POLISI SASA HIVI HAYAMSIKILIZI TENA AMIIRI JESHI WAKE.TUNAKWENDA WAPI!!!!!!!!!!!!KILIO TUIKOMBOE TANZANIA
 
WanaJF!

Binafsi nina amini katika 'uongozi' na sio hali ya taasisi, hii ni kwa kumaanisha kuwa endapo akipatikana kiongozi bora, basi hata taasisi iwe hoi namna gani itanyooka tu na kuwa yenye tija na yenye manufaa makubwa kwa umma.

Nina yasema haya kwa kutambua kuwa hivi karibuni una tarajiwa kufanyika uchaguzi wa ndani ya CHADEMA ambao umekuwa ukifanyika kwa kila baada ya miaka mitano, hivyo mimi kama mwananchi mpenda amani, haki na usawa, nimeona nitoe yaliyo moyoni kuhusu uchaguzi huo.

Zitto ni kijana ambae amehusika kwa kiasi kikubwa katika haya mabadiliko tunayo yaona hivi sasa kwa CHADEMA na taifa kwa ujumla wake, ni kijana ambae amejitoa kuhakikisha haki ina tolewa, usawa una kuwepo na sheria zinafuatwa, na hayo amekuwa akihakikisha yanafanywa na kuonekana kufanyika.

Zitto ndiye amekuwa tanuru la vuguvugu lenye kutoa hamasa na ujasili kwa vijana kuamka na kuhoji juu ya mambo mbalimbali yanayogusa mstakabali wa taifa letu, kwani itakumbukwa vijana wengi walijiunga na CHADEMA kwa kuvutiwa na ushawishi wa Zitto, uwezo wa kujenga hoja na uzalendo wake.

Aidha, itakumbukwa kuwa Zitto ndiye aliye ifyeka njia na kuwaandalia mazingira ya kuaminiwa na wananchi hawa wabunge wapya wa CHADEMA, kwani ni Zitto ndiye aliyekuwa akiibua mambo mbalimbali ya kifisadi serikalini, hii ilijenga imani kuwa ya wananchi kwa kijana huyu na kupelekea CHADEMA kujulikana nchini.

CHADEMA (nikiwa na maana ya wanachama) kama itajivika ujasiri na kukataa hali ya kuendeshwa na kikundi cha watu wachache na ikathubutu kumpa ridhaa ndugu Zitto nafasi ya uenyekiti wa chama hicho, binafsi nitatoa kura zangu kuanzia ya urais, ubunge mpaka udiwani kwa CHADEMA bila kujali ni nani aliye simamishwa kugombea nafasi hizo (soma aya ya kwanza).

ANGALIZO: USHABIKI WA ITIKADI ZA KISIASA NI KIKWAZO KWA MAENDELEO YA NCHI.

Anza kwanza kufikiria nani atamrithi mwenyekiti wako wa chama kabla hujarukia vyama vingine
 
Anza kwanza kufikiria nani atamrithi mwenyekiti wako wa chama kabla hujarukia vyama vingine

kweli ukweli Unauma, mwaka 2000-2005 Mbowe alikuwa bungeni hem nambie alifanya nini? na zito kafanya nini 2005-2010! kisha kama wewe ni mzalendo utatoa majibu sahihi kabisa
 
kweli ukweli Unauma, mwaka 2000-2005 Mbowe alikuwa bungeni hem nambie alifanya nini? na zito kafanya nini 2005-2010! kisha kama wewe ni mzalendo utatoa majibu sahihi kabisa

Ukweli gani?, kwanini nini CCM mnataka sana ZZK awe mwenyekiti?, hilo suala waachieni wana CDM wenyewe watajua mbivu na mbichi, sio ww na mwenzako ambao si wanachana
 
kweli ukweli Unauma, mwaka 2000-2005 Mbowe alikuwa bungeni hem nambie alifanya nini? na zito kafanya nini 2005-2010! kisha kama wewe ni mzalendo utatoa majibu sahihi kabisa

Lowassa na JK nani alikuwa mchapakazi?,kwanini hamkumpa Lowassa uwenyekiti mkampa JK?,jibu kwanza hili swali na mimi ntajibu lako
 
Back
Top Bottom