Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi ilikuwaje mpaka Zitto akawekewa kizuizi ili asigombee uenyekiti, nikumbushe ni kikao gani kilifanyika kumkataa Zitto asiwe mwenyekiti wa CHADEMA!
Mkuu, nina ushawishi kwenye jamii, hivyo sio tu mimi ambae nitapigania CHADEMA ishinde (endapo Zitto akiwa mwenyekiti), bali hata vijana na wazee watajumuika na mimi kuhakikisha hilo linafanikiwa.
Ubakie huko huko Magambani,Huku hatukutaki!
Leo "mateja" hawana maana kwenu?, mbona mnyika alikuwa akiwasomba kwenye malori ili wakampigie kura awe mbunge wa jimbo la Ubungo?
Swali la kujiuliza; Ni kwanini Mbowe, Mtei, Ndesamburo, Dr Slaa, Lema, Mnyika Nassary et al hawataki Zitto awe mwenyekiti CHADEMA?
Nimesha tolea ufafanuzi hilo kwenye post yangu ya kwanza, nimesema Zitto ndio sababu ya CHADEMA kuwa hapa ilipo kwani alijitoa sana kwenye hicho chama, wewe soma post kuu utaelewa tu.
WanaJF!
Binafsi nina amini katika 'uongozi' na sio hali ya taasisi, hii ni kwa kumaanisha kuwa endapo akipatikana kiongozi bora, basi hata taasisi iwe hoi namna gani itanyooka tu na kuwa yenye tija na yenye manufaa makubwa kwa umma.
Nina yasema haya kwa kutambua kuwa hivi karibuni una tarajiwa kufanyika uchaguzi wa ndani ya CHADEMA ambao umekuwa ukifanyika kwa kila baada ya miaka mitano, hivyo mimi kama mwananchi mpenda amani, haki na usawa, nimeona nitoe yaliyo moyoni kuhusu uchaguzi huo.
Zitto ni kijana ambae amehusika kwa kiasi kikubwa katika haya mabadiliko tunayo yaona hivi sasa kwa CHADEMA na taifa kwa ujumla wake, ni kijana ambae amejitoa kuhakikisha haki ina tolewa, usawa una kuwepo na sheria zinafuatwa, na hayo amekuwa akihakikisha yanafanywa na kuonekana kufanyika.
Zitto ndiye amekuwa tanuru la vuguvugu lenye kutoa hamasa na ujasili kwa vijana kuamka na kuhoji juu ya mambo mbalimbali yanayogusa mstakabali wa taifa letu, kwani itakumbukwa vijana wengi walijiunga na CHADEMA kwa kuvutiwa na ushawishi wa Zitto, uwezo wa kujenga hoja na uzalendo wake.
Aidha, itakumbukwa kuwa Zitto ndiye aliye ifyeka njia na kuwaandalia mazingira ya kuaminiwa na wananchi hawa wabunge wapya wa CHADEMA, kwani ni Zitto ndiye aliyekuwa akiibua mambo mbalimbali ya kifisadi serikalini, hii ilijenga imani kuwa ya wananchi kwa kijana huyu na kupelekea CHADEMA kujulikana nchini.
CHADEMA (nikiwa na maana ya wanachama) kama itajivika ujasiri na kukataa hali ya kuendeshwa na kikundi cha watu wachache na ikathubutu kumpa ridhaa ndugu Zitto nafasi ya uenyekiti wa chama hicho, binafsi nitatoa kura zangu kuanzia ya urais, ubunge mpaka udiwani kwa CHADEMA bila kujali ni nani aliye simamishwa kugombea nafasi hizo (soma aya ya kwanza).
ANGALIZO: USHABIKI WA ITIKADI ZA KISIASA NI KIKWAZO KWA MAENDELEO YA NCHI.
ZITTO KABWE kuwa mwenyekiti wa CHADEMA ni sawa na SHIBUDA kupewa cheo cha SLAA.[#DU! SHIBUDA PANDIKIZI LA MAGAMBA uliweke kuwa mwenyekiti aisee! CDM is so keen so that's why
is still surviving/but there is a need to mixup leadership chairpersons to make the taste of nationality!must done keenly||
Zitto mnafikiKura yako mmoja inauzito gani katika hili?
WanaJF!
Binafsi nina amini katika 'uongozi' na sio hali ya taasisi, hii ni kwa kumaanisha kuwa endapo akipatikana kiongozi bora, basi hata taasisi iwe hoi namna gani itanyooka tu na kuwa yenye tija na yenye manufaa makubwa kwa umma.
Nina yasema haya kwa kutambua kuwa hivi karibuni una tarajiwa kufanyika uchaguzi wa ndani ya CHADEMA ambao umekuwa ukifanyika kwa kila baada ya miaka mitano, hivyo mimi kama mwananchi mpenda amani, haki na usawa, nimeona nitoe yaliyo moyoni kuhusu uchaguzi huo.
Zitto ni kijana ambae amehusika kwa kiasi kikubwa katika haya mabadiliko tunayo yaona hivi sasa kwa CHADEMA na taifa kwa ujumla wake, ni kijana ambae amejitoa kuhakikisha haki ina tolewa, usawa una kuwepo na sheria zinafuatwa, na hayo amekuwa akihakikisha yanafanywa na kuonekana kufanyika.
Zitto ndiye amekuwa tanuru la vuguvugu lenye kutoa hamasa na ujasili kwa vijana kuamka na kuhoji juu ya mambo mbalimbali yanayogusa mstakabali wa taifa letu, kwani itakumbukwa vijana wengi walijiunga na CHADEMA kwa kuvutiwa na ushawishi wa Zitto, uwezo wa kujenga hoja na uzalendo wake.
Aidha, itakumbukwa kuwa Zitto ndiye aliye ifyeka njia na kuwaandalia mazingira ya kuaminiwa na wananchi hawa wabunge wapya wa CHADEMA, kwani ni Zitto ndiye aliyekuwa akiibua mambo mbalimbali ya kifisadi serikalini, hii ilijenga imani kuwa ya wananchi kwa kijana huyu na kupelekea CHADEMA kujulikana nchini.
CHADEMA (nikiwa na maana ya wanachama) kama itajivika ujasiri na kukataa hali ya kuendeshwa na kikundi cha watu wachache na ikathubutu kumpa ridhaa ndugu Zitto nafasi ya uenyekiti wa chama hicho, binafsi nitatoa kura zangu kuanzia ya urais, ubunge mpaka udiwani kwa CHADEMA bila kujali ni nani aliye simamishwa kugombea nafasi hizo (soma aya ya kwanza).
ANGALIZO: USHABIKI WA ITIKADI ZA KISIASA NI KIKWAZO KWA MAENDELEO YA NCHI.
Sijasema naamia CHADEMA, nimeahidi kuipigia kura CHADEMA endapo Zitto akiwa mwenyekiti. Naomba ieleweke hivyo.
huna jipya wewew ni masalia yalotimuliwa chadema wasokujua watahangaika sana.Mkuu, mimi ni mwananchi mpenda amani, haki na usawa.