Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Ni kwa sababu hamna kipengele kinachoonyesha muda wa uhai wa mkataba ndio maana tunasema kuwa hamna muda maalum. Kipengele cha 23 kinachohusu "Duration and Termination " kinasema :Hivi ili la mkataba kutokuwa na muda maalum au kutoweza kuvunjwa; mmelitoa wapi kutoka katika yale makubaliano?
Ni article zipi hizo zinazo sema hayo. Vinginevyo kwa sababu mmeamua kuamini hivyo aina maana huo ndio ukweli wenyewe.
1. a. Mkataba utakoma pale tu ambapo miradi yote itaisha permanently. Hatudhani kama miradi ya bandari na maeneo mengine yaliyokuwemo katika mkataba itakuja kuisha maana kila siku kuna uboreshaji n.k.
b. (Na HGAs zote zitakapo expire pamoja na mikataba mingine. Hizo HGAs ndio zinahusika katika utekelezaji wa mkataba.
2. Kama HGA itakuwa terminated itaendelea kuwepo kwa muda ambao nchi zilizoingia katika mkataba zitaona unafaa.
3. IGA inaweza kuvunjwa kwa kibali cha mojawapo ya nchi zilizoingia katika Mkataba.
4. Hamna nchi inayoruhusiwa kuukana (denounce), kujitoa, ku usitisha kwa muda au kuuvunja huu Mkataba katika mazingira yeyote ikiwa pamoja na kuukiuka (material breach), madiliko ya mazingira, uvunjaji wa uhusiano wa kibalozi au sababu nyingine yeyote inayotambuliwa katika sheria za kimataifa (International law). Pamoja na haya, migogoro yeyote itatatuliwa kufuatana na kifungu cha 20 cha Mkataba ( kifungu hicho kinazungumzia usuluhishi ambao utafanyika Johannesburg. Hakitaji taasisi ipi ya usuluhishi itahusika).
Sasa wewe nitajie wapi pametaja muda katika huu mkataba ili watu wasiamini kuwa ni wa milele.
Amandla...