Zitto ashauri iundwe kampuni ya ubia kati ya DP World na Tanzania kuendesha bandari

Zitto ashauri iundwe kampuni ya ubia kati ya DP World na Tanzania kuendesha bandari

Unataka mapendekezo gani.Mko madarakani kufanya nini sasa kama mnakua hamuwezi kuongoza kwa ufanisi.yaan mnashindwa alafu unataka mshindani wako akupe mawazo yanamna yakufanya.Ukishindwa unatakiwa kukaa pembeni aongoze mwingine sio kuomba huruma zakutaka kusaidiwa.
 
..good points.

..Na Dp World ameshawekeza ktk bandari ya Kenya[lamu], Congo Drc, na dry port Rwanda.

..sina uhakika kama DP World hawaendeshi sehemu ya bandari ya Mombasa.

..huenda DP World wanataka kuwa MONOPOLY wa bandari za Africa.
Ndio lengo lao.

Amandla...
 
Serikali ingetaka msioneshwe Wala isingepelekwa Bungeni kama huko nyuma.
Mikataba baina ya nchi ni lazima ipelekwe Bungeni na ipate baraka za wananchi. Ndio maana wakatoa siku moja ya wananchi kuchangia. Serikali ililazimika ama sivyo wangefanya kama walivyofanya katika mikataba mingine. Hawakufanya kwa utashi wao. Kwa maneno mengine mkataba usingekamilika kama wabunge wasingetoa ridhaa yao.

Amandla...
 
Hiyo ni njia moja - UBIA; au basi DP World Waje kama Consultants. TPA waendeshe Bandari, kisha DP World waishauri/ kuwafundisha TPA ni jinsi gani wanaweza kupata hiyo mizigo, ikiwemo kuingia ushirikiano na wao - wakati TPA wakiwa independent, na pia ni jinsi gani ya ku-automate operations za Bandari na kuunganish hiyo mifumo ya TPA, TRA ili isomane.
 
Back
Top Bottom