Zitto ashauri iundwe kampuni ya ubia kati ya DP World na Tanzania kuendesha bandari

Hivi ili la mkataba kutokuwa na muda maalum au kutoweza kuvunjwa; mmelitoa wapi kutoka katika yale makubaliano?

Ni article zipi hizo zinazo sema hayo. Vinginevyo kwa sababu mmeamua kuamini hivyo aina maana huo ndio ukweli wenyewe.
Ni kwa sababu hamna kipengele kinachoonyesha muda wa uhai wa mkataba ndio maana tunasema kuwa hamna muda maalum. Kipengele cha 23 kinachohusu "Duration and Termination " kinasema :
1. a. Mkataba utakoma pale tu ambapo miradi yote itaisha permanently. Hatudhani kama miradi ya bandari na maeneo mengine yaliyokuwemo katika mkataba itakuja kuisha maana kila siku kuna uboreshaji n.k.
b. (Na HGAs zote zitakapo expire pamoja na mikataba mingine. Hizo HGAs ndio zinahusika katika utekelezaji wa mkataba.
2. Kama HGA itakuwa terminated itaendelea kuwepo kwa muda ambao nchi zilizoingia katika mkataba zitaona unafaa.
3. IGA inaweza kuvunjwa kwa kibali cha mojawapo ya nchi zilizoingia katika Mkataba.
4. Hamna nchi inayoruhusiwa kuukana (denounce), kujitoa, ku usitisha kwa muda au kuuvunja huu Mkataba katika mazingira yeyote ikiwa pamoja na kuukiuka (material breach), madiliko ya mazingira, uvunjaji wa uhusiano wa kibalozi au sababu nyingine yeyote inayotambuliwa katika sheria za kimataifa (International law). Pamoja na haya, migogoro yeyote itatatuliwa kufuatana na kifungu cha 20 cha Mkataba ( kifungu hicho kinazungumzia usuluhishi ambao utafanyika Johannesburg. Hakitaji taasisi ipi ya usuluhishi itahusika).

Sasa wewe nitajie wapi pametaja muda katika huu mkataba ili watu wasiamini kuwa ni wa milele.

Amandla...
 
Umeambiwa vipengele vya Ukomo vitasema wakisainiana Mikataba ya utekelezaji
 
Hivyo vitakuwa ni ukomo wa mikataba ya utekelezaji (HGA) na sio ukomo wa mkatba mama (IGA).

Amandla...
Sasa mkataba wa Ukomo wa utekelezaji si ndio automatically unaondoa IGA? Maana ikibakia na huna Cha kufanya then inakusaidiaje?
 
Bora huyu
 
Umeambiwa vipengele vya Ukomo vitasema wakisainiana Mikataba ya utekelezaji

Mkataba MAMA unasema wazi Iwapo DP itataka kurenew mikataba itakayoingia na serikali basi serikali HAITOKUWA NA KIPINGAMIZI!. Kiufupi ni mpaka DP World watakapoamua kuondoka wenyewe, lakini Sisi tumeshapigwa pini, Hatuna nguvu tena za maamuzi ya bandari yetu.
 

Hakuna alternative, kwani hii bandari ni ya kwao? Sisi tunaenda kwenye utatuzi wa juu kabisa.
 
Serikali isiwe na kipingamizi hata kama ume underperform?
 
Kamwambie aliyekutuma, moto ndio kwanza unawaka na safari hii tutahakikisha huu mkataba unawatoa madarakani tunajua jinsi mnavyomtumia Zitto kupunguza nguvu ya upinzani lakini haitasaidia
Maandamano makubwa nchi nzima yanakuja.
JIANDAENI!
 
Sasa mkataba wa Ukomo wa utekelezaji si ndio automatically unaondoa IGA? Maana ikibakia na huna Cha kufanya then inakusaidiaje?
IGA ndio msingi wa mikataba (HGA) yote itakayofuata . Ukibadilisha sheria haina maana kuwa Katiba ndio imekufa. Au ukibadilisha madirisha kwenye nyumba haina maana kuwa hauhitaji tena msingi wa nyumba yako. Msingi ukiwa mbovu hauwezi kurekebishwa kwa kupaka rangi nyumba. Hivyo hivyo mapungufu yaliyomo katika IGA hayawezi kurekebishwa kwa kupitia HGA. HGA zitaisha lakini IGA itabaki pale pale.

Amandla...
 


Pitia, article 1 definitions inakuelezea ‘project agreement’ itakuwa ni mikataba watakayoingia baadae kwenye HGA na wanakuelezea hapo hiyo IGA unayoisoma sio mkataba rasmi.

Points zako
1. Kwanza umeweka maneno mkataba auna kikomo. Wakati appendices 1 inaelezea project zenyewe ni zipi na kila moja itakuwa na muda wa ujenzi na mkataba wake, kama article 1 ya project definition ilivyoolezea.

b. Sijakupata vizuri hapo una maanisha nini haswa.

Anyway nitajibu kwa nilivyo kuelewa katika hizo project agreements. Pamoja na investments kuna management na operation rights pia ambazo zinaisha baada ya kurudisha hela zao (logically speaking).

Sasa kama wanafanya kazi vizuri wanaweza weka option ya kuomba kuongezewa muda, ikifika review time wanaweza pewa au kataliwa kama ilivyokuwa kwa TICTS na Inchape kabla yao.

2. Doesn’t even make sense, utafutaje mkataba; halafu watu hao hao waliofuta mkataba waamue kuendelezaa kwa muda wanaodhani unafaa. Issue hapa labda ni interpretation zako tu.

3. Tatu hii nayo sijui umeitoa wapi.

IGA inakufa automatic toka ipitishwe bungeni kama ndani ya miezi 12 kutakuwa hakuna project agreement yeyote iliyosainiwa (hapo wanamaanisha katika zile zilizo orodeshwa in appendices 1). In other words hiyo IGA ni kama MoU tu lakini sio mkataba.

4. Hakuna nchi inaruhusiwa kujitoa na mengineyo uliyoyaelezea kwenye hiyo sentensi ya kwanza ya article 23 (4). Sentensi ya inayofuata hapo kwenye 23 (4) inasema isipokuwa kwa kufuata taratibu zilizowekwa in article 20.

Hayo masharti utayakuta kwenye IGA ni kwa mikataba yote ya kibiashara duniani uwezi kujitoa kiholela ukifanya ivyo utashitakiwa, so kuwepo kwake hapo ni emphasis tu. Vinginevyo njia za kumaliza migogoro ya uwekezaji zimetajwa.

Kutokuvunja mkataba ata serikali kubadilika au mahusiano ya nchi yakiaribika basically hiyo ni aspect ya stabilisation clause. Kwanini huwa inawekwa kama uwekezaji wako ili hela irudi inaweza chukua zaidi ya chaguzi tatu za nchi husika na hujui huyo atakae kuja mbele atakuwa na mtazamo gani. Kwenye kulinda investment return zao za muda mrefu hiko kipengele lazima kiwepo kwa mikataba yote ya muda mrefu (ipo hivyo duniani kote). However njia sahihi ya kufuata imeelezewa itakuwa ni article 20.

Migogoro kutatuliwa S.A, ni kawaida migogoro ya kibiashara inatatuliwa kupitia arbitration ya neutral ground na mnachagua nchi pamoja maana it doesn’t matter where. Regardless huko kwenye arbitration awatumii sheria za S.A kinachoangaliwa ni terms na sheria husika zilizotumika kuingia mkataba ambazo nyingi ni za Tanzania.

Arbitrator (mtoa maamuzi) kawaida ni industry expert labda mwanasheria tu mwenye uzoefu wa hiyo mikataba husika ya bandari duniani na ata yeye mnamuidhinisha kwa pamoja kabla ya kuchukua kesi.

Conclusion

As yet bado ujaonyesha mahala panaposema mkataba ni wa milele na auwezi vunjwa.

Mi siwezi kukuonyesha muda wa mkataba kwa sababu hayo mambo yatakuwa kwenye individual project agreements na HGA; ambazo hazipo kwa sasa.
 
 
 
Cha muhimu ni uadilifu. Ilishawahi kuundwa kampuni ya TANGOLD lakini ufisadi ukafanyika wa kutisha. Hata hiyo anayosema Zitto inaweza isisaidie kama hakuna uadilifu. CHADEMA tuwaonee huruma kwasababu ni chama kilichopo kwenye mwisho wa uhai wake.
 
Hata saa mbovu inapatia mara mbili kwa siku.
Hii sio mara ya kwanza kuingia katika mikataba mibovu na kukataa kata kata kushauriwa.
Wakati tunataka kununua rada kutoka kampuni ya British Aerospace (BAE), waziri wa serikali ya Uingereza Claire Short alituasa kwa kutuambia kuwa rada hiyo haitufai na tunapigwa katika bei. Kama kawaida yetu tukakaza shingo na kuwaambia kuwa wasituingilie maana sisi ni nchi huru. Baadae Serikali ya Uingereza iliishitaki BAE na mahakama ya Uingereza ikaiamuru iturudishie pesa iliyotupiga.
Tulipotaka kununua ndege ya Rais, tuliambiwa kuwa ni matumizi mabaya ya pesa zetu. Kama kawaida tulikataa ushauri huo na kutamka kuwa tuko tayari kula nyasi ili Rais wetu awe na ndege yake.
Wakati tunajisifu kuwa tumenunua ndege kwa pesa taslimu kuna watu walisema huo sio utaratibu mzuri. Waliopinga walionekana wasaliti na kuwa wamehongwa na mashirika ya ndege yanayoogopa ushindani kutoka ATC. Leo ndege nyingi tulizonunuakwa mbwembwe zimepaki na malipo ya maitenance yanatupa shida. Lakini ili kuonyesha tullivyo ngangari tumenunua ndege nyingine pamoja na hii ya sasa ya mizigo.
Hapa sijazungumzia mikataba ya IPTL, ya mkenya aliyetuambia atanunua korosho zetu zote, ya dawa ya Covid kutoka Madagascar ( hii angalau tulipewa bure), waganga wa mvua kutoka Thailand, mashamba ya prawns katika Rufiji Delta (kelele za wana harakati ziliuzuia) n.k.
Kusikiliza ushauri haijawahi kuwa dhambi.

Amandla...
 
Serikali ingetaka msioneshwe Wala isingepelekwa Bungeni kama huko nyuma.
 

..good points.

..Na Dp World ameshawekeza ktk bandari ya Kenya[lamu], Congo Drc, na dry port Rwanda.

..sina uhakika kama DP World hawaendeshi sehemu ya bandari ya Mombasa.

..huenda DP World wanataka kuwa MONOPOLY wa bandari za Africa.
 
Kwa Mara ya kwanza awamu ya sita imeenza kunitoka moyoni...huwezi ingia mkataba Kama huo wa Dp w.na bado ukapata mapenzi ya wananchi wengi wanaongea kinafiki tu Ila inaumaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…