Zitto ataka wanaoikosoa ACT-Wazalendo waanzishe chama chao

Zitto ataka wanaoikosoa ACT-Wazalendo waanzishe chama chao

Tulisema sana humu kuwa Zitto haaminiki hata mara moja! Huyu ni mtu wa maslahi zaidi na sio mpinzani wa dhati hata kidogo
 
Tulisema sana humu kuwa Zitto haaminiki hata mara moja! Huyu ni mtu wa maslahi zaidi na sio mpinzani wa dhati hata kidogo
Kuwa mpinzani maana yake nini? Kila chama kinapigania kuingia ikulu, kimepata nafasi ya kuingia ikulu mnataka kikatae ili iweje?
 
Ruzuku inatokana na " kura " mlizopata kwenye uchaguzi mkuu.

Hivyo kama uchaguzi ni batili na ruzuku unayopokea ni haramu vile vile
CDM wanasema ni batili kwa sababu walidhulumiwa kura kwa hiyo walistahili kupata ruzuku zaidi ya hiyo watakayopewa. Na kama nilivyosema ruzuku inatokana na kodi inayolipwa na wakazi wote wa Tanzania na sio wanachama wa CCM peke yake.

Kutaka wasichukue ni kama vile mnavyotaka wasipande ndege ambazo wamechangia kununua kwa sababu tu hawakukubaliana na uamuzi wa kuzinunua.

Amandla...
 
CDM wanasema ni batili kwa sababu walidhulumiwa kura kwa hiyo walistahili kupata ruzuku zaidi ya hiyo watakayopewa. Na kama nilivyosema ruzuku inatokana na kodi inayolipwa na wakazi wote wa Tanzania na sio wanachama wa CCM peke yake. Kutaka wasichukue ni kama vile mnavyotaka wasipande ndege ambazo wamechangia kununua kwa sababu tu hawakukubaliana na uamuzi wa kuzinunua.

Amandla...
Ahaa kumbe tatizo siyo uchaguzi bali kiasi cha ruzuku?

Wabunge 20 si haba kwa ruzuku!
 
Akili ya ubwabwa, pole.

Alisema kuwa chadema inapinga akina mdee kuingia bungeni ilihali ruzuku wanayopewa chadema ni pamoja na inayotokana na uwakilishi wa akina mdee. Meanwhile, kama ubunge wa akina mdee ni haramu basi chadema ikatae ruzuku inayotokana na wabunge viti maalum yaani akina mdee.
Hatuzungumzii mpira hapa. Wakina Mdee wamefukuzwa katika chama chao sio kwa sababu tu ya kuwazuia kuingia kwenye bunge ambalo wanaona ni haramu. Wao wamezuiwa kwa sababu hawakufuata taratibu na walienda kuapishwa bila ridhaa ya chama chao. Aidha, kwa sababu ruzuku haitokani na maamuzi ya Bunge basi haihusiki na Bunge lililopo.

Amandla...
 
Ahaa kumbe tatizo siyo uchaguzi bali kiasi cha ruzuku?!!

Wabunge 20 si haba kwa ruzuku!
Tatizo ni namna uchaguzi ulivyoendeshwa na kiasi cha kura ambazo inasemekana vyama vyote vilipata.

Aidha, una ushahidi gani kuwa CDM wamepewa na kupokea ruzuku?

Amandla...
 
Lengo la sasa la Zitto ni kukuza chama
Kutoka mbunge mmoja Hadi sasa kutoa makamu Zanzibar...


Mengineyo yote ni siasa
Zitto keshapata mileage kisiasa so far

Kutoka kupigwa vita na CHADEMA
Hadi kupigiwa kampeni na Chadema
Wewe umewaza kama mimi.
 
Hii mileage ya kukaa meza moja na wauaji haitamfikisha popote kwani uongo wake, unafiki na kuweka mbele maslahi binafsi vinajidhirisha tena kwa nguvu sana. Kwenye uchaguzi huru na wa haki huyu hatapata chochote labda “aahidiwe” kupewa viti 25 to 35 ili kumuwezesha kupata RUZUKU. Kule Twitter Zitto, Shariff Hamad, Nassor Mazrui na wengi wengineo wa ACT wamekimbia maana madongo wanayopigwa si ya kawaida. Watanzania wa 2020 si wale wa mwaka 47.
Lengo la sasa la Zitto ni kukuza chama
Kutoka mbunge mmoja Hadi sasa kutoa makamu Zanzibar...


Mengineyo yote ni siasa
Zitto keshapata mileage kisiasa so far

Kutoka kupigwa vita na CHADEMA
Hadi kupigiwa kampeni na Chadema
 
Nimeshangazwa na majibu ya mkuu wa chama cha ACT Wazalendo ndugu Zitto Kabwe aliyoyatoa kwenye mtandao wa twitter.

Zitto alikuwa akimjibu mwananchi mmoja aliyekuwa akionyesha frustrations zake juu ya uamuzi wa chama cha ACT kujiunga na Serikali ya CCM huko Zanzibar katika kile kinachoitwa serikali ya umoja wa kitaifa. Mwananchi huyo anaonyesha kuwa kuingia kwa ACT katika hiyo serikali hakuwezi kusaidia wananchi kupata uhuru mpana waliokuwa wakitamani kuwa nao.

Katika hali isiyo ya kawaida, isiyo ya uungwana na isiyo ya kiuongozi mkuu wa chama cha ACT ndugu Zitto badala ya kutumia fursa hiyo kumuelewesha au atleast akae kimya wananchi watumie haki yao ya kutoa maoni, yeye anamjibu kwa ufedhuli na jeuri kuwa "Kama unaona tumekosea basi anzisha chama chako".

Kwa kweli sikutegemea kiongozi haswa wa upinzani kutoa majibu ya nyodo kama haya kwa wananchi wanapouliza maswali ya msingi juu ya mienendo ya kisiasa nchini.

Labda Zitto afahamu tu kuwa sababu mojawapo ya leo ACT-Wazalendo kuwa hapa ni haohao wananchi ambao leo anawajibu kwa nyodo kuwa "anzisheni chama chenu"

Lakini pia Zitto akumbuke kuwa kuna watu wamekifia hicho chama, Wakati akijibu kwa majibu ya "Anzisheni chama chenu" Je amelifikiria hili kuwa kuna watu wame-pay ultimate price kwa hicho chama au kwa course yake waliyoinadi kwao na kwa hiyo ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wana haki ya kuhoji ukinyongakinyonga wa misimamo iliyowafanya hapo awali wawe tayari kukipigania hicho chama?

Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida, Viongozi wa ACT sasa hivi wameacha kujibu maswali magumu ya wananchi juu ya hatua yao ya kuingia kwenye SUK wakati waliitangazia dunia na nchi kiujumla kuwa uchaguzi uliopita ulikuwa haramu, Zitto mwenyewe akaweka saini tamko la pamoja la Upinzani kuwa hawautambui uchaguzi ule pamoja na natunda yake, Sasa leo wananchi wakihoji wanaambiwa jamani eeh kama hamtaki tulichokifanya basi nendeni CCM, au NCCR yaani ni majibu ya kifedhuli uliopitiliza!. Sasa wameacha kutoa majibu kwa wananchi, wameanza kublackmail wanachama wa ACT na kutoa kauli za nyodo kwa wananchi, kuwa "ACT ina wenyewe na nyie kaanzisheni chama chenu"

Sasa leo tunaona kwa macho yetu, watu tuliodhani ni wakomavu wa kisiasa, tuliodhani kuwa mashambulizi yao kwa CCM basi wao labda wana ngozi ngumu na kwamba labda wao wakipewa nchi basi watakuwa humble, watakuwa na humility, watajibu hoja kwa hoja kumbe hawa jamaa ni arrogant(wenye viburi), intolerant(wasio wavumilivu) na wanajiona wao ni wamiliki wa taasisi kwa kuwa walizianzisha na si wahudumu tu wa taasisi ambazo wao ni wanachama.

Hawa wapinzani hawana blank cheque ya kutuletea jeuri sisi wananchi, Kwa miaka mingi tumekuwa tukiishabumbulia CCM, lakini na wenyewe hawana impunity, tutawaekeza ukweli maana hivyo vyama kwa namba moja au nyingine vinanufaika kwa jasho la wananchi iwe kwa ruzuku au wanasiasa wao kulipwa kwa kodi za wananchi n.k

Zitto acha jeuri kwa wananchi, Jibu hoja na frustrations zao kwa hekima, utulivu, nidhamu na utu. Bila wananchi usingekuwa hapa kuwa na humility.

Hebu kwanza tumsikilize Zitto wa baada ya uchaguzi kisha tusome kuhusu Zitto wa sasa na tweet zake za nyodo kwa wananchi:

View attachment 1649528

Kisha tazama majibu yake ya sasa mwezi mmoja na nusu tu baada ya uchaguzi:
View attachment 1648516

Na mahali pengine anamjibu mwananchi hivi:

View attachment 1648775

Pia ameanza kublock watu wanaomcriticize mitandaoni:

View attachment 1649138
Uhuru gani tena wanaoutaka hao wanaomkosoa?
 
Mwenzenu kapigwa begi la hela sasa hivi anasubiri korina iishe aende kula raha ulaya,Dubai & Marekani
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Unafiki wa Zitto baada ya kununuliwa na maccm. Siku hizi amekuwa mwanaharakati wa issue za Uganda na Tigray ya hapa kwetu hayamuhusu tena baada ya kushikishwa mshiko wa uhakika na hivyo kupigwa MARUFUKU kuongezeka chochote kuhusu udhalimu na wizi wa wa October 28.

 
CCM itatolewa madarakani na mtu weak. Huyo wanaweza kuzungumza naye, lakini ukiwa ngangari mwisho wake utakimbia nchi kama akina Kambona na kushindwa kabisa hata kile kidogo ambacho ungewafanyia wananchi.

Hiki chama tawala kuna mbinu zake za kuweza kuzungumza nacho vinginevyo hufiki mbali. Waliposema wataingiza wananchi barabarani, niliikataa kabisa mbinu hiyo kwani isingefanikiwa kwa jinsi chama tawala ninachokifahamu.

Maalim na Zitto ni wanasiasa wenye IQ kubwa sana, ndio maana akina mimi tunashindwa kuwaelewa. Hivyo maamuzi waliyoamua ya kuingia SUK yalikuwa sahihi kabisa. Mwaka 2025 ndio tutajua nani alichagua na kupanga kete vizuri.
Unazungumzia hisia ambazo hata maalim na Zitto hawawezi kukuamini. Siasa ni kujenga trust kwa wananchi sio kujenga tumbo lako. Hata wa Wazanzibar leo hawamwamini tena Maalim. Ni bahati mbaya ndo hatashiriki tena siasa za kuchaguliwa, ninaamini. lakini, angekuwa na umri wa kugombea 2025 ninakuhakikishia ni watu wachache sana angewakokota, wengi wameishamshtukia. SUK ilikuwepo kabla ya Maalim na Zitto kuungana na Chadema na vyama vingine kuharamisha uchaguzi na kuzitaka jumuiya za kimataifa kuishughulikia serikali ya CCM. Leo Maalim na Zitto hawaaminiki tena hata kwenye jumuiya za kimataifa! Hiyo IQ unayoisema iko kwenye matumbo yao haipo katika shida za wananchi!
 
Back
Top Bottom