Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Kupokea ruzuku ni sawa na kujiunga na serikali uliosema hauitambui? Ninavyo jua mimi ruzuku inatokana na kodi ambazo hata wanachama wa CDM wanalipa. Kwa mtaji huo, ulitaka CDM wakatae pia kulipa kodi kwa sababu hawatambui serikali iliyopo?Zitto Kabwe yuko sahihi!
Chadema usoni mnajifanya kukomaa lakini ruzuku ya wabunge wa viti maalumu mnapokea!
Kupokea ruzuku ni tofauti kabisa na kiongozi wa Chama kusimama na kutambia jinsi anavyopanda gari la kifahari na kulindwa na askari walewale ambao majuzi tu alikuwa anawashutumu kuwa walikuwa wanawakamata na kuwatendea maovu wanachama wa chama chake. Mbaya zaidi anafanya hivi bila kuwaambia namna gani serikali yake itakavyo shughulikia maumivu ambayo wanachama wa chama chake walipata.
Amandla...