Zitto ataka wanaoikosoa ACT-Wazalendo waanzishe chama chao

Zitto ataka wanaoikosoa ACT-Wazalendo waanzishe chama chao

CCM siyo Saccos bali Chama cha Siasa Cha Wanachama tofauti na Vyama vya Upinzani ambavyo ni mali na watu siyo vya wanachama.
ingekuwa saccos msingekuwa mnatumia mabilioni kuiangamiza kuwabambikia kesi kuwapiga risasi uonevu unyanyasaji uovu mateso manyanyaso na kila mbinu za kuwadhoofisha ikiwemo kuubaka kuunajisi kuulawiti uchaguzi mkuu kwa njia haramu za kishetani
 
Hii ndio silaha inayotumia na Vyama vya Siasa Dhaifu kwa Wanachama wao Dhaifu ,ounde wanapoanza kuonesha kuwa na Mawazo tofauti....mojjawapo Ni CCM ..ndio maana majority wapo ndani wanaona Mambo yamevurugika lakini hhawatoki!
Safi Sana[emoji23][emoji23][emoji23]
Ukiona chama hakikufai ondoka, kaanzishe chako.
 
Ni bilion 10 tu, kwa mfano yeye akiweka kibindoni bilion 2, halafu nane zilizobaki akawagawia genge lake ili wamuunge mkono watulie wewe huoni kuwa inawezekana kabisa?
Jiwe anafahamika kuwa ni mwepesi wa kupenyeza rupia ili kutuliza upinzani mkali mfano mmojawapo ni jinsi alivyomtuliza Mange kwa mpunga mrefu
Kumbuka kuna ile trilion 1.5 ilipotea mpaka wakamtoa CAG kafara, hiyo ni sehemu ya zile pesa wanazopiga kifisadi zikiwemo 10% ununuzi wa Ndege na 10% kwenye tenda za SGR, flyover, bwawa la umeme na miradi yote mikubwa
 
Halafu atalalamika Magufuli dikteta?

Nyerere aliandika kijitabu kinaitwa"Argue, Don't Shout: An Official Guide On Foreign Policy By The President".

Aliwapa mabalozi wote wakifuatishe.

Maudhui makuu yalikuwa, wawakilishi wa nchi wanatakiwa kujenga hoja, si kufoka kwa kelele.

Zitto is shouting, not arguing.

Furthermore, he lacks the grace and good judgement to know when to reply and when to stay silent.

He has no savoir faire!
 
Halafu atalalamika Magufuli dikteta?

Nyerere aliandika kijitabu kinaitwa"Argue, Don't Shout: An Official Guide On Foreign Policy By The President".....
He's become arrogant with only one toothless seat in Zanzibar, I don't know how it would have turned out had his party been declared a winner in Zanzibar, he wouldn't listen to anybody!
 
Ukweli kilichofanywa na Zito na Maalim Seif, ni usaliti mkubwa, ubinafsi, hadaa, unafiki, kejeli na uharamia mkubwa kwa wananchi wa Zanzibar...
Point, ndo maana kuliko kuipigia ACT kura ni Bora mtu aipigie CCM, najiuliza ni ahadi ngapi alizopewa Mandela ili aachiwe na akazikataa kutoka kwa makuburu

Kwenye siasa kitu Cha kwanza ni msimamo na hiki zitto hana
 
He's become arrogant with only one toothless seat in Zanzibar, I don't know how it would have turned out had his party been declared a winner in Zanzibar, he wouldn't listen to anybody!
Anawafanyia arrogance wananchi ambao anawahitaji kujenga chama chake, hapo anajionesha.

1. Hana strategic thinking. Kwa wanasiasa, wananchi ni watu wa kuwaonesha unawajali.Kusema mtu aanzishe chama chake ni kuonesha humjali.Ni kama mfanyabiashara kumwambia mteja aende duka lingine au aanzishe duka lake. Hata wateja wengine wanaposikia kauli hiyo, wanaona mfanyabiashara huyu hajali wateja.Hii kauli kapewa mtu mmoja lakini imewafikia mamilioni ya watu.

2. Hana self control ya kudhibiti majibu ya hamaki. Wanasiasa ni watu, na wanahamaki.Ila hawaruhusiwi kuonesha hamaki zao hadharani.

3. Hajaonesha uelewa kwamba, si kila hoja tofauti inatakiwa kumalizwa kwa chama kipya kuanzishwa.Ingekuwa hivyo, kila chama kingepasuka mara nyingi kila mwaka.

4. Amejionesha yeye kama mmiliki wa chama.Hakuna mtu mmoja anayemiliki chama. Kauli hii ni ya kidikteta.Mimi huwa nasema nchi yetu ina matatizo mengi ya kisiasa, ukiwamo udikteta wa watawala.Lakini, watawala hawana hatimiliki ya udikteta.Hawana monopoly ya udikteta.Inaonekana tuna utamaduni wa kuwa na viongozi madikteta kwenye chama tawala na hata upinzani.

5.Inawezekana kabisa kuna habari nzito anazoona zitafichuliwa na majibizano haya, ndiyo maana kaamua kuyakata kwa jazba.Mara nyingi mtu anapokata maswali kwa jazba huwa anaficha kitu ambacho anaona kitaibuliwa na maswali hayo. Zitto anafaidika nini na muafaka huu? Kahongwa nini?
 
Anawafanyia arrogance wananchi ambao anawahitaji kujenga chama chake, hapo anajionesha....

Kwenye point yako ya 5 nahisi kuna mlungula, a.k.a rushwa au kununuliwa kumetembea kwenye ile move ili ACT iingie ndani ya Serikali huko Zenji . Serikali ya Jiwe ilikuwa inawahitaji ACT waingie huko ili kupunguza kelele na presure ya mataifa makubwa kwa serikali yake!
 
They will never get peace kwa kusaliti big course

Yaani hawa jamaa wameiondolea serikali ya CCM pressure kubwa ya ndani ya nchi na hata ya nje ambayo ingewaminya wafanye reforms fulanifulani za msingi.....
Zitto ni weak sana, na ni mtu ama wa papara asiye na utulivu katika kuyaendea mambo au anatumika. Kupata uhakika zaidi ni suala linalohitaji kufanyiwa kazi zaidi, kwa kuanzia na hili!

Kwamba Zitto ni weak hili sio jambo la kubishaniwa. Na kwamba hana utulivu nalo liko wazi ukifuatilia matukio ya nyuma. Hata alivyomdaka Membe ni matokeo ya kukosa utulivu, ingawa hili linaweza kuwa na sura nyingi.

Majibu ambayo Zitto anayatoa sasa yanamchora sasa kama mwanasiasa asiyestahili kupewa nafasi ya juu kabisa kwenye chama. Udhaifu wake umekifanya ACT kitekwe. Yeye mwenyewe hapo alipo kishakuwa mateka!
 
Kwenye point yako ya 5 nahisi kuna mlungula, a.k.a rushwa au kununuliwa kumetembea kwenye ile move ili ACT iingie ndani ya Serikali huko Zenji . Serikali ya Jiwe iilikwa inawahitaji ACT waingie huko ili kupunguza kelele na presure ya mataifa makubwa kwa serikali yake!
Kwa ngangali aliyokuwa kaweka Maalim Seif, mgogoro huu bila mlungula ulikuwa haumaliziki kirahisi hivi.

Tatizo, wanachama hawajapewa mgao, na hivyo si rahisi kuelewa.
 
Zitto ni weak sana, na ni mtu ama wa papara asiye na utulivu katika kuyaendea mambo au anatumika. Kupata uhakika zaidi ni suala linalohitaji kufanyiwa kazi zaidi, kwa kuanzia na hili!...

Wazanzibari wamempora Chama, pale alipo hana tofauti na jinsi alivyokuwa mzee Maganja kabla hajahama ACT.
 
Hata wewe haulewi maana ya dola milion 5 USD unataja tu namba, laiti ungeelewa usingeamini kirahisi hivyo kwamba Serikali inaweza kumpa Zito Kabwe hela zote hizo, for what ?
We jamaa una mikwara halafu mjinga sana haya zibadilishe hizo pesa kuwa pesa madafu halafu uone zinkuwa shilingi ngapi...... CCM kweli hamna akili kabisa.
 
We jamaa una mikwara hafu mjinga sana haya zibadilishe hzo pesa kuwa pesa madafu hafu uone zinkuwa shingap......CCM kweli hamna akili kabisa.

Hata nikibadilisha bado itakuja namba tu ambayo bado hauilewi vile vile ina maana gani, ...
 
Zitto ni weak sana, na ni mtu ama wa papara asiye na utulivu katika kuyaendea mambo au anatumika. Kupata uhakika zaidi ni suala linalohitaji kufanyiwa kazi zaidi, kwa kuanzia na hili!...
CCM itatolewa madarakani na mtu weak. Huyo wanaweza kuzungumza naye, lakini ukiwa ngangari mwisho wake utakimbia nchi kama akina Kambona na kushindwa kabisa hata kile kidogo ambacho ungewafanyia wananchi.

Hiki chama tawala kuna mbinu zake za kuweza kuzungumza nacho vinginevyo hufiki mbali. Waliposema wataingiza wananchi barabarani, niliikataa kabisa mbinu hiyo kwani isingefanikiwa kwa jinsi chama tawala ninachokifahamu.

Maalim na Zitto ni wanasiasa wenye IQ kubwa sana, ndio maana akina mimi tunashindwa kuwaelewa. Hivyo maamuzi waliyoamua ya kuingia SUK yalikuwa sahihi kabisa. Mwaka 2025 ndio tutajua nani alichagua na kupanga kete vizuri.
 
Kwa hiyo kwa akili yako finyu ya matope unataka kuaminisha watu kuwa Zitto ameongwa dola bil 10? Bwege na kubwa jinga,yaani bil 10 apewe mtu kisa SUK!
Wewe Akili finyu ni kuona kuwa Zitto hajapewa hizo pesa wakati kapokea tayari, wewe ndiyo bwege na kubwa jinga unatetea upumbavu hutaki kukemea ununuzi wa wapinzani kwa njia haramu za kishetani
 

Nimeshtushwa sana naingia tweeter nakuta hii tweet ya Zitto Kabwe. Sikutegemea kama angeweza kuandika kitu kama hichi.


View attachment 1649184

Kwa mazingira haya, ni wazi kwamba Zitto anaichukulia ACT kama mali yake binafsi kama nyumba na gari lake, na ana uwezo wa kuamua na kufanya chochote bila kuingiliwa.

Binafsi nawaonea sana huruma wale wanajitia ACT kindakindaki. Wanamshutumu bure Mbowe, sijawahi ona ka tweet pumba kiasi hiki.

Kuna siku mtashangaa ACT imekuwa registered kama Chattle ya kuombea mkopo benki... Maana ni mali ya mtu binafsi.
 
Back
Top Bottom