Zitto ataka wanaoikosoa ACT-Wazalendo waanzishe chama chao

Siasa za Kibongo ni futuhi tupu. Zitto kutoka kuhukumiwa kifo na WanaCCM hadi kuwa kipenzi namba moja cha WanaCCM!
 
Kwa nini unashangaa Mkuu? Ni wewe peke yako tu unayedai kushangaa. Alichosema Mhe Zitto ni msimamo wa ACT tangu zamani. ACT ni sawa na laundry, mashine ya kutakatisha madhambi.

Jiulize: Waarabu walipofukuzwa CUF na Professor Lipumba, lakini, badala ya kuanzisha chama chao cha hizbu (wananchi), wakanunua cha Zitto. Pia utakumbuka Membe kafukuzwa CCM badala ya kuanzisha chake, kaenda kwa Zitto. Kuna vyama 23 vya siasa vimesajiliwa, Membe na Waarabu wa CUF wangeweza kuchagua kimoja wapo, lakini dau la Zitto likashinda. Kuna
Lowassa mwaka ule alikuwa na dilemma hiyo hiyo, aende CHADEMA au NCCR Mageuzi au ACT? Dau la Chadema likashinda and the rest is history.

Zitto anasema "kuna vyama vingine 22, kama hutaki changu ongeza dau tupambane". Sasa hivi Zitto hana Ubunge wala udiwani Bara, wala hata viti maalum. Kula yake itabaki kulekule Visiwani kwa Waarabu waliotoka CUF, lazima atakuwa anakatiwa kitu kidogo walau kuendesha headquarters. Je, iwapo akiamua kujitoa, atakula wapi?
 
Mkuu Missile of the Nation kama utakuwa na kumbukumbu nzuri nafikiri ilikuwa ni mwezi wa saba mwaka huu,wewe na mimi tulipishana lugha hapa hapa jukwaani juu ya uadilifu wa baadhi ya viongozi wa ACT wazalendo.

Ulikomaa sana na kuwasifia sana kina Membe na Zitto juu ya uadilifu wao na ukatuaminisha jinsi walivyo kuwa committed ili kuwatumikia wananchi kama chama kikuu cha upinzani.


Leo hii nafurahi sana umegundua nini nilikuwa namaanisha hasa juu ya ngozi halisi ya Zitto kwenye siasa za upinzani hapa nchini kwetu.
 
"Asiyemtaka Lowassa ni mchawi, aondoke CHADEMA” - Mbowe, July 2015.
Naona safari hii umelambishwa shubiri,umetupwa kama ganda la muwa lisilo na thamani.

Hutokaa uisahau CCM ya kina ngosha, sasa kaa chini utulieze akili yako ili ulee watoto wako wasiyo na baba.
 
Kila siku huwa nawambia humu kuwa Zitto ndiye mwanasiasa mchumia tumbo namba Tanzania hamuamini. Kumbe chama ni mali yake na si taasisi ya umma.
 
Tulivyo mfukuza CDM watu walitokwa na mapovu lakini tulikuwa na maana kubwa sana, maana kunguru hafugiki.
 
Katika hili Zitto hana majibu ya kuwashibisha wananchi, kwahiyo lazima atajibu pumba tu. Majibu hana atajibu nini unafikiri?
 
Kukosolewa ni Jambo la kawaida hata nyumbani na kazini au popote hasa kwenye uongozi
Sasa yeye hataki.
 

Kuna makosa madogo madogo ya kisiasa ambayo wanasiasa hufanya na hayo yanasameheka kwa haraka, Lakini pia kuna makosa makubwa ambayo si rahisi kusameheka kiuraisi kwa sababu yanarudisha nyuma jitihada za kujenga Taifa lenye utawala bora zaidi, haki za binadamu zaidi, demokrasia pana zaidi etc

Ukweli ni kwamba ACT wamewahi kufanya kazi nzuri sana ya kuibana serikali ya Magufuli kwenye issues nyingi za mambo ya uchumi, kisiasa, kisheria n.k Zitto alijitahidi kufanya kazi kubwa na nzuri ya upinzani kipindi ambapo Lissu alikuwa huko nje akitibiwa, hatuwezi kumnyang'anya credi kwa hilo, na Ukweli ni kuwa ACT ilikuwa inaenda vizuri sana hadi tarehe 28 mwezi wa 10 mwaka huu, na kwa maoni yangu kilikuwa ni chama kizuri sana kwa kusimamia misingi mizuri .

Ila kitendo cha kureverse gains zote ambazo wapinzani walishaanza kuzipata kwahatua mbalimbali za kuiweka mtu kati serikali ya Magufuli kutokana na matendo yake ya kuharibu demokrasia na kuendesha nchi bila kufuata utawala wa sheria hilo limetunyong'onyesha sana wale tuliokuwa tukiona kuwa hiki chama kina ajenda makini


Lakini hili la kujiunga na SUK wamekosea mno, na pia majibu haya ambayo Zitto anatoa si majibu mazuri na tunamkemea kwa majibu hayo!
 
Sisi tumeishi na Zitto ,tunamfahamu sana Zitto hasa linapofika suala la maslahi.
 
Labda unajidanganya wewe kiukweli Mh. Maalim Seif amechoka kilichobaki ni ujuzi tu wa kisiasa kwani ujuzi hauzeeki.
 
Siyo Zitto alitaka maandamano aliyetaka maandamano hajanunuliwa na CCM, pia ukumbuke maandamano yalipangwa tarehe 2 lakini tarehe 1 siku moja kabla Polisi kwa amri ya CCM wakawakamata viongozi wa CHADEMA, maandamano yalikuwepo lakini Polisi wakayazuia kwa uoga wao tu.
 
Sipati picha watu 100 wakaanzisha vyama vyao...
 
Kama Wewe una haki ya kuuliza chochote basi tambua pia una wajibu wa kupokea majibu yoyote

Huwa simkubali kabisa huyu Mkongo ila ninatambua ana haki nae kujibu anachoona sahihi cha msingi asitukane tu!

Hakuna Chama chochote cha Upinzani hapa Nchini kinaweza kukataa offer ya kuunda Serikal ya Umoja wa kitaifa, kinachotokea ni kijicho tu

Kuna watu walipopewa fursa ya kuhudhuria sherehe za Uhuru zilizofanyika Mwanza Mwaka Jana waliipokea kwa Mikono miwili na Mbowe alihudhuria akamshukuru sana Rais, Zitto aliikosa fursa akakakejeli sana na kuwaita wenzie wame legeza msimamo na kujiona Mwamba … Safari hii kapata Zitto waliokosa wanamkejeli Zitto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…