Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
"Ni kama watawala wetu wanatamani the Chinese way. Wanatamani eh mfumo wetu ungekuwa kama CCP, the Chinese Communist Party. Ninavyoona.
Lakini wale China, pamoja na kwamba ni chama kimoja, eh kwanza hawana mchezo na ufasadi. Juzi mawaziri wao wawili wa ulinzi wamenyongwa. Mawaziri wawili wa ulinzi! Defense Minister China ni the highest position. Ukiweka wizara ya mambo ya nje, wizara ya fedha, wizara ya ulinzi... ndio wizara ambazo any of them anaweza akawa Rais wa China. Wawili wamenyongwa!
Kazi kama mnataka the Chinese way, mkubali meritocracy. Mkatae uchawa. Huwezi kuwa na uchawa na the Chinese way, huwezi kupata vyote.
Kama unataka the Chinese way—unataka CCM ndio iwe chama pekee peke yake, kidhibiti kila kitu, jeshi liwe la CCM, usalama ndio wa CCM, polisi ndio wa CCM—basi, lazima muwe na meritocracy. Watu wapate nafasi kutokana na uwezo. Huwezi kuwa na the Chinese way alafu kuwe na uchawa, haiwezekani. Havendani.
So, it's a hard choice they have to make. Kwa hiyo ni jambo ambalo... sasa sisi tulishachagua since 1992, hapana sisi hatuendi njia ya China. Sisi tunakwenda njia ya mfumo wa vyama vingi. Maana yake ni kwamba ni lazima muwe mmejiandaa kisaikolojia, wakati wowote chama chochote kinaweza kikakuwa madarakani."