Zitto anasema kweli na kweli tupu! Kwa nini wale wanne wa NCCR waliondoka Chadema? Jibu: wameona ni chama kinachoendeshwa Kidikteta na Kidini, kama ni muIslam huna thamani Chadema, kama yanayomkuta Zitto sasa hivi na karibuni tutasukia Arfi nae hayo hayo.
..chadema walili-mishandle suala la kafulila na wenzake.
..waache kuhangaika na majimbo yaliyochukuliwa na nccr.
..wanachopaswa kufanya sasa hivi ni kujaribu kupokonya yale majimbo yaliyochukuliwa na ccm.
Watu wa kigoma wote uraia wao una utata na ndio maana watata...kazi ubishi tuu na kujiona wanajua kila kitu,kajitu kafupi,kichwa kibaya...aagh...taabu kwelikweli
Kwanza kabisa siamini kama Zitto alisema hivyo. Hata hivyo Zitto siku hizi haaminiki sana maana ana tabia ya kutoa matamshi yanayotiliwa mashaka. Kama kweli ametamka hivyo, yeye ndiye anayetakiwa kutoa majibu sababu ya hilo kutokea.
Kama Zitto hakutoa matamshi hayo basi ni mbinu zile zile za kutaka kukivuruga Chadema na mwanya wameuona kuwa unapatikana kwa kupitia Zitto. Wakati mwingine tunaweza kuamini kuwayeye amekubali kutumika kuhujumu Chadema.
Kuhusu kauli ya Zitto kuwa wabunge 4 wa NCCR kutoka mkoa wa Kigoma ambao wametokea Chadema na hivyo mwaka 2015 kunaweza kukawa na uwezekano wa kutokuwa na mbunge wa Chadema ninaona yafuatayo:
1. Inaaminika kuwa Zitto mwenyewe ndiye aliyewasaidia watu kama kina Mh. Kafulila katika kupata ubunge kupitia NCCR. Ni yeye Zitto aliyeahidi kuwa atamsaidia Kafulila katika kampeni. Hili liliwafanya watu kujiuliza itakuwaje pale Chadema itakapomsimamisha mgombea ubunge katika Jimbo hilo hilo ambalo Kafulila anagombea kupitia NCCR? Ni wazi naibu katibu mkuu wa Chama anapotoa matamshi ya kumsaidia mbunge wa chama kingine hata kama ni cha upinzani bila sababu zinazoeleweka tafsiri yake ni kukihujumu chama. Ikumbukwe kuwa Kafulila kabla ya kuondoka Chadema aliwahi kumpigia debe Zitto wakati anawania Uenyekiti wa Chadema. Hivyo Zitto alikuwa sababu ya hao wabunge wa NCCR kuondoka toka Chadema.
2. Kuna mwenekano wa haraka ambao unaweza kutafsiriwa kuwa Zitto ana lengo la kuendelea kuleta chokochoko ndani ya Chadema ili awe na sababu ama ya kuondolewa( kitu ambacho ni kigumu) au kujiondoa mwenyewe. Baada ya kuondoka Chadema atakuwa amejiandilia mahali pa kutua. Hapo anaandaa mazingira.
3. Zitto anaonekana kujaribu kila mbinu ambayo inawezeka kufanya kazi katika kufikia malengo yake binafsi aliyonayo. Kila mara anataka watu wasahau kitu kimoja pale anapoleta kitu kipya. Bado mashaka yetu yataendelea kuwepo kuhusu mambo ambayo Zitto anayafanya na malengo yake katika Chadema.
Zitto usijihangaishe sana, kama una mapenzi ya kweli kwa Chadema tutayajua tu lakini mpaka sasa huaminiki. Hili wala lisihusianishwe na dini ya Zitto maana suala la udini limeonekana kama mtaji wa kuvuruga Watanzania na hasa pale Chadema ilipohusishwa na Ukristu. Kutokuaminika kwako kunaonekana katika baadhi ya matendo na maneno yako. Mifano michache ikiwa: moja, kukubali kuwa kwenye kamati ya rais ya madini. Tulihoji kama unaweza kuleta matunda yoyote kwani kamati hizi zilieleweka kama mbinu ya kuwapumbaza Watanzania. Hadi leo matunda ya kamati hiyo hatujayaona. Pili, ukasema Dowans inunuliwe. Wewe kama mpinzani na unaelewa kuwa Dowans ni dada yake Richmond. Iweje tuikatae Richmond lakini tuipokee Dowans? Hoja hiyo ilipingwa na baadhi ya wabunge wa CCM, huoni ulikuwa kioja? Hiyo Dowans hatuwafahamu wamiliki wake ingawaje wengine wanasema ni dili ya mafisadi watatu.Tatu, juzi juzi mlipiga kura kuhusu uamuzi wa kutoka bungeni JK atakapoingia na wewe ukapingana na uamuzi wa kikao cha kidemokrasia. Baada ya hapo ukaendelea kuropoka kwenye vyombo vya habari kwamba wewe unamheshimu JK ndiyo maana hukukubali uamuzi wa Chama chako. Jk na Chadema nani unamheshimu zaidi?
Amesema Chadema ifanye tathimini, yeye sio Chadema?
Nina wasiwasi na habari yako mkuu, source pls!
Jana naibu katibu mkuu wa CDM Zitto kabwe amefanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya kawawa mjini kigoma na kueleza haja ya kufanya tathnimini ndani ya chama juu ya uchaguzi uliopiita
Alisema katiak majimbo nane ya mkoa wa Kigoma CDM imepata kiti kimoja, NCCR mageuzi vinne na vilivyobaki vimekwenda kwa CCM
amesema jambo la kujiuliza kuwa kati ya wbaunge wanne wa NCCR mageuzi, watatu wametoka CDM na hadi mwaka jana walikuwa huko
amesema CDM ifanye tathimini kwani itacfika wakati hasa 2015 inaweza ikakosa ambunge katika mkoa wa Kigoma
mwaka huu mapambano humo humo
mkitaka salama yenu mbowe aondoke muone chama kinavyosonga mbele
zanzibar tuna wabunge wangapi? Je Mtwara,lindi, dodoma tuna wabunge wangapi kwanini kigoma ambako tuna mbunge angalau mmoja..