Na ndivyo nilivyokujibu miye maana aliyenzisha mada kazungumzia M4C sana tu na kwamba hawamuhitaji Zitto na kueleza mambo kibao yanayomhusu Kitila kumuunga mkono Zitto. Haikuwa haja wala sababu maana M4C yenyewe Zitto na Kitila ni wahusika ktk maandalizi yake. Imefika hadi kila anayekubaliana na Zitto basi ni adui badala ya kumsikiliza kwanza mkaelewa kwa nini kasimamia mtazamo wake.
Mkuu wangu kila kinachoelea kimeundwa, Chadema haikushuka toka mbinguni imeundwa na watu wamekijenga chama hicho kuwa hapo kilipo. Sasa naanza kumwelewa Zitto anaposema OVYO maana imekuwa ujinga mtupu kwa mada kama hizi. Kila siku kukicha ni kuhusu Zitto au Uislaam yaani hamchoki kuzungumzia watu wengine mkijiona nyie wabora zaidi. Na nyie ndio mnataka kuifanya CHASO mradi binafsi maana kuna watu mnawatenga isipokuwa nyie tu ndio wazuuuri msiokuwa na mfano.
Halafu sijasema hamtakiwi kutokubaliana, hata hapa nadhani hatukubaliani lakini sioni sababu ya kuchukiana kiasi hicho. .. Na ndio maana tunatakiwa kusahihishana ama kuelekezana lakini sio kuunda chuki na Uadui ambao haukisaidii chama, wewe au Zitto. Na nimesema tena binafsi yangu kuna mambo sikubaliani na Zitto, Mbowe wala Dr.Slaa na husema pale napoona wamepotoka wao ktk yale waloyasema ama kuyafanya lakini hata siku moja kama ningekuwa ktk wajumbe wa chama ama kiongozi ngazi yoyote ile nisinge diriki kuandika lolote lilohusiana na vikao vya chama unless ni kwa faida ya chama..
Mkuu Kombe naomba ifike wakati tufunge mijadala hii maana haitujengi na wala haijengi chama:
Ni vyema watu tukaheshimiana na kuheshimu wengine, pia ni lazima tujue hatuwezi kupendwa na wote!
Japo nimesikitishwa na tishio la mkuu Mkandara kurudisha kadi ya chama lakini lazima niheshimu maamuzi yake!
Mimi ninacho amini mpigania haki hachoki wala hawezi kukata tamaa, na lazima tukubali kuwa cdm si chama cha malaika bali binadamu hivyo binadamu kugombana ni swala la kawaida ni swala la kuchukua hatua kuyamaliza haya mambo sisi wenyewe tena hana kwa hana si kutumia miitandao.
Ni lazima watu watambue kuwa kutukana watu na viongozi kupitia mitandao si busara na wala hkutatui tatizo bali kuongeza chuki baini yetu!
Mungu ni mwema cdm haitasambaratika tuvumiliane kwenye hali zote.
Mungu ibariki CHADEMA,MUNGU WABARIKI VIONGOZI WOTE
Alaaa! kumbe huu ni msimamo wa chama?..SIKUJUA..Basi nihesabuni sio mwanachama na kadi yenu nitawarudishia..Sitaki unafiki kabisa..
Mkuu, nyinyi nyote hamjamuelewa Mkandara....mkandara kaanza kuibadilikia CDM baada ya wafuasi wengi waCDM hapa jamviniMkandara mbona unakoamaa sana watu wampende Zitto bila sababu?Zitto mwenyewe ana tabia zinazochukiza watu huku akizidi kuzikuza.Sasa naona umeamua kukubali kuwa kazi yako humu ndani ni kuishambulia CDM tuu.
Sidhani kwa mtu ana ye kitakia mema chama ana weza kutamka maneno kama haya! Lazima tujue kuwa mtu hawezi kupendwa na watu wote, na mtu wenye matunda ndio utupiwa mawe!
Maneno yako nimeshindwa kuyatofautisha na maneno ya wassira!
Kwasababu nyinyi mashabiki wa CDM mnakashifu sanadini yake ya uislaammpambanaji wa kweli hawezi kukata tamaa,kwa nini utishie kurudisha kadi ya chama?
Sababu zipi za kurudisha kadi ya chama?
Mkuu Mwita,
Asante sana kamanda kwa kusimamia ukweli.Great Thinkers wa JF wanajua kinachoendelea tangu jana
Tuendeleze harakati kamanda
Kwasababu nyinyi mashabiki wa CDM mnakashifu sanadini yake ya uislaam
Naomba usi hukumu cdm kwa makosa ya vivuli(mizimu)!
Pili mimi binafsi siwezi kufanya hivyo na wala sijawai fanya hivyo na sitokuja kufanya!
Sipendi tuzungumzie maswala ya dini na sidhani kama hii ni sababu ya Mkuu mkandara kusema ana rudisha kadi ya chama, wala sidhani!
Wala hatuwezi kuhukumu chama kwa vivuli na tutakuwa hatutendi haki kabisa!
Kamanda tuko pamoja.
Mwalimu Nyerere alipata kusema umasikini wa akili (mawazo) ni mbaya kuliko umasikini wowote ule.
Kuna watu wanajitanabaisha kwamba ni wana Chadema lakini kwa makusudi kabisa wameamua kujitia umasikini wa akili.
Wasiwasi wangu ni kwamba most of them hawana kazi maalum za kuwaweka mjini kwahiyo wameamua kufanya kazi moja tu ya kuwatukana, kuwakashifu na kuwadhalilisha viongozi wetu.
Siwezi kukubaliana na mtu yeyote anayetukana viongozi wangu ama wanachama wenzangu kwa sababu zozote zile hasa hapa JF ambapo wengi wanatumia majina fake (nayaita mizimu ya JF). Lazima tufike mahali tukubaliane kutokubaliana ili tu move forward.
Hawa watu wanaokesha wakitukana viongozi wetu mitandaoni wanalipwa na nani kwa kazi hiyo wanayoifanya?
Mkuu mwita,Mkuu Mkandara nimesikitishwa sana na tishio/kusudio lako la kutaka kurudisha kadi ya Chadema kwasababu unaona Zitto anashambuliwa na ''vijana wa Chadema''.
Hivi inawezekanaje kukereka na mizimu ya JF inayojiita vijana wa Chadema to the extent ya kutaka kusitisha uanachama wako? Msimamo wako unanipa maswali kadhaa; Ulijiunga Chadema kumfuata Zitto ama ulivutiwa na sera za chama?
Je umewahi kusoma kwenye facebook kuona wanachoandika akina Mchange, Mtela, Juliana, Immaculate, Nyakarungu, Chagulani pamoja na wengine wengi wa kundi lao dhidi ya Dr. Slaa?
Hii notion ya kwamba kila mtu anayempinga Zitto anamchukia umeitoa wapi mkuu wangu mbona unakwenda mbali sana?
Hao vijana wanaokesha mitandaoni wakimtukana Dr. Slaa na kumtukuza Zitto ndio unawaona wa maana kuliko hawa wanaompinga Zitto? Nidhamu kwa viongozi unayoizungumzia hapa inakuwa na mashiko kwa upande mmoja tu ulio na maslahi nao au sijakupata vizuri kamanda wangu?
Kamanda tuko pamoja.
Mwalimu Nyerere alipata kusema umasikini wa akili (mawazo) ni mbaya kuliko umasikini wowote ule.
Kuna watu wanajitanabaisha kwamba ni wana Chadema lakini kwa makusudi kabisa wameamua kujitia umasikini wa akili.
Wasiwasi wangu ni kwamba most of them hawana kazi maalum za kuwaweka mjini kwahiyo wameamua kufanya kazi moja tu ya kuwatukana, kuwakashifu na kuwadhalilisha viongozi wetu.
Siwezi kukubaliana na mtu yeyote anayetukana viongozi wangu ama wanachama wenzangu kwa sababu zozote zile hasa hapa JF ambapo wengi wanatumia majina fake (nayaita mizimu ya JF). Lazima tufike mahali tukubaliane kutokubaliana ili tu move forward.
Hawa watu wanaokesha wakitukana viongozi wetu mitandaoni wanalipwa na nani kwa kazi hiyo wanayoifanya?
Mkuu mwita,
Labda katika utafiti wako kati ya Dr.slaa na Zitto nani anaongozwa kusemwa vibaya,kusimangwa kwenye mitandao ya kijamiii?
ukinpa jibu nitatoa nilichokuwa nataka kueleza mkuu
Tumeyasema sana takribani mwaka na nusu sasa.Chadema ina matatizo na yawezekana kabisa ukawa mwisho wa Umaarufu wake. Nazisoma dalili za chama kusambaratika kabla ya 2015, na maadam mashambulizi yanazidi kwa Zitto na Kitila sijui kama tutafika, sisi wengine tayari tumeisha anza kukusanya empty cartons...
Niungane naMwita Maranya, katika vijana wanaosimamia kile wanachokiamini kwa hoja na mantiki Ben ni mmoja wapo.Maandishi yake yana ukomavu wa kisiasa. Hata pale anapopingwa bado husimama kutetea hoja zake kwa mantiki.-Siku watanzania tutakapoamua kuamini katika ujenzi wa Taasisi imara badala ya watu tutakua tmepiga hatua sana
-Hatutafuti kujenga watu bali Chama imara....katika taasisi adilifu na inayosimamia mchakato wa mabadiliko kwa ufanisi
-Hakuna asiyejua Taifa letu lina ombwe la kisera na kiitikadi.Hatuwezi kutatua au kuziba ombwe hili kwa kutegemea haiba(legacy) ya mtu mmoja mmoja.Tukifanya hivyo tutakuwa tunafanya worse kuliko enzi za state party.Tutakua tunaandaa mazingira ya mtu kushika hatamu
Hoja hii haitakiwi kupaliliwa na vijana ambao ndiyo wanaotarajiwa kuamua hatima ya Taifa letu
Hebu tujenge Chama kwanza kwani bila chama imara hakuna mgombea yeyote hata awe na nguvu kiasi gani atakayeweza kupambana mfumo huu ulioasisiwa na CCM kwa makusudi kabisa kwq maslahi yake
Hatujengi watu imara wa kupigana vita za koo.Tunajenga chama kuongoza ukombozi wa watanzania.
Kumuunga mtu mkono bila kujali mahitaji ya kisera na kiitikadi katika kile anachosimamia ni immaturitu ya aina yake.Kwa kijana msomi kabisa anayeelewa haya na akafanya makusudi atakua msaliti katika harakati hizi
Kwa vile Zitto ni role model wako kama unavyonena, je, hiyo inahalisha umjenge kisiasa kwa kuzusha maneno au Uongo? Je, unataka kuwaambia nini wanachadema, kwamba uwepo wako ndani ya chama si kwa sera bali kuamini mtu! Hapo kuna siasa au ni si-hasaTUNTEMEKE;4954880]Makala yako imeyakosa kachumbari hii hapa.Umeainisha vizuri kabisa kwamab Zitto ni ngao,kifua cha CHADEMA .Umemuunga mkono kutangaza nia ya Urais kwa asilimia mia moja.Nakupongeza kwa hilo.ZITTO HATA MIMI NAKUUNGA MKONO,NAKUSAPOTI KISIASA NA WEWE NDIYE ULINIFANYA NICHUKUE KADI
Je, uchafu wa Dr Slaa unavithibitisho au ni hisia tu! Chadema kinajengwa kama chama cha siasa au taasisi ya kidini? Ni nani miongoni wa wanachadema unaweza kumtoa hadharani na kutuhakikishia uadilifu wake katika imani!LAKINI IKUMBUKWE WAZI NI BORA HAMSINI NZIMA KULIKO MIAMOJA MBOVU.KWA UCHAFU ALIONAO DR.SLAA KUANZIA KWENYE MSINGI WAKE WA KIDINI HADI MWENENDO WAKE NDANI YA CHAMA HATA MIMI SIWEZI KUTHUBUTU KUMUUNGA MKONO AU KUMFANYA AWE MODEL WANGU WA KISIASA
Hebu fafanua au weka wazi ili tusiojua tujue, unaposema kampuni una maana gani? na hao viongozi wa kuwekwa na Mbowe ni wapi. Nakiri sina ufahamu naombaunisadie kuweka sawa kama Mwananchi tu.KWA NAMNA MBOWE ANAVYOKIGEUZA CHAMA KAMPUNI,ANAVYOWAJAZA WACHAGGA PALE MAKAO MAKUU NA KWENYE UONGOZI MBALIMBALI WA CHAMA MIKOANI,NAKUHAKIKISHIA HATA KWA MJEREDI SIWEZI KUMUUNGA MKONO
Kwa mtazamo wako upo sahihi, kwa wachambuzi wa mambo ya kisiasa hakuna ukweli.MCHANGE KACHAGUA FUNGU LILIO JEMA ANAMSAPOTI NA KUMTETEA MTU AMBAYE HANA KASHFA ZA AKINA DR.SLAA AU MBOWE.
Umetumia vigezo gani na takwimu zipi kufikia conclusion?ZITTO NDIYE KIONGOZI PEKEE NDANI YA CHADEMA AMBAYE ANAKUBALIKA KWA VIJANA,WAZEE NA VIONGOZI WENZAKE KASORO HAO WAWILI NAO NIKWASABABU ZITTO ANAONEKANA KUWA NA POLITICAL CAPITAL KUBWA SANA NDANI YA NCHI NA NDANI YA CHAMA
Kashfa ya kusaliti dini na kashfa namba 6 zinahusiana vipi na mambo ya kisiasa? Kashfa hiyo inakiathiri vipi chama?NACHUKIZWA NA MWENENDO WA DR.SLAA1.KASHFA YAKE YA KUSALITI DINI YAKE
2.KASHFA INAYOENDELEA HADI SASA YA KUONGOZWA NA MCHUMBA WAKE
3,KASHFA YA KUTENGENEZA MTANDANO WA MAJUNGU NA FITINA NDANI YA CHAMA
4.KASHFA YA KULA HELA ZA CHAMA
5.KASHFA YA KUFUKUZA VIONGOZI WA CHAMA KATIKA NGAZI MBALIMBALI ZA UKURUGENZI,MKOA NA TAWI KWA SABABU TU JOSEPHINE HAPENDANI NAO,ZITTO ANAKUBALIKA