TUNTEMEKE;4954880]Makala yako imeyakosa kachumbari hii hapa.Umeainisha vizuri kabisa kwamab Zitto ni ngao,kifua cha CHADEMA .Umemuunga mkono kutangaza nia ya Urais kwa asilimia mia moja.Nakupongeza kwa hilo.ZITTO HATA MIMI NAKUUNGA MKONO,NAKUSAPOTI KISIASA NA WEWE NDIYE ULINIFANYA NICHUKUE KADI
Kwa vile Zitto ni role model wako kama unavyonena, je, hiyo inahalisha umjenge kisiasa kwa kuzusha maneno au Uongo? Je, unataka kuwaambia nini wanachadema, kwamba uwepo wako ndani ya chama si kwa sera bali kuamini mtu! Hapo kuna siasa au ni si-hasa
LAKINI IKUMBUKWE WAZI NI BORA HAMSINI NZIMA KULIKO MIAMOJA MBOVU.KWA UCHAFU ALIONAO DR.SLAA KUANZIA KWENYE MSINGI WAKE WA KIDINI HADI MWENENDO WAKE NDANI YA CHAMA HATA MIMI SIWEZI KUTHUBUTU KUMUUNGA MKONO AU KUMFANYA AWE MODEL WANGU WA KISIASA
Je, uchafu wa Dr Slaa unavithibitisho au ni hisia tu! Chadema kinajengwa kama chama cha siasa au taasisi ya kidini? Ni nani miongoni wa wanachadema unaweza kumtoa hadharani na kutuhakikishia uadilifu wake katika imani!
KWA NAMNA MBOWE ANAVYOKIGEUZA CHAMA KAMPUNI,ANAVYOWAJAZA WACHAGGA PALE MAKAO MAKUU NA KWENYE UONGOZI MBALIMBALI WA CHAMA MIKOANI,NAKUHAKIKISHIA HATA KWA MJEREDI SIWEZI KUMUUNGA MKONO
Hebu fafanua au weka wazi ili tusiojua tujue, unaposema kampuni una maana gani? na hao viongozi wa kuwekwa na Mbowe ni wapi. Nakiri sina ufahamu naombaunisadie kuweka sawa kama Mwananchi tu.
MCHANGE KACHAGUA FUNGU LILIO JEMA ANAMSAPOTI NA KUMTETEA MTU AMBAYE HANA KASHFA ZA AKINA DR.SLAA AU MBOWE.
Kwa mtazamo wako upo sahihi, kwa wachambuzi wa mambo ya kisiasa hakuna ukweli.
Kwani huwezi kumtetea Zitto bila kuwakashfu watu wengine? Nasema kuwakashfi kwasababu hujaweka uthibitisho wa tuhuma zako zaidi ya hisia.
ZITTO NDIYE KIONGOZI PEKEE NDANI YA CHADEMA AMBAYE ANAKUBALIKA KWA VIJANA,WAZEE NA VIONGOZI WENZAKE KASORO HAO WAWILI NAO NIKWASABABU ZITTO ANAONEKANA KUWA NA POLITICAL CAPITAL KUBWA SANA NDANI YA NCHI NA NDANI YA CHAMA
Umetumia vigezo gani na takwimu zipi kufikia conclusion?
NACHUKIZWA NA MWENENDO WA DR.SLAA1.KASHFA YAKE YA KUSALITI DINI YAKE
2.KASHFA INAYOENDELEA HADI SASA YA KUONGOZWA NA MCHUMBA WAKE
3,KASHFA YA KUTENGENEZA MTANDANO WA MAJUNGU NA FITINA NDANI YA CHAMA
4.KASHFA YA KULA HELA ZA CHAMA
5.KASHFA YA KUFUKUZA VIONGOZI WA CHAMA KATIKA NGAZI MBALIMBALI ZA UKURUGENZI,MKOA NA TAWI KWA SABABU TU JOSEPHINE HAPENDANI NAO,ZITTO ANAKUBALIKA
Kashfa ya kusaliti dini na kashfa namba 6 zinahusiana vipi na mambo ya kisiasa? Kashfa hiyo inakiathiri vipi chama?
Kashfa ya 2 anaongozwa vipi, una vithibitisho au hisia! Je, akitokea mtu na kusema wewe ni kibaka tunapaswa kuamini tu kwasababu kasema mtu au tunahitaji vithibitisho kabla ya hitimisho. Chako dhidi ya Dr Slaa ni kipi?
Kashfa 3, mtandao upi ni wa majungu mbona bado unatuweka gizani. Kwanini usiutaje huo mtandao hadharani
Hadi hapo wewe ukiwa mwanachadema unayemuunga mkono Zitto, tayari umeshajipiga risasi mguuni( shoot yourself on the foot). Umekichafua chama katika maeneo yote ambayo kipo ''vulnerable''
Akipatikana mwanasiasa mahiri atazitumia hoja zako kuwamaliza Chadema na Zitto akiwemo.
Ulichokifanya ni kazi ya Abnuwasi aliyekalia tawi na kukata tawi hilo upande wa shina.
Kuna tatizo ndani ya Chadema! Lishughulikieni. Nilikuwa napitia makabrasha nikaona enzi za NCCR na CUF.
Nilidhani hizo zimepita nalazimika kusema bado!