Zitto hana chama, chama ni cha Wapemba na wafuasi wa Maalimu Seif

Zitto hana chama, chama ni cha Wapemba na wafuasi wa Maalimu Seif

Aisee! Kumbe kuna vyama vipo up for grabs? Ngoja na mimi nitafute kimoja nikikwapue.
 
Siasa zetu za kuchaguana kwa kuangalia sura na mengineyo haziwezi kumfanya Zitto aachiwe makaratasi ya msajili.

Naona huyu ana bahati ya kuachiwa urithi wa wafuasi wa Maalim Seif, hivyo ataendelea kutembea nao mpaka pale naye atakapomuachia kiongozi mwingine huo urithi.
Hata Mbatia aliachiwa urithi wa wanachama na Mrema mifano ni mingi.
 
Sidhani kama Zitto ni mjinga hivyo.
Mola aepushie mbali. Ila siasa huwa hazitabiriki. Wewe ulitegemea kweli miaka miwili iliyopita kuwa leo hii Ndugai angekuwa amepitishwa kwenye tanuru la moto kama alilopitia ?

Maalim Seif hakuwahi kutegemea kuwa kuna siku Lipumba angemgeuka kwa zile hustle walizopitia pamoja
 
Mola aepushie mbali. Ila siasa huwa hazitabiriki. Wewe ulitegemea kweli miaka miwili iliyopita kuwa leo hii Ndugai angekuwa amepitishwa kwenye tanuru la moto kama alilopitia ?

Maalim Seif hakuwahi kutegemea kuwa kuna siku Lipumba angemgeuka kwa zile hustle walizopitia pamoja
Siasa ni kuzicheza karata vizuri.
 
Quinine NAOMBA NIKUITE AKILI KUBWA. Umeleta hoja mbayo si rahisi mtu kuifikiria. Kwa wazazibari, hakuna chama kinaitwa ACT , Kiichojengwa kwenye mioyo yao ni chama kinaitwa "CUF_ MAALIM SEIF". Wao belief yao ni hiyo.

Kwa uzandiki wa Magufuli na Lipumba, akaiua CUF na Wazazibar wakabaki bila chama cha kuwaunganisha . Wafanyeje na walijua wakianzisha chama hakiwezi kusajiliwa. JISHIKIZE KWA ACT cum Zito.

Hivyo Zito Zanzibar hana chama wala wafuasi wa ROHONI, wanajishikiza... na bara hawa wafuasi. It is a matter of time when it is ripe to have their own identity cemented on the foundation of Maalim Seif.

Zito kwa Zanzibar anabebwa may be na dini! mwenzetu huyu katika Imani....
 
chama chenyewe alikikwapua kutoka kwa Lucas Kadawi Limbu na wenzake. Kisha akawafanyia roho mbaye wenzake akina Kitila na mama Mghwila, wakatimkia ccm. Ipo siku ukweli mchungu utakuwa dhahiri kwake
Huyu ndiye aliyekabidhiwa cheti cha usajili wa kudumu wa ACT sijui kama hata Zitto anamkumbuka.

83AED71F-24F9-4A8A-95B2-314DCFBF3F83.jpeg
 
Kilicho msumbua Zitto ni kutaka nafasi ya kiongozi wa upinzani bungeni akidhani atapata wabunge wengi toka Zanzibar lakini Mwendazake akapiga tobo yeye mwenyewe na kuishia kupata wabunge wanne tuu
 
ACT - Wazalendo haina wanachama wala jengo la ofisi inalomiliki Bara. ACT inategemea nguvu ya wanachama kutoka Zanzibar wengi wakiwa ni wale waliokuwa wafuasi wa CUF- Maalimu Seif.

ACT -Wazalendo haina Jengo la Chama kwa maana ya umiliki, jengo walilopewa na Maalimu Seif Foundation ni lile walilokuwa wanatumia waliokuwa Wabunge watiifu wa Maalimu Seif, linamilikiwa na familia ya Seif.

ACT Wazalendo haina mtandao Bara mtandao wake uko Zanzibar. Kwa mtu makini ataelewa hapa mwenye nguvu ya chama ni nani kati ya Zitto, Wazanzibari na familia ya Seif.

Siku wenye chama chao wakiamua kuondoka na jengo lao chama kitakufa Zitto atabaki na makaratasi ya Msajili wa vyama vya siasa tu. Jifunze kutoka kwa Lipumba na CUF yake.

Najua wafuasi wa Zitto hawapendi kusikia haya lkn, Ukweli ndio huo.

Zitto and others, Keep this short Thread you will thank me later.
ACT inatumika na CCM
 
Back
Top Bottom