Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Zito ni pandakizi tangu akiwa CHADEMA.. na aliandaliwa na CCM ili aje kuidhoofisha kabisa kama ule mpando wa kuwa mwenyekiti ungefauluChama cha ACT kimeanzishwa na kina JK, Membe, Januari, Mwigulu nk kama Backup ya CCM baada ya kuzidiwa na CDM. Zito ndio alipewa jukumu hilo. Hao kina Limbu walitangulizwa tu baadae akataka kulazimisha kuwa kiongozi. Lakini wenye chama wakafanya yao na Zito akapewa nafasi yake. Rejea uchaguzi wa 2015 ACT ikiwa changa kabisa, ilisimamisha wagombea wa nafasi zote kuanzia urais, ubunge na udiwani nchi nzima, huku haifahamiki hela zao zilitoka wapi.
Magufuli 2015 ndio aliharibu mpango wa ACT kuwa chama kikuu cha upinzani, kwani alikuwa hampendi Zito, na pia hakuwa analipenda kundi la JK ambao ndio wafadhili wa ACT. Ni bahati mbaya wakati Maalim Seif anaporwa chama na Magufuli kwa kumtumia Lipumba, Maalim Seif akatafuta chama akaona ACT ndio hakina kiongozi wa muda mrefu na sio cha muda mrefu kama ilivyo CDM, NCCR, TLP nk. Alijua fika akiwa ACT atakuwa na maamuzi yote kama alivyokuwa CUF, na kweli ndio ilivyokuwa, ndio maana alishikilia kumuunga mkono Lisu kwenye urais, na sio Membe kama ambavyo Zito alitaka kwani Membe ndio wenye chama.
Zito ataendelea kuwa kiongozi wa chama cha ACT, kama ataendelea kuwafanya hao Wapemba wafanye Siasa zinazotakiwa na CCM. Hao Wapemba watavurugana na zito siasa za kweli za ushindani zitakapoanza na CDM kushika nafasi yake kama inavyotegemewa. Na zito anajakikisha anafanya siasa zinazotakiwa na CCM, kwa kuwahadaa ACT Wapemba kuwa hizo ni siasa za kistaarabu. Hili jengo la ACT lina fedha ya ufadhilii wa CCM, ndio maana huoni wakitaja thamani ya jengo, wala chanzo cha fedha hizo.
Hilo liliposhindikana ndio ukaundwa mpango wa usaliti chini ya viongozi watatu M1,M2 na M3.. M1 ilikuja kujulikana kwa wote ni Zito
Baada ya mtikisiko mdogo wa usaliti uliolenga kukigawa CHADEMA kuwa mapande mawili, kina Zito na kundi lake walipoteana na kusalitiana upya wenyewe kwa wenyewe
Wengine wakabaki na Zito ACT na wengine wakatimkia CCM kuunga juhudi na kupewa zawadi ya vyeo kina Shonza n the like.. Lakini picha halikuishia hapo.. Zito ndani ya ACT akapewa kazi ya kuhujumu kwa mlango wa nyuma juhudi na harakati zozote za upinzani (CHADEMA) kwa namna yoyote ile inayowezekana kufanya hivyo.. Na ndio anachokifanya mpaka wa leo
Zito hana mpango wowote wa kukipeleka ACT ikulu, hana mpango wowote wa kupigania mageuzi ya kweli, hana mpango wowote wa kuwakomboa watanzania kwenye shida yoyote... Yupo kwa ajili ya kutumika na kutumikia malipo ya ahadi