Zitto Kabwe: ACT sio chama cha kupiga kelele na kubwabwaja-bwabwaja, tutashiriki uchaguzi hata kama hakuna Katiba mpya

Zitto Kabwe: ACT sio chama cha kupiga kelele na kubwabwaja-bwabwaja, tutashiriki uchaguzi hata kama hakuna Katiba mpya

Hata CHADEMA uchaguzi lazima washiriki katika mazingira yoyote yale.
 
Zitto asiposhiriki uchaguzi CCM itafanyaje sasa? Kazi ya Zitto na Chama chake ni kulinda maslahi ya kiongozi yoyote muislam atayekuwa madarakani muda huo.
Hawezi kuacha ndugu yake katika Imani aaibike (Hata kama ni kwa gharama ya maisha ya watanzania)
Kwanza Zitto siyo mtanzania,uchungu autoe wapi na nchi hii.
Act wazalendo na CCM wanaunda SUK sasa inawezekanaje asishiriki uchaguzi? Hii haikupaswa kuwa habari
 
Akijibu maswali katika mahojiano na Edwin Odemba katika Kipindi cha Medani za Siasa ikiwemo suala la kuwa makali yake kisiasa yamekwisha na madai kuwa yeye na Chama chake ni kama CCM B, Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe anasema:

“(Kuhusu suala la usaliti) Waulize wao, hizo ni propaganda za kisiasa, ni za kawaida sana kwenye utamaduni wetu wa kisiasa. Wakati NCCR Mageuzi na CUF wakiwa ndio vyama vikubwa vya upinzani hapa Nchini walikuwa wakiwaita CHADEMA kuwa ni CCM B.

CHADEMA ikaamka ikajipanga na kikawa chama kikubwa nacho kikaanza kuwiata NCCR na CUF kuwa ni CCM B, kwa hiyo mimi sioni tabu hata kidogo (kuitwa CCM B) muhimu ni sisi kusimama kwenye reli kwa yale ambayo tunayasimamia.

Aina yetu ya kufanya siasa haiwezi kuwa kama yao, hata tufanye vizuri namna gani hawawezi kuach kutuita hivyo wanavyotuita, tunafanya kazi yetu kama Chama cha Upinzani, tunatoa maoni yetu, tunatoa sera mbadala ili kuboresha maisha ya Watanzania.”

Alipoulizwa kuwa anaichukuliaje kauli ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu kuwa CHADEMA ndio chama pekee cha upinzania cha ukweli na kinachosimamia shida na kueleza shida za Watanzania.

AULIZA, TUNDU LISSU YEYE NI NANI?
Zitto anasema “(Tundu Lissu) yeye ni nani? Ana wajibu wa kuzungumzia chama chake, hana wajibu wa kuzungumzia vyama vingine na hawezi kuwa IS Unit ya namna gani vyama vingine vinafanya siasa.

“Chama chetu ni chama pekee ambacho lilipotokea tatizo la bei ya mafuta kupanda tulitoa mapendekezo ya namna ya kupunguza kodi mbalimbali na Serikali ikafanya, tunazungumzia kuhusu kudhibiti mfumo wa bei ya vya vyakula, ukitazama kwenye vyombo vya Habari sisi ndio tunangumza.

“Sisi sio chama cha ajenda moja ndio maana tunazungumza masuala yote ya Wananchi, Baraza Kivuli la Mawaziri linafanya kazi kubwa ya kuibua maswala mbalimbali, tunatimiza wajibu wetu, sisi sio chama cha kupiga kelele siyo chama cha kubwabwajabwabwaja, inapotokea changamoto ya kitaifaifa utatuona, hatusemi tu bali tunapendekeza namna ya kufanya.

“Wapiga kelele na wanaobwabwa waache waendelea wanavyofanya, sisi tutaendelea na mfumo wetu wa siasa, tutakutana kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mtaa na Uchaguzi Mkuu, tutaona Watanzania wanapenda aina gani ya siasa, ya kelele na kubwabwaja au siasa za kukosoa na kupendekeza mbadala kisera, Wananchi ndio watakaoamua kwenye uchaguzi.”

ACT KUSHIRIKI UCHAGUZI
Alipoulizwa kuhusu madai ya CHADEMA kuwa haitashiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ikiwa hakutakuwa na muafaka kuhusu Katiba Mpya anasema:

“Tunajiandaa na uchaguzi, tutashiriki chaguzi zote zinazokuja (2024, 2025) katika mazingira yoyote, miaka hii mitatu ya kukaa na Bunge la Chama kimoja tumeshuhudia masuala ya Wananchi hayajadiliwi ndani ya Bunge, hatuwezi kumuacha Nguruwe kwenye shamba la mihogo atamaliza mihogo yote shambani.

Tutashiriki ndani ya Bunge tupate wawakilishi ndani ya Bunge ili yale ambayo Watanzania wanayataka yanapatikana, hatutasusa.”

KUNG’OLEWA KWA JAMES MBATIA NDANI YA NCCR
Zitto anasema “Hayo ni mambo ya kupuuza madai kuwa niliingilia kuondolewa kwa Mbatia NCCR, sisi hatuingilii mimi sihusiki na kuondolewa kwa James Mbatia kwenye nafasi yake, kwanza si rafiki yangu na wala sina mazoea naye, sijawasiliana naye tangu aondolewe kwenye nafasi yake ili kumfariji na sitafanya hivyo.

“Hao waliojitokeza kumtetea kiko wapi? Wamefanya nini? Naamini aliyekuwa Mwenyekiti wa NCCR anajua taratibu za kufuata na wao wenyewe watamalizana, ni changamoto za kisiasa.”
Safi sana, hongera Mheshimiwa Zitto, wabwabwajaji watajifunza kwako, nina imani watabadili gia angani waachane na ubwabwajaji. Kongore.

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo katiba mpya yenyewe haitakuwepo hadi 2025.
Sisi tunahitaji maendeleo kama ujenzi wa Hospitali, vituo vya afya, zahanati pamoja na shule kwa ajili ya watoto na wajukuu wetu, maji safi na salama, barabara nzuri, umeme hata kwa sisi wa vitongojini n.k. Kwani katiba mpya itavileta hivyo ikibadilishwa, kazi iendelee mama chapa kazi, wabwabwajaji wapuuze midomo mali zao wabwabwaje hadi wawe ubwabwa.

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Zitto asiposhiriki uchaguzi CCM itafanyaje sasa? Kazi ya Zitto na Chama chake ni kulinda maslahi ya kiongozi yoyote muislam atayekuwa madarakani muda huo.
Hawezi kuacha ndugu yake katika Imani aaibike (Hata kama ni kwa gharama ya maisha ya watanzania)
Kwanza Zitto siyo mtanzania,uchungu autoe wapi na nchi hii.
Kwamba Nyepesi ni Mbembe wa Kongo?
 
Mbinu hii ya ACT ya kutoa hoja mbadala hufaa sana ktk nchi zenye katiba bora na utawala wa kidwmokrasia. Lkn kwa chama kama ccm na taifa kama Tanzania mbinu ya ACT ni kuisherehesha ccm na kuifanya iendelee kutawala.

Ccm itaondolewa madarakani kwa kulianzisha.
 
Back
Top Bottom