Zitto Kabwe: ACT-Wazalendo itaunga mkono juhudi za Serikali

Zitto Kabwe: ACT-Wazalendo itaunga mkono juhudi za Serikali

Mhe. Zito Kabwe ni Mzalendo wa kweli mwenye uchungu na kuipenda nchi yake kwa dhati ya moyo wake.

ACT ni chama ambacho nakikubali, chama cha siasa kinacho nadi sera mbadala kwa hoja sio matusi wala dhihaka kama walivyo Chadema na Nccr.

Siasa sio ugomvi wala uadui bali siasa ni kushawishi kwa hoja madhubuti.
vyama vingine vya upinzani viige mfano mzuri kutoka ACT
Inafahamika huna akili dada
 
Hii ni mara ya sita anaongea kuhusu kuiunga mkono serikali hii nyizi na onevu kwa wananchi wake ,nikwamba anatafuta huruma ya mama apewe teuzi au?? Maana haeleweki.
Zito anaipenda kigoma awamu hii inaonesha kuifungua kigoma ugomvi wanini tena hapa nikuunga juhudi tu hatamimi nampongeza zito naunga mkono serekali pia serekali itukumbuke wavuvi tulifilisiwa kinyonge namwenda zake mama tutazame tuliozulumiwa na utawala ule sisi wavuvi kata yakalya (w) uvinza
 
Kwa hiyo kuna watu wanamsikiliza zitto ,asee kweli kuishi kwingi kuona mengi
 
Ok tumemuelewa kuwa Zito tatizo lake ilikua Magufuli na sio yaliyokuwa yanafanyika.

Samia anafanya miradi ile ile ya Magufuli ambayo kipindi kile Zito alikua anaipinga ila sasa ameamua kuisupport.

Well hii tuite nini??
Anatafuta connection ili awe napakutokea.
 
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Ndg. Zitto zuberi kabwe amesema chama hicho kitaunga mkono juhudi za serikali katika miradi mbalimbali ya maendeleo na amewataka wananchi na wanachama wa chama hicho, kuendelea kufuatilia kwa kina iliyotekelezwa ili kukamilika kwa wakati
Lini chama chake kitashinda uchaguzi na kuunda Serikali kama ataendelea kuunga mkono juhudi ya chama kingine miaka miaka?!......
 
Lini chama chake kitashinda uchaguzi na kulinda Serikali kama ataendelea kuunga mkono juhudi ya chama kingine miaka miaka?!......
Kupitia kuunga mkono juhudi hizo huenda ili akubalike na lolote linaweza kutokea na yeye kupata shavu
 
2025 nilipanga kuwapa kura yangu sasa nitaipeleka kwa mzee wa ubwabwa
 
Zitto ni kada wa CCM iliyevishwa nguo za zambarau badala ya kijani. Hana jipya wala maana. Kwa wakati huu ni bora kumsikiliza mzee Pole Pole kuliko Zitto.
 
Hii ni mara ya sita anaongea kuhusu kuiunga mkono serikali hii nyizi na onevu kwa wananchi wake ,nikwamba anatafuta huruma ya mama apewe teuzi au?? Maana haeleweki.
Zitto anajiona amefikia level ya kuwa waziri wa fedha. Anachokitafuta ni uteuzi ili akaitumikie serikali.

Kwa hatua aliyofikia anaweza kuwatelekeza wenzake kwenye chama akakimbilia CCM ili akaonje zile za kujipimia na zile za kupiga kwa urefu wa kamba.

God save our country.
 
Bado hawajampa chochote? Maana anarudia rudia naona hawajamsikia,aongeze volume
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Ndg. Zitto zuberi kabwe amesema chama hicho kitaunga mkono juhudi za serikali katika miradi mbalimbali ya maendeleo na amewataka wananchi na wanachama wa chama hicho, kuendelea kufuatilia kwa kina iliyotekelezwa ili kukamilika kwa wakati
 
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Ndg. Zitto zuberi kabwe amesema chama hicho kitaunga mkono juhudi za serikali katika miradi mbalimbali ya maendeleo na amewataka wananchi na wanachama wa chama hicho, kuendelea kufuatilia kwa kina iliyotekelezwa ili kukamilika kwa wakati
Classic Zitto. Hapa insinuation ni kuwa kuna vyama ambavyo vinapinga juhudi za serikali katika miradi ya maendeleo. Kuwa kwa kusema, hebu ngoja kwanza tuangalie uratibu uliofuata kupatikana kwa hiyo miradi au kwa nini mradi huu wakati kuna mahitaji makubwa zaidi mengine ambayo yana umuhimu zaidi, n.k. ni kupinga juhudi za serikali kutokana na ubinafsi, sio uzalendo.

Classic kuuma na kupuliza. Kama kusema mwenzetu ana matatizo ya kisheria. Inabidi tu kumvulia kofia.

Amandla...
 
Back
Top Bottom