Mbowe mbona kama kashatulizwa na hana makali yoyote.
Mimi napenda logical consistency tu.
Kama kuhodhi madaraka muda mrefu ni kitu kibaya, basi tusimlaumu Zitto kujiuzulu. In fact Zitto anatakiwa awe mfano wa kuigwa hapo.
Kama kujiuzulu katika mapambano ni kitu kibaya, basi tusimtake Mbowe ajiuzulu katikati ya mapambano.
Kwa sasa hivi, kwa uchambuzi uliouandika, inaonekana karata ya kujiuzulu inatumika kisiasa tu kwa interests za watu, na inakosa uzito wa hoja kubwa za kifalsafa.
It's just games to win at politics, not deep rooted governance issues. There is a big difference.
Inawezekana ni kweli Mbowe hana makali, lakini CCM wana propaganda kwamba Mbowe ni mwenzao, hili linafanywa ili akose ushawishi kwenye kambi yake ya Upinzani, ambako kawasumbua CCM kwa muda mrefu sana. Inaonekana wameanza kufanikiwa kwasababu wanachama wengi wa chama chake wameanza kuamini hilo, sijui kama ni kweli au ndizo propaganda zenyewe. CCM wamefanya kila aina ya ufedhuli kuisambaratisha CHADEMA, lakini Mbowe imekuwa ni kisiki kigumu kwao kwa muda mrefu tena sana.
Mbowe anajua kujenga hoja, mbowe nana jua ku recruit vijana na kuwajenga ndani ya chama chake. Mbowe amekabidhiwa chama kichanga amekifanya kiwe kikomavu. haya yote CCM wanayafahamu. Miongo yote CCM wamecheza rafu kwa Chadema, kuweka mapandikizi, na hata kuwa nunua viongozi ndani ya chadema yote hiyo ni kutaka kuimaliza CHADEMA lakini Mbowe bado ana recruit vijana na wana kubalika. Patrobas Katambi, Dr.Vincent Mashinji, Mwita Waitara, Dr.Slaa na wengine wengi, ccm walifanya na kuuaminisha umma kwamba wanaikimbia kwasababu zoote zilizosemwa lakini Mbowe bado ana recruit na wanakubalika na wanaendelea kuisumbua CCM.
Hivyo hata hili naamini liko mule mule kwenye kumchafua Mbowe ili kuuaminisha umma kwamba hafai kuwa kiongozi, na mbinafsi. Lakini kumbuka hivi vyama bado vichanga sana visipopata viongozi wazuri wenye kujali Maslahi yao havifiki mbali. Na yoote hayao yana ratibiwa na CCM.
Walijaribu kumrubuni Maalim Seif wakashindwa, waka mtumia Hamad Rashid na kumsaidia kuanzisha chma cha ADC, wakashindwa, wakamtumia Prof.Lipumba aliyejiuzulu mwenyewe na kuutangazia umma, lakini kupitia ofisi ya msajili wakafanikiwa kuisambaratisha CUF.
NCCR unafahamu ilivyokuwa imara, CCM wakaigawa mara mbili, Wakaimaliza. Mrema na TLP alikuwa Imara, wakammaliza.
Juzi hapa umesikia NCCR tena, wanaimaliza kupitia SELASINI, wanamfukuza Mwabukusi.
Wao CCM ndio wanataka Mbowe ajiuzulu, wanafahamu hapo watakuwa wamefanikiwa kuimaliza CHADEMA. Wanadai kazeeka. Unajua Philip Mangula kakaa muda gani ccm kama katibu mkuu, Muangalie Abdulaman Kinana ni kijana?
Sasa Mbowe akiondoka unadhani Chadema itahimili vishindo vya CCM? CCM wanataka wenye bei, lengo lao ni kutaka kutawala milele.
Wameiba chaguzi, kuikatisha chadema tamaa wanakuta Mbowe hatetereki, wamemchukulia viongozi yupo tu, wameharibu ngome upande wa kina mama kulazimisha kuwapa ubunge kina Halima na wenzake 18, na kujaribu kutaka kuiua chadema wamekuta ukuta, na wamepigania kesi kwa mahakamani na kwa msajili bado ccm wameshindwa lakini hawataki kuwaachia kina Halima. Yoote analengwa Mbowe.
Wana mchonganisha na Lisu wanamkuta katulia sasa wameona kujiuzulu ndiyo karata yao.
Anyway kila myu anaona anavyoona lakini naamini CCM wana mbinu chafu sana. Tutaona kama watafanikiwa kwenye hili.
Utasikia sio mzalendo, lakini wanadai wamesha mlambisha asali, na eti yuko ccm.