Zitto Kabwe ampiga 'kijembe' Tundu Lissu kuhusu hoja za hati ya Muungano.

Zitto Kabwe ampiga 'kijembe' Tundu Lissu kuhusu hoja za hati ya Muungano.

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Posts
5,536
Reaction score
2,266
Wakati akichangia hoja za Kamati za Bunge Maalumu namba moja hadi 12, juu ya Sura ya Kwanza na Sura ya Sita ya Rasimu ya Katiba, Zitto Kabwe alisema wajumbe hawako Bungeni kwa ajili ya KUKUMBUSHANA HISTORIA YA TANZANIA KUHUSU MUUNGANO, kwa maana kuwa, kujadili hati za muungano ni useless and uncalled for, bali wabunge wako bungeni kutafuta mfumo wa uendeshaji wa maisha ya wananchi wa leo na kesho utakao kubaliwa na wananchi wengi na siyo mfumo wa uendeshaji wa jana.

Tunaielewa historia ya nchi yetu, hakuna haja ya kukumbushana, tuepuke lugha za matusi, chuki, ubaguzi, tubakie na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," alisema Zitto.

Zitto Kabwe alibainisha na kusema, Mchakato huu tuufanye kwa kujadiliana kwa hoja, tusitukanane, muundo wowote wa serikali unaweza kuvunja Muungano, kikubwa ni kuafikiana maridhiano kutoka pande zote mbili za Muungano.

Kabwe Zitto amesema muundo wowote wa serikali uwe serikali moja, mbili au tatu unaweza kuvunja Muungano ikiwa hakutakuwa na muafaka wa pande zote mbili za Muungano.

Katika hatua nyingine Zitto alisema ikiwa itaundwa serikali isiyo na maridhiano ya pande zote mbili za Muungano, gharama ya kuulinda Muungano huo itakuwa ni kubwa sana.

[video=youtube_share;nFRJDBXZJVo]http://youtu.be/nFRJDBXZJVo[/video]
 
Maoni yake binafsi! Kwa kadiri ya uelewa wake!

Mimi kama ninavyoamini kuna wengi wataniunga mkono, naamini ni busara kujua ulipokosea, ili urekebishe kosa. Ukiona aibu kureview makosa yako utashindwa kuona kosa na hivyo historia inaweza kujirudia.

Mpaka sasa tuna matatizo ya kutosha ya Muungano (tunayaita kero za muungano) Haya yalisababishwa na makosa ya waliouanzisha. Ni vizuri, kama tunataka kuyamaliza tujue walikosea wapi ili turekebishe. kwa mfano:

Kukosekana kwa kwa serikali ya Tanganyika kunamaanisha kuwa serikali ya Tanganyika imemezwa ndani ya ile ya Muungano. hivyo maswala yote ya Tanganyika yanatatuliwa na serikali ya Muungano. Ni serkali hii hii ya Muungano inayofanya kazi Mpaka Zanzibar kwenye yale mambo tunayosema ya-Muungano. Kwa hiyo ni sawa na Kusema Serikali ya Tanganyika inafanya maamuzi ya Zanzibar wakati serikali ya Mapinduzi ya Zenj haina haki hiyo. Mnaonaje, Tusiseme kasoro? Tutarekebisha nini? Kwa mtindo huo wa kuionea haya historia kwa kujidai tunaijua, kero hizi zitakwisha?

Kimtizamo sikubaliani. Badala yake nasisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuisikia historia yao tena na tena bila kukerwa wala kuionea haya. Hata kama inachanganya kichwa. tukumbuke kuwa watoto wetu wengi hawajui hiyo historia kwa sababu iliyopo kwenye vitabu ni ya uongo. Na hata hiyo ya uongo haiwafikii tena kwa kuwa hizo shule za kata hazina vitabu.

Yale mawazo ya mwenzetu ZZK, kwa mtazamo wangu, yalikuwa na walakini!
 
Kichwa cha Habari kimekaa kizushi. Lissu ni namba nyingine vijembe vya Zitto haviwezi kuhafifisha hoja zake. Huwezi kujenga Taifa la baadaye bila kutathimini tulikotoka, wapi tulikosea na tusahihishe Vipi. Mimi namuumga mkono Lissu kutupa ukweli wa lile mwalimu alichotufanyia watanzania.
 

Hii ina uhusiano gani na hoja iliyoko mezani. Are you BAVICHA in making?

Yaani kwa ujinga wako unabadilisha jina kwenye phonebook ya simu moja na kuandika jina la Ridhiwani Kikwete halafu unatumia simu nyingine ku-text ili ionekane aliyekuwa ana text in Ridhiwani Kikwete halafu una save screenshot na kuleta hapa kwenye jukwaa la watu walioenda shule.

Tatizo watu kama wewe mmepewa kazi za spinning za kisiasa ambazo ziko juu ya uwezo wenu.

Kwa mtu ambaye siyo mtaalamu wa computer programming ndiyo anaweza kuukubali huu upuuzi kuwa ni kweli.


Kwenye ulimwengu unaochagizwa na 0 or 1 digitally, everything is possible.

Hizo childish spinning zinaweza kukubalika kwenye ofisi za BAVICHA.
 
Hatutilii maanani maneno na michango yq mbunge wa mahakama
 
Yaaani hili neno intarahamwe nimelipenda sana sijui prof alifikiriq nini
 
Hii ina uhusiano gani na hoja iliyoko mezani.

Kwa mtu ambaye siyo mtaalamu wa computer programming ndiyo anaweza kuukubali huu upuuzi kuwa ni kweli.

Kwenye ulimwengu unaochagizwa na 0 or 1 digitally, everything is possible.

Hizo childish spinning zinaweza kukubalika kwenye ofisi za BAVICHA.

Kuna hoja gani uliyoi "table" hapo, kijembe kwa Lissu ni kipi hapo. Hangaikeni na Lowassa wenu hapo, na mwana wa mfalme kasema Lowassa hagusi kwao "magogoni" patamu hapo. Magamba yanapapatuana.
 
Ni wapi jina la Lissu limetajwa?
You need to possess thinking capacity which strive to get below surface of Zitto argument.

You need to have skills of persistence to examine and re-examine an argument in order to take in all the angles and measure with evidence.

Kama unasubiri mpaka jina litajwe, endelea kusubiri labda litatajwa.
 
Intarahamwe mnatapa tapa sana mwaka huu..

Mmeshikwa pabaya sana

Intarahamwe wanaingia vipi hapa?.

Hebu jaribu angalau kujenga hoja kulingana na msingi wa hoja uliopo mezani.
 
You need to possess thinking capacity which strive to get below surface of Zitto argument.

You need to have skills of persistence to examine and re-examine an argument in order to take in all the angles and measure with evidence.

Kama unasubiri mpaka jina litajwe, endelea kusubiri labda litatajwa.

Kwa hiyo humo ulimochora kizungu ndo kuna jina Lissu... you're just another rubber sheath...
 
MwanaDiwani, umemsoma hapo juu measkron, naona umepita fyaaaa!

Ndugu, nimemsoma na nimemjibu kulingana na uwezo wa akili na fikra zake.

Alichokifanya ni sawa sawa na kuandika post card digitally.

Ni kwa watu wenye uelewa mfupi wa mambo ya digital print ndiyo wanaweza kukubaliana na kile alichokiweka.
 
Last edited by a moderator:
Hatutilii maanani maneno na michango yq mbunge wa mahakama
Unafahamu maana ya kutilia maanani?.

Hata kuandika tu kuhusiana na jambo lenyewe inabainisha unatilia maanani.

Wewe niwa kuonewa huruma tu kwa sababu hufahamu hata unachokifanya!
 
Unawezaje kutibu ugonjwa bila kujua chanzo?

Ni Wa-Tanzania wachache sana kati ya ml 45 wanaojua kuhusu muungano na kero zake..Tusipotoshe Elimu Tz inahitajika sana..

Kuhusu Lisu..Mbona hajatajwa kwenye hii Video? MwanaDiwani acha umbea..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom