Zitto Kabwe ampiga 'kijembe' Tundu Lissu kuhusu hoja za hati ya Muungano.

Zitto Kabwe ampiga 'kijembe' Tundu Lissu kuhusu hoja za hati ya Muungano.


attachment.php
 
Wakati akichangia hoja za Kamati za Bunge Maalumu namba moja hadi 12, juu ya Sura ya Kwanza na Sura ya Sita ya Rasimu ya Katiba, Zitto Kabwe alisema wajumbe hawako Bungeni kwa ajili ya KUKUMBUSHANA HISTORIA YA TANZANIA KUHUSU MUUNGANO, kwa maana kuwa, kujadili hati za muungano ni useless and uncalled for bali wabunge wako bungeni kutafuta mfumo wa uendeshaji wa maisha ya wananchi wa leo na kesho utakao kubaliwa na wananchi wengi na siyo mfumo wa jana.

Tunaielewa historia ya nchi yetu, hakuna haja ya kukumbushana, tuepuke lugha za matusi, chuki, ubaguzi, tubakie na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Zitto.

Zitto Kabwe alibainisha na kusema, Mchakato huu tuufanye kwa kujadiliana kwa hoja, tusitukanane, muundo wowote wa serikali unaweza kuvunja Muungano, kikubwa ni kuafikiana maridhiano kutoka pande zote mbili za Muungano.

Kabwe Zitto amesema muundo wowote wa serikali uwe serikali moja, mbili au tatu unaweza kuvunja Muungano ikiwa hakutakuwa na muafaka wa pande zote mbili za Muungano.

Katika hatua nyingine Zitto alisema ikiwa itaundwa serikali isiyo na maridhiano ya pande zote mbili za Muungano, gharama ya kuulinda Muungano huo itakuwa ni kubwa sana.

[video=youtube_share;nFRJDBXZJVo]http://youtu.be/nFRJDBXZJVo[/video]

Hopeless you
 
Jamani alikuwa anamaanisha historia ya zanzibar ambayo wenye kujua wanajua iliambatana maumivu makubwa kwa hio tusameheane na tusonge mbele maana tukianza kuchokonoa tutarudi kulekule kwenye chuki na visasi.ambako ndiko ndugu zetu wanataka kuturudisha ili tupate machungu tuanze kuulizia ndugu zetu kama kassim hanga na wengine wengi walouawa kikatili ndani na nje ya asp.tusamehe na tusahau.sasa hawa walofanya haya mambo cha kushangaza badala ya kuwa wapole bado wanasema hawajatosheka wanatoa kauli za vitisho ndio maana zitto anasema tuyaache hayo ni mambo makubwa sana kuna watu wataenda the hague na wala sio hati ya muungano.suala la hati ni more academic na ni vigumu kwa watu wa kawaida kulielewa.lakini Lissu ana hoja ya kisomi na hata akienda mahakamani atashinda hamna hati pale zile hati za kughushi kama ulivyo muungano wenyewe.nini kifanyike? Hamna namna sasa ni wakati wa kuuweka vizuri kisiasa na kisheria ili watoto wetu ambao watakuwa watundu kuliko sisi wasije wakapelekana mahakamani kuhusu suala hili.
 
Hauwezi kuchambua kitu au kujadili katiba kwa undani kama haujui history, Zitto kachemka.
 
Zitto anafikil watanzania wote wanaijua historia ya nchi kama wana siasa. Mi namkubal Lissu amefanya watu wengi tukanza kujua Tanganyika ilivyo kufa
 
huyu ana busara sana sijui kwa nini wengine hawatambui hili
 
Kinachonisikitisha ni kwamba,"""" historian ya ukoo wenu unaijua hadi kwa babu yako mzaa baba. And not beyond that"""""
Vipi ulishawahi kuomba Cheti cha nndoa cha wazazi wako?????? Au bado wanaishi Pasi na mapenzi ya mungu?????

Just look at yourself! Kwamba unaona aibu kujua historia yako? Au unaona madhambi mliyoficha ndani ya historia hiyo ni hayafai watu wengine kuyajua?

Let me tell you this. Wale Watanzania wa kipindi kile, wale mliokuwa mnawaambia upuuzi wanawasikiliza na wanawaelewa, wale hawapo, mmebaki wachache sana. Na ukiangalia ni vijana mlio na mawazo ya kizee tu. And that is not my problem, neither is ours! Mtaendelea kubaki wachachache, mtaendelae kupungua mpaka mtaisha. I thank God kwamba Wananchi wanazidi kuamka, na uelewa wao unaongezeka and they are curious. Wanataka kujua everything. Na wana haki hiyo pia! That I like!

Mwisho, nakuhakikishia kuwa jamii bora ni ile inayojua ilikotoka na inakokwenda. Binafsi nadhani haina haja kuonea aibu past yetu. Kila mtu anajua we can not change it. But we can do something about tomorrow, perhaps today. Lakini HATUWEZI KUFANYA HIVYO TUSIPOJUA TULIKOSEA WAPI. Ni watu wa ajabu tu, wanaopenda kuishi dunia ya kusadikika, ndiyo wanaoweza kuionea aibu historia yao. Na sana siyo kwa kuwa historia yao ni mbaya, la hasha! ni kwa kuwa that same history will show people of what kind of animals their leaders have been! And that, nna uhakika ndicho kinachokusumbua wewe na wenzio wenye mawazo kama yako.

Lakini mimi na watoto wangu, pamoja na wapenda maendeleo wote, TUTAIPENDA NCHI HII, hata kama ilikotoka kulikuwa kubaya, TUTAIPIGANIA hata kama nyie hamtaki na TUTASHINDA tu hata kama itachukua muda! That is a fact. Note this kwa sababu you will learn it as you see it coming! Mabadiliko ni lazima na hayapingiki. Hakuna sehemu yoyote ambapo wengi walitaka mabadiliko yakazuiwa. Take that as a lesson my dear. Many thanks.
 
Mtu mwenye busara na ufahamu ni yule anaeweza kutowa hotuba nzuri na asitaje jina la mtu wala chama chochote na hotuba ujumbe ukafika kwa mlengwa
Ndugu, watu kama hawa hawawezi hata kuelewa kuna kitu inaitwa kuhusika kimazingira au ushahidi wa kimazingira.

Ninewaambia walisubiri hilo jina litajwe ili waanze kujenga hoja.
 
Yah, Zitto is one of the best young leader who has very bright future in this Nation. The guys is bright, full of wisdom and he can play his cards very well

Bravo Zitto
Young leader kila siku? Hazeeki kama kingunge sio!
 
Yah, Zitto is one of the best young leader who has very bright future in this Nation. The guys is bright, full of wisdom and he can play his cards very well

Bravo Zitto
Young leader kila siku? Hazeeki kama kingunge sio!
 
Intarahamwe wanaingia vipi hapa?.

Hebu jaribu angalau kujenga hoja kulingana na msingi wa hoja uliopo mezani.

Mbona mimi naona kama Zitto amewapiga KIJEMBE CCM ambao nguzo ya madai yao ni kwamba serikali 3 zitavunja muungano, kitu ambacho Zitoo anakanusha kwamba bila maridhiano serikali 1,2,3 hazitasaidia zitavunja muungano. Mimi nilifikiri kama GT usinge miss hiyo nukta iliyobeba ujumbe wote wa Zitto.
 
Hii ina uhusiano gani na hoja iliyoko mezani. Are you BAVICHA in making?

Yaani kwa ujinga wako unabadilisha jina kwenye phonebook ya simu moja na kuandika jina la Ridhiwani Kikwete halafu unatumia simu nyingine ku-text ili ionekane aliyekuwa ana text in Ridhiwani Kikwete halafu una save screenshot na kuleta hapa kwenye jukwaa la watu walioenda shule.

Tatizo watu kama wewe mmepewa kazi za spinning za kisiasa ambazo ziko juu ya uwezo wenu.

Kwa mtu ambaye siyo mtaalamu wa computer programming ndiyo anaweza kuukubali huu upuuzi kuwa ni kweli.


Kwenye ulimwengu unaochagizwa na 0 or 1 digitally, everything is possible.

Hizo childish spinning zinaweza kukubalika kwenye ofisi za BAVICHA.

Nashukuru jamaa kuweka pia nakushukuru wewe zaidi kwa kunielimisha na kunifumua.
 
Wakati akichangia hoja za Kamati za Bunge Maalumu namba moja hadi 12, juu ya Sura ya Kwanza na Sura ya Sita ya Rasimu ya Katiba, Zitto Kabwe alisema wajumbe hawako Bungeni kwa ajili ya KUKUMBUSHANA HISTORIA YA TANZANIA KUHUSU MUUNGANO, kwa maana kuwa, kujadili hati za muungano ni useless and uncalled for, bali wabunge wako bungeni kutafuta mfumo wa uendeshaji wa maisha ya wananchi wa leo na kesho utakao kubaliwa na wananchi wengi na siyo mfumo wa uendeshaji wa jana.

Tunaielewa historia ya nchi yetu, hakuna haja ya kukumbushana, tuepuke lugha za matusi, chuki, ubaguzi, tubakie na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
,” alisema Zitto.

Zitto Kabwe alibainisha na kusema, Mchakato huu tuufanye kwa kujadiliana kwa hoja, tusitukanane, muundo wowote wa serikali unaweza kuvunja Muungano, kikubwa ni kuafikiana maridhiano kutoka pande zote mbili za Muungano.

Kabwe Zitto amesema muundo wowote wa serikali uwe serikali moja, mbili au tatu unaweza kuvunja Muungano ikiwa hakutakuwa na muafaka wa pande zote mbili za Muungano.

Katika hatua nyingine Zitto alisema ikiwa itaundwa serikali isiyo na maridhiano ya pande zote mbili za Muungano, gharama ya kuulinda Muungano huo itakuwa ni kubwa sana.
Haihitaji uwe msomi kujua habari hii ni umbeya na uzandiki.Ukiangalia nilipokoleza utagundua wanaopingwa na kusemwa ni CCM wala siyo TL.
 
Back
Top Bottom