Zitto Kabwe: Anayefikiri Tanzania itapata Katiba Mpya bila kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi hana ubongo

" Yeyote yule anayefikiri kuwa Tanzania itapata katiba mpya bila kwanza kuwa na Tumehuru ya uchaguzi hana ubongo" Zitto

Inaelekea Zitto na chama chake wanategemea kuwa kwa vyovyote vile watapata viti vya kuridhisha Zanzibar ambavyo vitawawezesha kuwa Chama Kikuu rasmi cha upinzani Bungeni. Mpaka sasa hivi hajaweza kuelezea huo uhuru wa Tume hiyo utahakikishiwa vipi bila ya kuwa na Katiba Mpya? Aidha, wenzake wameeleza kuwa Tume ni sehemu tu ya mfumo wa uchaguzi mkuu. Wanaokataa kutoa fomu kwa wagombea, wanaokata majina ya wapinzani, wanaowatia ndani wagombea wa upinzani n.k. sio Tume. Mwaka 2020 kuna mgombea wa Chadema alitaka kunyimwa fomu za uchaguzi kwa kisingizio kuwa zimeishachukuliwa na mgombe wa Chadema. Mpaka sasa hivi ACT wamegombea sehemu nyingi tu na wameshinda kiti kimoja tu kwa mbinde. Nini kinamuaminisha kuwa nini kitakuwa tofauti 2025? Anaamini kuwa wakurugenzi watabadilika madoa? Kwa kweli hatutendei haki.

Amandla...
 
Haka ka jamaa hivi hakajajijua kwamba hakaaminiki tena? mlio karibu nako hebu kaambieni.
 
Hivi katiba mpya inasaidiaje wapinzani kupata madaraka?!
Wapinzani wengi wa Tanzania na wafuasi wao wamejaa funza vichwani.

Kuna nyumbu wanamshambulia Zitto kwa sababu tu ni Zitto. Yaani hawana hoja ya msingi ya kuonesha kwanini Katiba Mpya inatakiwa kuanza kabla ya Tume huru.
 
Lengo la Katiba mpya sio kuwapa upinzani madaraka. Lengo ni kuhakikisha kuwa mshindi anashinda katika mazingira ya uwazi na haki.

Amandla...
Sasa unatakiwa kuelewa kuwa mchakato wa Katiba mpya unaishia kwa wananchi kupiga kura ya kuunga mkono Katiba mpya au kuikataa, hilo zoezi linasimamiwa na Tume ya uchaguzi ambayo nyumbu wa Chadema wanasema haina haja ya kufanyiwa reforms.
 
Sio lazima iwe hivyo. Na wanachosema Chadema ni kuwa total overhaul ya Tume haiwezi kufanyika chini ya katiba iliyopo. Wanaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa uchaguzi wa huru na haki utapatikana pale tu wale wote wanaohusika kwa njia moja na uchaguzi watakapokarabatiwa na kuwekwa huru chini ya Katiba Mpya. Kitu cha msingi ni wenye mamlaka kukubali kuwa kuna haja ya haki kutawala process nzima ya uchaguzi. Njia pekee ya kufanya hivyo ni kuwa na Katiba inayohakikisha haki kwa washiriki wote. Hata ukiwa na kitu kinachoitwa Tume Huru, ni kazi bure kama wasimamizi wa uchaguzi wataendelea kuwa makada wa chama kimoja na vyombo vya dola kuona kuwa ni wajibu wake kulinda maslahi ya upande mmoja. Ndio maana hao nyumbu wa Chadema wanasema reforms kwa sake ya reform tu, haitoshi. Na hasa kama reform hizo zitakuwa limited kwenye Tume ya Uchaguzi peke yake.

Sasa, kwa nini watu wasijikite kujibu hoja za CHADEMA kama ulivyoziainisha hapa, na badala yake wanashikilia tu "TUME HURU", bila hata ya kueleza hiyo tume huru itapatikana vipi!

Sasa huyo anayesema wengine hawana "ubongo', aeleze, hiyo tume huru ataipata kwa njia zipi.
 
Wapinzani wengi wa Tanzania na wafuasi wao wamejaa funza vichwani.

Kuna nyumbu wanamshambulia Zitto kwa sababu tu ni Zitto. Yaani hawana hoja ya msingi ya kuonesha kwanini Katiba Mpya inatakiwa kuanza kabla ya Tume huru.
Badala ya kujibu swali unakimbilia kuwashambulia wapinzani 🙁
 
Lengo la Katiba mpya sio kuwapa upinzani madaraka. Lengo ni kuhakikisha kuwa mshindi anashinda katika mazingira ya uwazi na haki.

Amandla...
Ni kweli ila nashangaa huyu jamaa Pohamba anajenga hoja kwamba katiba mpya ni njia ya wapinzani kupata madaraka kwa mkato, so namuuliza inakuaje katiba mpya inasaidia wapinzani?

Ina maana ccm haiwezi uchaguzi chini ya katiba mpya?!
 
Mzito kabwela, analipwa kule analipwa huku daadeki ni kama prof Lipumbavu tu alipopewa mission ya kuiua CUF kajamaa wamekatumia sana kwenye mishe zao ila kana benefit kwakua ndi ajira yake
 
Msimamo wa Zitto kutoka moyoni kwake huu hapa😁😁😁
 
..Michakato ya kupata Tume Huru na Katiba mpya inatakiwa iende kwa pamoja.

..Hili suala linahitaji MARIDHIANO na sio upande mmoja kushambulia upande mwingine.

..CCM wanataka kutokee ugomvi kati ya Tume Huru vs Katiba mpya ili tufike 2024/25 tukiwa tumekosa vyote.
Hapana.

Ni wazi/dhahiri, sheria mama (Katiba), ndiyo inayotoa maelekezo namna ya kupata Tume Huru. Hapa hakuna mkanganyiko wa aina yoyote ile.
 
Sio lazima iwe hivyo. Na wanachosema Chadema ni kuwa total overhaul ya Tume haiwezi kufanyika chini ya katiba iliyopo. Wanaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa uchaguzi wa huru na haki utapatikana pale tu wale wote wanaohusika kwa njia moja na uchaguzi watakapokarabatiwa na kuwekwa huru chini ya Katiba Mpya. Kitu cha msingi ni wenye mamlaka kukubali kuwa kuna haja ya haki kutawala process nzima ya uchaguzi. Njia pekee ya kufanya hivyo ni kuwa na Katiba inayohakikisha haki kwa washiriki wote. Hata ukiwa na kitu kinachoitwa Tume Huru, ni kazi bure kama wasimamizi wa uchaguzi wataendelea kuwa makada wa chama kimoja na vyombo vya dola kuona kuwa ni wajibu wake kulinda maslahi ya upande mmoja. Ndio maana hao nyumbu wa Chadema wanasema reforms kwa sake ya reform tu, haitoshi. Na hasa kama reform hizo zitakuwa limited kwenye Tume ya Uchaguzi peke yake.

Amandla...
Issue ya ku demand Katiba Mpya kwenye jamii ya watu walioelimika haipaswi kuhodhiwa na chama fulani cha siasa. Ukiona maelezo yamejikita kwenye uchadema au uzambarau ujue kama taifa bado hatujajua nini cha kufanya.
 
Back
Top Bottom