Zitto Kabwe asubiriwa na Bunge kueleza lengo la barua yake Benki ya Dunia kuzuia mkopo wa kuboresha Elimu (SEQUIP)

Zitto Kabwe asubiriwa na Bunge kueleza lengo la barua yake Benki ya Dunia kuzuia mkopo wa kuboresha Elimu (SEQUIP)

Nani angemsikiliza? Sana sana angezomewa na wagonga meza. Kwani ni mikataba mingapi ya hovyo imepitishwa pale bungeni? Wapinzani wakipinga na kutaka maboresho wanazomewa na kutolewa nje. Leo hii supika ndiyo anasema angemsilikiliza Zitto?

Sent using Jamii Forums mobile app

Nani aliwahi kutolewa bungeni kwa kutoa mapendekezo ya maboresho ya sera?
 
Kazi za mbunge zimeanishwa wazi kabisa hiyo ya kuwasiliana na benki ya dunia kwa kutumia Ofisi ya bunge na karatasi yenye nembo ya bunge haimo kwenye kazi za mbunge.
Kazi za mbunge zimeainishwa wapi na ni zipi?

Kwa nini mbunge kuwasiliana na benki ya dunia si sehemu ya kazi za mbunge?

Wapi imeandikwa hivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugai hajui kuwa licha ya Zitto kuwa Mbunge lakini bado ni mwananchi wa Tanzania na anahaki ya freedom of speech na kufanya yote anayoweza kufanya katika kushape maamuzi na sera za serikali ilimradi havunji sheria?.

KWANI ZITTO KAVUNJA SHERIA GANI YA NCHI?
 
Ndugai amesema kama kulikuwa na tatizo la kisera, ni mambo ya kujadiliwa bungeni. Sio mara ya kwanza kutokea sera zikawa na udhaifu au zinahitaji maboresho.

Anasema Zitto alipaswa awasilishe maoni yake na mapendekezo kuhusu ubovu wa sera ya elimu kisha litazamwe. Ndio kazi za bunge.

Sasa yeye anaenda kupiga kelele nje ya nchi kwa sababu hakubaliani na sera kweli?

Awajibishwe.
Zitto njoo huku mkuu, kuna watu wanataka kudondoka kwa pressure!!
 
Back
Top Bottom