Zitto Kabwe asubiriwa na Bunge kueleza lengo la barua yake Benki ya Dunia kuzuia mkopo wa kuboresha Elimu (SEQUIP)

Zitto Kabwe asubiriwa na Bunge kueleza lengo la barua yake Benki ya Dunia kuzuia mkopo wa kuboresha Elimu (SEQUIP)

Tulikataa USD 500 million za Millennium Challenge Account mwaka 2016 na tumedunda miaka yote hiyo bila tabu. Sasa tatizo liko wapi kama tunanyimwa million 500 leo?

Inaelekea Zitto yuko sawa .... Pesa ya kampeni itakuwa imepwelea!!
 
Spika Job Ndugai amesema wanamsubiri Mbunge Zitto Kabwe awaeleze kwanini aliandika barua kwa Benki ya Dunia kuzuia mkopo kwa ajili ya elimu nchini.

My take huyu jamaa anayejiita Zitto sisi wananchi wa Kigoma tutamuadhibu kwenye sanduku la kura.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sema mtalazimisha ushindi. Lakini hilo halitawasaidia, unadhani anahitaji kuwa bungeni ili atoe maoni yake na kusikilizwa? Tutaanzisha petition ya bidhaa za Tanzania kususiwa kimataifa hadi mshike adabu. Na sio kazi kubwa sana.
 
Nani angemsikiliza? Sana sana angezomewa na wagonga meza. Kwani ni mikataba mingapi ya hovyo imepitishwa pale bungeni? Wapinzani wakipinga na kutaka maboresho wanazomewa na kutolewa nje. Leo hii supika ndiyo anasema angemsilikiliza Zitto?

Sent using Jamii Forums mobile app
Asingemsikiliza,akithubutu kufanya hivyo(Akimpa nafasi ya kuongelea hiyo Sera Bungeni hata yeye Ndugai angekiona cha moto tokea kwa jiwe na wapambe wake.
Namshauri kama anaona vipi aruhusu muswada wa Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba ya Wananchi.
Akiwezesha hilo tutampigia kampeni arejee Binge LA 12 na awe Spika wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi za mbunge zimeanishwa wazi kabisa hiyo ya kuwasiliana na benki ya dunia kwa kutumia Ofisi ya bunge na karatasi yenye nembo ya bunge haimo kwenye kazi za mbunge.
Na hilo nalo pia ni kosa jingine kubwa. Barua aliyoiandika hakuwa ametumwa na Bunge, ilikuwa ni yake binafsi, na hakutakiwa kuisaini akiwa anaonyesha kuwa ni Mbunge wa JMT, bali alitakiwa aisaini akiwa anaonyesha kuwa ni Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT. Mandate iliyomfanya aandike barua hiyo ni Uongozi wake ndani ya chama anachokiongoza na si kama Mbunge wa JMT. HIlo ni kosa jingine kubwa, tena kubwa asana
 
Zitto kwenye barua yake kwenda WB kaweka icon ya bunge la Tanzania bila idhini ya bunge
Ndugai hajui kuwa licha ya Zitto kuwa Mbunge lakini bado ni mwananchi wa Tanzania na anahaki ya freedom of speech na kufanya yote anayoweza kufanya katika kushape maamuzi na sera za serikali ilimradi havunji sheria?.

KWANI ZITTO KAVUNJA SHERIA GANI YA NCHI?
 
Back
Top Bottom