Zitto Kabwe asubiriwa na Bunge kueleza lengo la barua yake Benki ya Dunia kuzuia mkopo wa kuboresha Elimu (SEQUIP)

1) amejua kujenga na kutetea hoja wakamuelewa
2) Zitto kawakilisha tu kundi kubwa la watetezi wa haki elimu kwa wasichana wa Tanzania
3) Ndugai, bunge lako limekuwa part ya serikali.....limekuwa hovyo kabisa na dawa ni kuli-bypass
4) afuate urasimu wa kuwasilisha mabadiliko ya sera wakati document linasogea mbele?
5) hata angeleta hoja bungeni, jibu tunalijua kwamba mngekataa
 
Kazi za mbunge zimeanishwa wazi kabisa hiyo ya kuwasiliana na benki ya dunia kwa kutumia Ofisi ya bunge na karatasi yenye nembo ya bunge haimo kwenye kazi za mbunge.

Huu ni mwendelezo wa ujinga wetu. Kwa nini tuna avoid tatizo la msingi? Hayo mambo anayolalamikia Zitto ni mambo ambayo yamekosa suluhu ya ndani kwa sababu yanapigiwa kelele kila kona na watu wengi sana including hata jumuia za kimataifa. Bila ku review hii misimamo ya kibabe hali itakuwa ngumu Zaidi huko tunakokwenda. Tukubali kuwa kuna njia bora Zaidi ya ke deal na hizo issue kuliko tuliyochagua. Baba huwezi anzisha ugomvi na jirani yako wakati anakuzidi ubavu huko ni kutafuta aibu kubwa zaidi.
 
Interest,

Ningeshangaa sana kama spika asingekuwa upande huu. Miswada yote hupita kwa sauti kubwa ndiyoooooooooo hivyo basi ninaona wachache wamegundua pa kusemea na kusikilizwa.

After all shida iko wapi tunajenga nchi yetu kwa mapato yetu ya ndani. Dr Abasi jana kasema kwamba kwa makusanyo tumevunja rekodi ya dunia. Naamini hilo pengo la WB litazibwa bila issue yoyote.
 
Zitto yupo sahihi kwani kosa lake likowapi wakitaka kusema mnawaziba midomo wafanyaje sasa kila mtu apambane na hali yake na sisi nimatajiri hatuna shida na misaada wala mikopo tuache porojo tukafanye kazi FANYENI KAZI WAUNGWANA
 
Sielewi... naomba unielimishe Tafadhali
 
Unapokuwa mbunge kwenye Bunge la Tanzania ujue kuwa ubunge wako unatambuliwa na Jumuia ya Madola kwa sababu Bunge la Tanzania ni mwanachama wa mabunge ya Jumuia ya Madola.
Ni sawa, unachosema, vyovyote vile anatambulika na WB. Hata wewe hapo ulipo, WB wanakutambua aidha kama raia wa Tanzania au kwa cheo kingine uchochte lichonacho, hata kama hakina uhusiano na malaka za Serikali. Na kwa swala hili basi, alitakiwa aandike barua aidha kama mtu binafsi, au Kiongozi wa ACT Wazalendo, na si kama Mbunge kwa sababu Bunge halikuwa na hoja hiyo. Hapa kinachogomba ni kuwa ameandika barua kama Mbunge, kulisingizia Bunge hoja ambayo halikuwa nayo, ni hoja ya chama chake au ya kwake binafsi. Amefanya vizuri lakini kwa sababu amejiingiza kwenye target ya Bunge pasipo mwenyewe kujua
 

Hawa watu wanatudharau sana wanafikiri wwatanzania wa leo hawana access na information wala uwezo wa kufikiri. Na wanajisahaulisha haraka sana. Ila wanachoumbani kitu kibaya sana kwa nchi yetu.
 
Zitto Kabwe kaitendea haki Kigoma kwa kuwa Mbunge anaetetea maslahi ya watoto wa Kike bila kujali itikadi zao.

Hakika huyu ni Mbunge wa Mfano,Bunge linayomengi ya kuhoji kabla ya kumuhoji Zitto.

Bunge lihoji ujenzi wa Chato International Airport bajeti ilipitishwa wapi?

Bunge lihoji waliompiga risasi mbunge mwenzao.

Ndugai ahoji kwanza waliomfukuza ubunge Mgonjwa aliepigwa risasi kiwa anwajibika Bungeni.

Vitishi vya Ndugai visimrudishe Zitto nyuma bali ajue kuwa Watanzania wanafuatilia na sasa wamejiridhisha kuwa yupo sahihi.

CCM wameumizwa na Barua ya Zitto huku wakijua kuwa Zitto si miongoni mwa wanaowaunga mkono.

Tunaelekea uchaguzi mkuu,Dunia lazima ielekeze macho Tanzania kuwatazama mwewe wenye njaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Ni muda gani zitto anakuwa si mbunge? Huko shuleni mnaenda kusomea nini
 
Hatuichukii nchi yetu. Tunaipenda. Isipokuwa, tunatofautiana na serikali katika masuala mengi. Serikali inapita. NCHI YETU inabaki. Tutaendelea kuipenda nchi yetu na tofauti zetu na serikali zitaendelea kuwepo. Hadi waheshimu haki za binadamu, demokrasia na utawala bora.

Pesa za mabeberu zinanuka damu. Au sio waungwana? Hakika, tulikubaliana hivyo kwenye kikao kilichopita. inatushangaza wengi sana kwanini serikali ya CCM inazililia na kutoa machozi kwa hizi US$500M!

Kama zilivyo benki zote.Kila benki ina vigezo vyake vya kutoa mkopo.ukienda NMB watakuambia uwe na hati,kitambulisho nk. World Bank wana vigezo, demokrasia uhuru wa habari,n.k wabunge waposema Zitto amezuia mkopo mbona hawaoni vigezo CCM walivyokiuka.Donor country inalilia mkopo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitto anayo IQ kubwa kudeal na watu wasiojali tena sheria na katiba yetu.

World Bank watakuwa wamezuia huo mkopo,kama wamezuia litakuwa jambo jema,wasubiri mpaka Rais mpya aingie madarakani mwezi Novemba ndio walete hizo pesa,sasa hivi fedha itaelekezwa kusaidia CCM kwenye uchaguzi,ukisikia kelele za wana CCM ujue nyundo imetua utosini.Wananchi naona wanashangilia kila kona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kumbe sindano imewakolea?
 
Kwamba Zitto akiwa kiongozi wa chama cha ACT anaoteza sifa ya kuwa Mbunge?

Hakuna mipaka ya Ubunge wa Zitto ilimradi anachokifanya kipo ndani ya sheria.

Zitto shika hapohapo,hawana hoja mbadala ,sasa naona wanahaha na kudhani vitisho vitawasaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…