Zitto Kabwe asubiriwa na Bunge kueleza lengo la barua yake Benki ya Dunia kuzuia mkopo wa kuboresha Elimu (SEQUIP)

Mkuu Ni muda gani zitto anakuwa si mbunge? Huko shuleni mnaenda kusomea nini
Na wewe ni mgumu kuelewa! Sikatai kwamba Zitto hana mamlaka ya kuandika barua WB akiwa kama Mbunge, hapana, mamlaka hayo anayo. Hoja ni kwamba, alichowaandikia WB ameandika akiwa kama mpinzani, kitu ambacho pia ni sahihi. Alichokosea ni kuandika barua ikiwa na mandhari inayoonyesha kuwa imeandikwa na Mbunge wa JMT, hicho ndicho hakiko sahihi. Alitakiwa aandike aidha kama raia wa Tanzania, au kama Kiongozi wa Chama. Huwezi ukatumia headed paper ya Bunge kuandikia barua nje ya mipaka ya nchi yetu, barua yenye kubeba maudhui ya chama cha upinzani. Au ukaisaini barua hiyo kama mbunge, hapana Labda kama ingekuwa ni hoja ya wapinzani Bungeni na si ya mtu mmoja ambaye pia ni kiongozi wa chama cha upinzani
 
Rai yangu zitto alindwe yasije yakatokea yaleyale ya lissu.ccm Ni makatili sana.
 
Hahaa kweli wewe una tatizo, mipaka ya mbunge inaishia ndani tu? Huna hoja boss
 
Haijalishi ana ushawishi au hana, issue hapa ni kwamba ameandika barua ya kuzuia hela zisije kwenye Nchi yake anayoishi
Weka vizuri, kazuia zisiende kwa serikali ya awamu ya tano ili wapewe ccm kwa mgongo Wa kunua vyuo vyake.
 
Saw
Unapokuwa mbunge kwenye Bunge la Tanzania ujue kuwa ubunge wako unatambuliwa na Jumuia ya Madola kwa sababu Bunge la Tanzania ni mwanachama wa mabunge ya Jumuia ya Madola.
Sawa sio tatizo, zitto kapewa ubunge Na wananchi kwa miaka mitano, mwenye haki ya kulalamika Ni wananchi wake Na sio mende mwingine yeyote.
 
Kweli kwa ccm Na serikali yake, zitto Ni msaliti.
 
Kwa trump wapinzani wanapewa nafasi sana, sio hapa bongo. Kina mbowe wamebambikiziwa makesi mengi hatari
 
Kwa trump wapinzani wanapewa nafasi sana, sio hapa bongo. Kina mbowe wamebambikiziwa makesi mengi hatari

sasa si bora wapinzani wa usa, wanongea malengo! sasa bongo kuna upinzani? kwa mfano kuna chama kimoja wamekuja na sera ya kuwakata ela matajiri ikasaidie maskini na imepitishwa na chama chao ndo imekua sera kuu mda wote sasa uku mnasubiri ccm wafanye uovu alafu nyie muende na wave, upinzani gan sasa huu
 
Ndugu tujuze hawa CCM wamekiuka vigezo vipi hapa naona kiza tu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Z
Wananchi tunampokea Zitto kwa shwangwe Ndugai akameze vidonge vyake
Nani Ampokee Zitto wakati kwenye vijiwe vya Jukwaa la meza ya Duara, Murusi , Ngomeni, na Vijiwe vya kahawa hapa Kigoma ujiji kila Mtu ameshikwa na butwaa kitendo cha Zigo, wanashangaa. Wengine wanajua itakuwa vir vimekimbilia kichwani ndiyo amechanganyikiwa πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
amelinajisi bunge. Huyu bwana hafai kurudi bungeni mwaka huu...

Wananchi wa kigoma mpingeni huyu bwana kwa nguvu zote, ni msaliti wa taifa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…