Zitto Kabwe asubiriwa na Bunge kueleza lengo la barua yake Benki ya Dunia kuzuia mkopo wa kuboresha Elimu (SEQUIP)

Zitto Kabwe asubiriwa na Bunge kueleza lengo la barua yake Benki ya Dunia kuzuia mkopo wa kuboresha Elimu (SEQUIP)

Ningekuwa mimi nisingempa nafasi Zitto aeleze bunge kwani atashinda kimantiki labda watumie hoja ya nguvu lkn kwa nguvu ya hoja Zitto anashinda. Kosa pekee alilotenda, kama ni kweli, ni kutumia nembo ya bunge.
 
Interest,
Alitegemea apeleke hiyo hoja bungeni ijadiliwe?
Kwani hizo pesa zinatolewa na na bunge au serikali ya tanzania? Yeye alipeleka hoje kwa wale wanaotoa mkopo.

Sasa ndugai anataka bunge la ccm ambalo limeshaamriwa wapitishe kila kitu wangeipinga hiyo hoja ya kukopa, wakati hizo pesa zilikuwa zitumike kuwasaidia wao kwenye uchaguzi 2020?
 
Mabeberu mnaowapigia magoti wawapande kisa mkopo, au mabeberu gani unayomaanisha.

Umesikia maccm yalivyokwapua hela za Epassport? Maccm yameiba Tr 1 dili fake....
Sasa Ndunga si apige kelele na hayo mahela ma trillion hayo yaliyokwapuliwa yarudi yakahudumie elimu badala yake ndunga akaishia kula na CAG na bado anataka kumtafuta Zitto.Zitto ni mtetezi wa kweli wa wanyonge.Na sio mnafiki kama.....

Inasikitisha sana kuona jinsi ambavyo baadhi ya wabunge wasivyoweza kutetea wananchi.Zitto ameona mbali na kutambua kuwa mwisho wa siku huo mkopo ukipita mwananchi mnyonge mwenye mlo mmoja kwa siku ndiye atakayebebeshwa limzigo hilo na wananchi wengi tumeliona hilo.

Wabunge wetu watukufu tunawaomba fikirini kuongeza uzito ili mkopo huo usitoke.Nchi yetu ni tajiri kwa nini tunahangaika na mikopo itakayokuja kutuumiza baadaye.Kama nyie mmejitosheleza sawa.lakini mnapita vijijini na mnaona hali halisi ya umaskini mkubwa uliopo.

Chonde chonde hii fedha tunayolia nayo ni ndogo sana.Pambaneni zile 1.5 na nyingine nyiiiingi tu zipatikane nikianza kuorodhesha hapatatosha.Zinatosha kabisa hiyo elimu mnayotaka.

Zitto ni wetu sisi wanyonge na tunamkubali sana.Mwacheni na nyie mtutetee.
 
Spika Job Ndugai amesema wanamsubiri Mbunge Zitto Kabwe awaeleze kwanini aliandika barua kwa Benki ya Dunia kuzuia mkopo kwa ajili ya elimu nchini.

My take huyu jamaa anayejiita Zitto sisi wananchi wa Kigoma tutamuadhibu kwenye sanduku la kura.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wa Kigoma tunakaaga kimya tukisubiri wakati..usituzungumzie..wewe hutoki kigoma..ulabheha
 
Wewe kama mtumishi wa taasisi unaweza kutumia nendo ya taasisi yako kufikisha ujumbe kwenye taasisi nyingine bila ruhusa ya ofisi yako?
Mtumishi wa taasisi kwa kevel gani?

CEO ni mtumishi wa taasisi na yeye ndiye anatoa ruhusa ya nembo kutumiwa.

Mbunge ana a very unique mandate by virtue if being elected by the people.

Mnataka wabunge waombe ruhusa kuandika barua yenye ketterhead ya bunge?

Nimeuliza seali hapo juu. Ikiwa Mbunge anaandika barua World Bank, kuomba habari za kumchunguza Spika kama anatumia hela za World Bank kinyume na malengo rasmi, unataka mbunge huyo aomne ruhusa kutumia ketterhead ya bunge?

Mpaka sasa sijajibiwa. Mnasoma na kuliacha tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
#Habari:Bunge limemwagiza mwanasheria mkuu wa serikali kuangalia kama kuna viashiria vya makosa ya jinai kwa mbunge wa jimbo la kigoma mjini Mhe.Zitto Kabwe kutumia nembo ya bunge kuandika barua benki ya dunia ili isitishe mkopo kwa ajili ya kuendeleza sekta ya elimu nchini.
FB_IMG_1580473888689.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lazima Bunge limuazimie.
Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai amesema kama kulikuwa na tatizo la kisera, ni mambo ya kujadiliwa bungeni. Sio mara ya kwanza kutokea sera zikawa na udhaifu au zinahitaji maboresho.

Anasema Zitto alipaswa awasilishe maoni yake na mapendekezo kuhusu ubovu wa sera ya elimu kisha litazamwe. Ndio kazi za bunge. Sasa yeye anaenda kupiga kelele nje ya nchi kwa sababu hakubaliani na sera kweli?

Awajibishwe.

=========
Leo Ijumaa Januari 31, 2020 bungeni jijini Dodoma, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema wanamsubiri Zitto awaeleze kwa nini aliandika barua hiyo.

“Mtu unaweza kuwa na tofauti na sera au mtazamo kati ya wewe mbunge au upande wa Serikali na kadhalika, lakini kufikia mahali pa ‘kublock’ Tanzania isipate fursa fulani nadhani ni kwenda mbali mno.”

“Kwa sababu watoto watakaokosa fursa hiyo ni watoto wa Tanzania ni walimu wa Tanzania ni miundombinu ya elimu ya Tanzania, sijui katika hilo kama mbunge unanufaika nini maana kama ni suala la utofauti la kisera haya ni mambo ya kujadiliana tu,” amesema Spika Ndugai.

Katika kusisitiza hilo, Spika Ndugai amesema, “ningependa kutoa ushauri wa ujumla tu kwamba ni vema kutumia fursa yetu kama wawakilishi wa wananchi tukaelimishana tukaelezana kuliko kuwakosesha Watanzania fursa wakati baadhi yetu watoto wetu wapo Feza Boys, wapo Marian Girls halafu unablock msaada kwa watoto walio wengi wa wapiga kura wetu jambo ambalo halifai kabisa.”

Hata hivyo hapo jana Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Joseph Kakunda alisema kitendo cha Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kuandika barua ya kutaka kuzuia mkopo wa elimu unaotolewa na Benki ya Dunia (WB) ni kituko nani aibu.

Kakunda aliyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia taarifa za kamati za Bunge za bajeti na Uwekezaji na Mitaji ya Umma.

“Naomba nizungumze masikitiko yangu dhidi ya barua moja ambayo mwenzetu mmoja (Zitto) ameiandika kutaka kuzuia fedha za miradi ya elimu ni kituko na ni aibu sana kwetu sisi wabunge kuona mwenzetu ameandika barua,” alisema Kakunda ambaye pia ni Mbunge wa Sikonge (CCM) mkoani Tabora

Alisema barua hiyo wangekuwa wameandika watu wa mashirika yasiyo ya kiserikali yeye asingestuka sana lakini kuandikwa na mbunge mwenzao wakati Serikali imepeleka Sh1 bilioni kwa ajili ya kukarabati Sekondari ya Kigoma iliyoko kwenye jimbo lake ni jambo la kusikitisha.

“Sasa hivi Sekondari ya Kigoma ni kama mpya. Na vilevile Serikali imepeleka zaidi ya Sh4 bilioni kwa ajili ya kuboresha elimu. Sasa anazuia zisije kwa haraka kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa kitanzania nieleze masikitiko makubwa sana,”amesema.

“Nilitamani nipaze sauti huko aliko anisikie lakini kwa sababu yuko mbali naachia hapo lakini atasikia kutoka kwenye Hansard (kumbukumbu Rasmi za Bunge)" alisema Mh. Kakunda

Huyo Ndugai anadhani kwamba hatujui kwamba hilo bunge hakuna jambo lolote la wapinzani linafanyiwa kazi? Tume huru ya uchaguzi ndio kilio cha wapinzani, mbona hawako tayari ijadiliwe huko bungeni? Ni hivi, Zito atoe mashitaka awezavyo huko nje maana huku ndani hayo mambo hayawezi kujadiliwa.
 
#Habari:Bunge limemwagiza mwanasheria mkuu wa serikali kuangalia kama kuna viashiria vya makosa ya jinai kwa mbunge wa jimbo la kigoma mjini Mhe.Zitto Kabwe kutumia nembo ya bunge kuandika barua benki ya dunia ili isitishe mkopo kwa ajili ya kuendeleza sekta ya elimu nchini.View attachment 1342135

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo ******* anateseka na mengi,ukiachia Zitto kuna kale kaugonjwa hatarishi pia kanamtesa!
 
Kazi za mbunge zimeanishwa wazi kabisa hiyo ya kuwasiliana na benki ya dunia kwa kutumia Ofisi ya bunge na karatasi yenye nembo ya bunge haimo kwenye kazi za mbunge.
Hivyo ndiyo ilivyokuwa?
 
hata trump mgomvi sana lakini kwenye swala la kiutaifa huezi skia wapinzani wamefanya jambo kama hili kwa kwel upinzani mjitathmini sana haswa wabunge wenu! Duniani kote kuna upinzani kuanzia kwenye dini mpaka maisha ya kawaida lakini chakula kikilimwa na mkulima wote tunakula, mengi yataongewa kuhusu upande wa spika lakini ameongea point yenye maaana sana

Huko US mifumo yao ina nguvu, utafananisha na hapa kwetu sheria na katiba ya nchi inatekelezwa kwa mapenzi ya rais? Namtaka Zito asipate woga wowote bali aseme uhayawani wowote unaoendelea hapa nchini, wananchi wengi hatupendi kuburuzwa na ccm hivyo tutamuunga mkono kwenda nje kusaka msaada wa kutoburuzwa na shetani.
 
Huko US mifumo yao ina nguvu, utafananisha na hapa kwetu sheria na katiba ya nchi inatekelezwa kwa mapenzi ya rais? Namtaka Zito asipate woga wowote bali aseme uhayawani wowote unaoendelea hapa nchini, wananchi wengi hatupendi kuburuzwa na ccm hivyo tutamuunga mkono kwenda nje kusaka msaada wa kutoburuzwa na shetani.

sio mifumo, tatizo hoja zenye mashiko! wapinzania wanakuaga na hoja zenye akili sana nimetoa mfano wa jamaa aliesema matajri walipishwe kodi ya kusaidia maskini , ona hoja kama izo: sasa nyie hata ilani ya chama hatuwelewi, inafika mpaka hatua mnachukua mgombea wa ccm mnamuweka mwakilishi wenu, sasa hio ni akili? upinzani mm naona mrudi tu shule kwanza unampinga mtu aliekupa mtu wa kugombea , what type of mind is this
 
Back
Top Bottom