Zitto Kabwe asubiriwa na Bunge kueleza lengo la barua yake Benki ya Dunia kuzuia mkopo wa kuboresha Elimu (SEQUIP)

Zitto Kabwe asubiriwa na Bunge kueleza lengo la barua yake Benki ya Dunia kuzuia mkopo wa kuboresha Elimu (SEQUIP)

Bunge liazimie Zitto azuiwe Vikao vya Bunge mpaka 2025, kwa maana hata akishinda Uchaguzi ujao abaki kwenye kifungo

Sent using Jamii Forums mobile app

Tunataka nchi za ulaya na Amerika zichukue hatua kali dhidi ya huu utawala unaokandamiza mitazamo mbadala. Bunge gani hilo la kumtishia mtu, hilo bunge la kuburuzwa na rais ndio lakumtisha mtu? Wale wanaosaka maisha ndio watatemekea hilo bunge kibogoyo.
 
Tunataka nchi za ulaya na Amerika zichukue hatua kali dhidi ya huu utawala unaokandamiza mitazamo mbadala.
Mkuu hii ni nchi huru inayojiamulia mambo yake. Kama tumeamua watoto wanaopata ujauzito wasome kwa njia mbadala, itakuwa hivyo. Ndio demokrasia.
 
stakehigh,
Huyu mgombea aliyetoka CCM hao wapinzani walipewa na CCM au alitumia pesa yake kwenda kusaka madaraka? Huko ccm aliondoka baada ya kunyimwa nafasi na wala hakutolewa ofa, hao viongozi wa upinzani kwa tamaa yao ya pesa wakachukua pesa yake wakampa nafasi.

Hiyo CCM unayoisifia kuwa ina sera, sio ndio hao mwishoni mwaka awamu iliyopita walikuwa wanatuimbisha uchumi wa gas, leo kaja rais mwingine haongelei uchumi wa gas bali umeme wa maji!? Hapo kuna jipya gani kama sio wale wale kasoro tarehe?
 
Mkuu hii ni nchi huru inayojiamulia mambo yake. Hao unaodhani watasaidia ni watu wanaotazama maslahi yao tu. Kama yanawaendea vizuri hawatajali shida zako.

Huu mkopo utatolewa na hakuna chochote kinaweza kuzuia. Walileta mikwara kwenye sheria ya takwimu, kiko wapi?

Bila shaka hujui dunia inaendaje!

Mkopo utakuja baada ya kutii masharti. Sheria ya takwimu nayo isipobadilishwa siku mkienda kutaka mkopo mwenendo utakuwa ni huo huo. Na hatua zikichukuliwa dhidi ya sheria kandamizi tutawaunga mkono. Kujiamulia mambo yako, sio kutumia madaraka ya urais kunajisi chaguzi za nchi.
 
Huyu mgombea aliyetoka ccm hao wapinzani walipewa na ccm au alitumia pesa yake kwenda kusaka madaraka? Huko ccm aliondoka baada ya kunyimwa nafasi na wala hakutolewa ofa, hao viongozi wa upinzani kwa tamaa yao ya pesa wakachukua pesa yake wakampa nafasi. Hiyo ccm unayoisifia kuwa ina sera, sio ndio hao mwishoni mwaka awamu iliyopita walikuwa wanatuimbisha uchumi wa gas, leo kaja rais mwingine haongelei uchumi wa gas bali umeme wa maji!? Hapo kuna jipya gani kama sio wale wale kasoro tarehe?

sasa shida iko wap apo? si bora useme kitu ambacho kipo within your limits za akili waje watu wakukosea kuliko ufanye upuuzi ambao hata kukosoa ni kituko, ni mara 1000 ccm waendelee kushika madaraka mpaka pale kitakapokuja chama ambacho kinaweza kubypass weakness za ccm!
 
Hicho chama kinachoweza kubypass weakness za ccm kinangoja nini kisianze sasa? Kama ni ccm kutoka madarakani walipaswa wasiwepo maana huwa wananyimwa kura sana, lakini kwa kuwa wanaudhibiti wa dola wanachezea chaguzi za nchi. Machafuko peke yake ndio yatawatoa. Na hilo litawezekana kwa msaada wa hayo mataifa ya nje.
 
Mkopo utakuja baada ya kutii masharti. Sheria ya takwimu nayo isipobadilishwa siku mkienda kutaka mkopo mwenendo utakuwa ni huo huo. Na hatua zikichukuliwa dhidi ya sheria kandamizi tutawaunga mkono. Kujiamulia mambo yako, sio kutumia madaraka ya urais kunajisi chaguzi za nchi.

Sheria ya takwimu pamoja na madhaifu yake, haikutosha kuzuia mkopo wa awali licha ya mikwara mingi. Mkopo sio msaada, wao wanahitaji pia kukopesha kwa maslahi yao.

Siungi mkono ukandamizaji wa aina yoyote, lakini njia zinazotumika kupindua meza kwa namna hii zina gharama kubwa mno.

Sitazishiriki.
 
Hicho chama kinachoweza kubypass weakness za ccm kinangoja nini kisianze sasa? Kama ni ccm kutoka madarakani walipaswa wasiwepo maana huwa wananyimwa kura sana, lakini kwa kuwa wanaudhibiti wa dola wanachezea chaguzi za nchi. Machafuko peke yake ndio yatawatoa. Na hilo litawezekana kwa msaada wa hayo mataifa ya nje.

aliekwambia wananyimwa kura ni nan? ccm has roots nzito sio kama upinzani! wewe unasubiria kura za watu wa mjini,? ccm hata kama ukiwa na agenda kwamba wanaibaga kura kwenye uwanja wa actions still ccm ina mapungufu yake lakini hawajawahi vuka mpaka wa ukichaa kama upinzani, na kila mtu anajua kabisa ccm wana mapungufu ndio lakini unaweza fananisha na hao upinzani? upinzani hawana mapungufu yaani hawana akili ndo jina zuri linalowafaa
 
Kuna kitu kinaenda kutokea kwa Zito kati ya aya:
1. Kufukuzwa ubunge
2.Chama chake kufutwa
3.kwenda Jela kwa kutumia nembo ya bunge kwa taarifa binafsi

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nyundo ya zitto imetua kwenye utosi wa ccm.....ccm sio wa kucheka nao hata kidogo
 
Kuna kitu kinaenda kutokea kwa Zito kati ya aya:
1. Kufukuzwa ubunge
2.Chama chake kufutwa
3.kwenda Jela kwa kutumia nembo ya bunge kwa taarifa binafsi

Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu hujui historia ya siasa za Tanzania, Zitto angekuwa mwepesi wasingemkawiza, hata ukiangalia body language ya Ndugai unaona kabisa Zitto ni mzito, sio Ndugai yule anayeongeaga kwa mikogo na kujimbafai.. leo ametulia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi ni muhimu zaidi, Taifa ni tunu kila mtu anajivunia nchi yake, anatambulika kwa nchi yake, ni kama mzazi, baba au mama hata angekuwa na kasoro au vilema vingapi bado atakuwa baba au mama.
CCM wanafanya makosa wakati mwingine na watawala kwamba ukisisia kauli zao utadhani Ccm tu ndio wanaunda taifa, hapana kila alive wa Tanzania kwa mujibu wa sheria zetu ni mwananchi, anao utaifa ndani mwake na hapo ndipo inakuja hoja ya maridhiano, mazungumzo wote ni baba moja
Viongozi wasione wale wanaowapinga kwa hasira ni ndugu zao.
Nimuombe Raid wetu na viongozi wote ngazi zote wajue haya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Raisi wetu ndiyo kazuia mkopo ikiwa serikali ilijipanga sawa sawa ikiwa na wasomi na weledi katika kuomba mikopo kwa mabeberu inawezaje kushindwa na mtu 1 tu Zito kabwe

Hivyo maombi ya serikali yalikuwa na mapungufu mengi tena ya wazi ndiyo Zito kaweza kuwapiku nani mkosaji?

Ina maana Ndugai uelewi? Au ndo ule usemi wa kila watanzania wanne mmoja ni kichaa yaan namaanisha nikihesabu kuanzia kwa MSEKWA, SITTA, MAKINDA, ALAFU WEWE? oooo nimekumbuka unatoka Dodoma, wasalimie Milembe Hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria ya takwimu pamoja na madhaifu yake, haikutosha kuzuia mkopo wa awali licha ya mikwara mingi. Mkopo sio msaada, wao wanahitaji pia kukopesha kwa maslahi yao.

Siungi mkono ukandamizaji wa aina yoyote, lakini njia zinazotumika kupindua meza kwa namna hii zina gharama kubwa mno.

Sitazishiriki.

Hakuna anayetaka ushiriki, onyesho uzi wowote uliowahi kukemea ukandamizaji ili tujue huungi mkono ukandamizaji. Hiyo mbinu aliyotumia Zito ni sahihi, maana hakuna nafasi yoyote ya kupinga hizo tabia huku ndani ukiwa mpinzani na ukasikilizwa. Kama uwanja wa kupinga hayo mambo ya ukandamizaji hayana nafasi humu ndani, hiyo njia ya Zito ndio njia sahihi na tunamuunnga mkono.

Hivi juzi uchaguzi umechezewa, ni wapi ww umewahi kuonyesha kwamba jambo lile sio sawa? Namtaka Zito huko alipo atoe na ushahidi mbalimbali wa ukandamizaji unaoendelea hapa nchini, kwa watawala kushirikiana na vyombo vya dola na taasisi nyingine za kimamlaka.
 
Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai amesema kama kulikuwa na tatizo la kisera, ni mambo ya kujadiliwa bungeni. Sio mara ya kwanza kutokea sera zikawa na udhaifu au zinahitaji maboresho.

Anasema Zitto alipaswa awasilishe maoni yake na mapendekezo kuhusu ubovu wa sera ya elimu kisha litazamwe. Ndio kazi za bunge. Sasa yeye anaenda kupiga kelele nje ya nchi kwa sababu hakubaliani na sera kweli?

Awajibishwe.

=========
Leo Ijumaa Januari 31, 2020 bungeni jijini Dodoma, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema wanamsubiri Zitto awaeleze kwa nini aliandika barua hiyo.

“Mtu unaweza kuwa na tofauti na sera au mtazamo kati ya wewe mbunge au upande wa Serikali na kadhalika, lakini kufikia mahali pa ‘kublock’ Tanzania isipate fursa fulani nadhani ni kwenda mbali mno.”

“Kwa sababu watoto watakaokosa fursa hiyo ni watoto wa Tanzania ni walimu wa Tanzania ni miundombinu ya elimu ya Tanzania, sijui katika hilo kama mbunge unanufaika nini maana kama ni suala la utofauti la kisera haya ni mambo ya kujadiliana tu,” amesema Spika Ndugai.

Katika kusisitiza hilo, Spika Ndugai amesema, “ningependa kutoa ushauri wa ujumla tu kwamba ni vema kutumia fursa yetu kama wawakilishi wa wananchi tukaelimishana tukaelezana kuliko kuwakosesha Watanzania fursa wakati baadhi yetu watoto wetu wapo Feza Boys, wapo Marian Girls halafu unablock msaada kwa watoto walio wengi wa wapiga kura wetu jambo ambalo halifai kabisa.”

Hata hivyo hapo jana Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Joseph Kakunda alisema kitendo cha Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kuandika barua ya kutaka kuzuia mkopo wa elimu unaotolewa na Benki ya Dunia (WB) ni kituko nani aibu.

Kakunda aliyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia taarifa za kamati za Bunge za bajeti na Uwekezaji na Mitaji ya Umma.

“Naomba nizungumze masikitiko yangu dhidi ya barua moja ambayo mwenzetu mmoja (Zitto) ameiandika kutaka kuzuia fedha za miradi ya elimu ni kituko na ni aibu sana kwetu sisi wabunge kuona mwenzetu ameandika barua,” alisema Kakunda ambaye pia ni Mbunge wa Sikonge (CCM) mkoani Tabora

Alisema barua hiyo wangekuwa wameandika watu wa mashirika yasiyo ya kiserikali yeye asingestuka sana lakini kuandikwa na mbunge mwenzao wakati Serikali imepeleka Sh1 bilioni kwa ajili ya kukarabati Sekondari ya Kigoma iliyoko kwenye jimbo lake ni jambo la kusikitisha.

“Sasa hivi Sekondari ya Kigoma ni kama mpya. Na vilevile Serikali imepeleka zaidi ya Sh4 bilioni kwa ajili ya kuboresha elimu. Sasa anazuia zisije kwa haraka kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa kitanzania nieleze masikitiko makubwa sana,”amesema.

“Nilitamani nipaze sauti huko aliko anisikie lakini kwa sababu yuko mbali naachia hapo lakini atasikia kutoka kwenye Hansard (kumbukumbu Rasmi za Bunge)" alisema Mh. Kakunda

Hiyo Bluetooth spika haina ubavu huo.
 
Hakuna anayetaka ushiriki, onyesho uzi wowote uliowahi kukemea ukandamizaji ili tujue huungi mkono ukandamizaji. Hiyo mbinu aliyotumia Zito ni sahihi, maana hakuna nafasi yoyote ya kupinga hizo tabia huku ndani ukiwa mpinzani na ukasikilizwa. Kama uwanja wa kupinga hayo mambo ya ukandamizaji hayana nafasi humu ndani, hiyo njia ya Zito ndio njia sahihi na tunamuunnga mkono.

Hivi juzi uchaguzi umechezewa, ni wapi ww umewahi kuonyesha kwamba jambo lile sio sawa? Namtaka Zito huko alipo atoe na ushahidi mbalimbali wa ukandamizaji unaoendelea hapa nchini, kwa watawala kushirikiana na vyombo vya dola na taasisi nyingine za kimamlaka.

Soma threads zangu za nyuma. Sisimamii upande mmoja. Nasimamia ninachoona ni sahihi na sio lazima nitolee tamko kila kitu kwa uzuri au ubaya wake. Sio lazima.

Kuhusu haki na ukandamizwaji ni same old cry tangu dunia iumbwe. Malalamiko hayajawahi kuisha na hayataisha.

Isitoshe, huu ukandamizaji unaotajwa siku hizi umeegemea zaidi kwa wanasiasa na wanaharakati. Huko uchafu ni mwingi so mnajuana. Msiwagharimu wasiohusika kwenye maslahi yenu.

Sitashiriki.
 
aliekwambia wananyimwa kura ni nan? ccm has roots nzito sio kama upinzani! wewe unasubiria kura za watu wa mjini,? ccm hata kama ukiwa na agenda kwamba wanaibaga kura kwenye uwanja wa actions still ccm ina mapungufu yake lakini hawajawahi vuka mpaka wa ukichaa kama upinzani, na kila mtu anajua kabisa ccm wana mapungufu ndio lakini unaweza fananisha na hao upinzani? upinzani hawana mapungufu yaani hawana akili ndo jina zuri linalowafaa

Ukisikia kunyimwa kura unadhani ni lazima ukose hata kura moja? Kura za watu wa mjini sio kura? au kura za watu wa mjini zina thamani nusu? Zamani ndio kulikuwa na hiyo Hadaa eti ccm wanashinda vijijini ila sio sasa. Wanachokifanya ccm kwenye chaguzi kiko wazi usidhani hatuoni uhayawani wao. Wapinzani hawataki upendeleo wowote bali wanataka mshindi halali. Nipe tofauti ya upinzani kisha weka ubora wa ccm ili nione kweli kuna tofauti ya kuwafanya ccm washinde kwa 100%. Tunataka tume huru ya uchaguzi, hizi nyingine zote ni mbwembwe tu, wananchi ndio wataamua wanamtaka nani na sio rais anamtaka nani awe kiongozi.
 
Back
Top Bottom