Swala ninalojadili mimi hapa ni NAMNA ALIVYOANDIKA BARUA, na si KWA NINI AMEANDIKA BARUA. Ameandika barua ikiwa na maudhui ya chama cha ACT, lakini akasingizia kuwa ni ya Bunge la JMT, kwa sababu ametumia HEADED PAPER ya Bunge, na akaisaini barua hiyo kama Mbunge wa Bunge la JMT. Hii kesi Zitto akichomoa, nitajua kuna watu wana bahati Duniani.
Kuna mtu mwingine huko nyuma aliwahi kupata kesi inayofanana na hii, anaitwa Leo Lwekamwa. Yeye alikanyaga Katiba ya JMT kwa hasira, halafu akazua kesi moja ilijulikana kwa jina maarufu kama KESI YA KUSIGINA KATIBA. Huyu bwana mpaka ilifikia hatua akawa anatoa utetezi mahakamani kuwa hakuikanyaga Katiba ila ilidondokea miguuni kwake kwa bahati mbaya wakati anaongea. Nina wasiwasi hata Zitto naye anaweza akaja na utetezi kuwa hakuandika barua WB ila ilichapishwa barua feki kwenye mitandao ya jamii ikiwa inaonyesha kuwa ameiandika yeye. Hapa hachomoki, hata iweje, mtakuja kuniambia. Kwanza anapoteza ubunge ikiwa ni pamoja na ban ya kugombea ubunge tena, halafu yule Kamishna Jenerali mpya alyeapishwa juzi naye kuna uwezekano akamhost kwa kipindi kisichopungua miaka kadhaa. Acha wafanye makosa ili wawe wanajifunza