Zitto Kabwe aunga Mkono Serikali 3 baada ya Hotuba ya Jaji Warioba Dodoma

Kamanda Francis

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2013
Posts
834
Reaction score
140
Zitto ameonekana Kufurahishwa na ufafanuzi wa Jaji Warioba na hata Kupelekea kuwashawishi Wajumbe wenzake kwamba, hawana budi kujadili namna ya Kuuboresha zaidi muundo huo wa Serikali tatu badala ya kujadili Serikali mbili ambazo yeye mwenyewe amekiri kwamba hazitakuwa Suluhisho la Kero za muungano kupitia ukurasa wake wa facebook.

Hii imemtokea baada ya jana Kuusikiliza kwa makini ufafanuzi wa Jaji Warioba kuhusu muundo huo wa Serikali tatu, pia Kwa mujibu wa Maelezo ya Julius S. Mtatiro Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge maalum la Katiba amesema Idadi kubwa ya Wajumbe wa CCM, jana baada ya kutoka ndani Ukumbi wa Bunge, walionekana kuridhishwa na ufafanuzi wa hotuba ya Warioba huku wengine wakitamka wazi kuwa Serikali tatu ndio mpango mzima.

Nawasilisha!

Chanzo: Zitto Kabwe's facebook page....
 
huo ni mtazamo wake, hakuna nchi duniani yenye serikali tatu, labda sisi tuwe wa kwanza..3 hazina tija yoyote kufurahishana wakati tunaingia hasara, siungi mkono, suluhisho ni serikali moja tu
 
Punguza VIROBA na GONGO Mkuu
 
Jana kuna uzi uliletwa hapa kua Zitto na January Makamba wamempinga mzee Warioba kupitia tweets zao. Sasa tuelewe lipi hapa.!!!????!!?
 
huo ni mtazamo wake, hakuna nchi duniani yenye serikali tatu, labda sisi tuwe wa kwanza..3 hazina tija yoyote kufurahishana wakati tunaingia hasara, siungi mkono, suluhisho ni serikali moja tu

upende usipende serikali tatu ni mpango wa sasa
 
Kumbe watanzania wengi ni wavivu wa kufikili yaani kwa kero hz tuu ambazo zinazungumzika leo tunakata tamaa na kuona mfumo uliopo wa serikali ndio tatizo? Nadilikikusema tumepotea na hoja hii inapaswa kupingwa kwa nguvu zote, hv hii tume inajuwa afya ya serikali tatu na mbili ipi bora? Au wamekurupuka tuu?.
 
huo ni mtazamo wake, hakuna nchi duniani yenye serikali tatu, labda sisi tuwe wa kwanza..3 hazina tija yoyote kufurahishana wakati tunaingia hasara, siungi mkono, suluhisho ni serikali moja tu

ila ushaona nchi moja serikali mbili? hivi visiwa vya komoro vina serikali ngapi acha uzoba
 
Hi inapokuwa Serikali tatu, kila nchi na Rais wake mwenye Mamlaka kamili, huyo Rais wa Muungano atakuwa hana maana ya kuwepo, labda kama hawa Marais wawili watakuwa Magavana au Mawaziri Wakuu.
 
huo ni mtazamo wake, hakuna nchi duniani yenye serikali tatu, labda sisi tuwe wa kwanza..3 hazina tija yoyote kufurahishana wakati tunaingia hasara, siungi mkono, suluhisho ni serikali moja tu

Tukisema serikali moja, na Zanzibar pendwa tunaifanyaje? Je, kwa maoni yao wanaridhia hii? Manake naona kama msuguano uko zaidi kipande hicho. Labda kama tuende kidikteta kuwa maamuzi ni hayo...watake, wasitake.
 
Kumbe watanzania wengi ni wavivu wa kufikili yaani kwa kero hz tuu ambazo zinazungumzika leo tunakata tamaa na kuona mfumo uliopo wa serikali ndio tatizo? Nadilikikusema tumepotea na hoja hii inapaswa kupingwa kwa nguvu zote, hv hii tume inajuwa afya ya serikali tatu na mbili ipi bora? Au wamekurupuka tuu?.

Tume imetoa maoni ya Watanzania.
 
Kumbe watanzania wengi ni wavivu wa kufikili yaani kwa kero hz tuu ambazo zinazungumzika leo tunakata tamaa na kuona mfumo uliopo wa serikali ndio tatizo? Nadilikikusema tumepotea na hoja hii inapaswa kupingwa kwa nguvu zote, hv hii tume inajuwa afya ya serikali tatu na mbili ipi bora? Au wamekurupuka tuu?.

Mkuu ni vizuri ukajipa nafasi akilini mwako kusikia wanayosema wengine badala ya kuwa na msimamo wa "labda nife ndo nitakubali" kwa ninavyoelewa ni kwamba Tume ni mchambuzi na anapendekeza kutokana na uchambuzi huo. Kusema wamekurupuka ni kuwakosea adabu. Kama wewe huoni umuhimu wa kukifanyia kazi walichokipendekeza si uje na hoja zako ili na wengine tujue kwa nini hutaki yaliyopendekezwa? Hivi tukianza kila mtu asipokubaliana na kile kinachosemwa na mwingine kukebehi kwamba amekurupuka tutafika kweli? chukulia mfano; iwe Rais ametangaza Baraza la Mawaziri halafu mtu asiyekubaliana naye aseme Mhe. Rais amekurupuka na kuishia hapo bila kutoa sababu si mtu huyo ataonekana ni mufilisi! Kwa upande wangu yeyote atakayekuja na hoja ya kunishawishi yenye maana kwa mimi ni watoto na wajukuu wangu nitaunga mkono lakini si kuja na lugha za kebehi namna hii.
 
Kumbe watanzania wengi ni wavivu wa kufikili yaani kwa kero hz tuu ambazo zinazungumzika leo tunakata tamaa na kuona mfumo uliopo wa serikali ndio tatizo? Nadilikikusema tumepotea na hoja hii inapaswa kupingwa kwa nguvu zote, hv hii tume inajuwa afya ya serikali tatu na mbili ipi bora? Au wamekurupuka tuu?.

Kijana wangu wewe ndiye mkurupukaji! Na mvivu wa kufikiri.aliyekutuma nani? Huna mamlaka yoyote ya kisheria kuipinga serikali 3 maana ni maoni ya wananchi moja kwa moja ambao ndo wanamuweka Rais madarakani.
Zitto kasema ukweli unafiki kwake ni mwiko.
 
Back
Top Bottom