Zitto Kabwe aunga Mkono Serikali 3 baada ya Hotuba ya Jaji Warioba Dodoma

Zitto Kabwe aunga Mkono Serikali 3 baada ya Hotuba ya Jaji Warioba Dodoma

Aliepost alikuwa nalakwake jambo au alitumwa na cdm ili apotoshe umma wa muone zt hafai nawambia petro post yako imefeli na waliekutuma kawambie mtu huyo achafuliki .
 
huo ni mtazamo wake, hakuna nchi duniani yenye serikali tatu, labda sisi tuwe wa kwanza..3 hazina tija yoyote kufurahishana wakati tunaingia hasara, siungi mkono, suluhisho ni serikali moja tu
Wabongo kwa ku copy, sasa kwa kuwa hakuna na nyie hamuwezi, je muungano wa nchi mbili ukafom nchi mbili umeuona wapi?
 
Wabongo kwa ku copy, sasa kwa kuwa hakuna na nyie hamuwezi, je muungano wa nchi mbili ukafom nchi mbili umeuona wapi?

wewe usiyecopy niambie hiyo nchi yenye serikali tatu ni ipi??
 
Mimi siungi mkono serikali tatu, ni gharama na mzigo zaidi kwa watanzania.
 
ZZK siku hizi mbona JF anaikimbia sana?? Njoo huku uje useme mwenyewe maana kule FB watu wanaweza hijack ID yako mkuu!!! JF iko protected!!! Ha ha ha ha!!! Naamini atakuwa alisoma makonde ya jana JF kuhusu yeye na January makamba basi ikabidi aanze kivingine tena FB.
 
... Idadi kubwa ya Wajumbe wa CCM, jana baada ya kutoka ndani Ukumbi wa Bunge, walionekana kuridhishwa na ufafanuzi wa hotuba ya Warioba huku wengine wakitamka wazi kuwa Serikali tatu ndio mpango mzima...
Hao wajumbe wa CCM ni wa kupelekwapelekwa tu, akija JK akasema serikali mbili, watarudi tena kule kule! Ni sawa na wale wapiga kura kwenye wimbo wa 'Ndio Mzee' wa Profesa Jay, walimkubali mgombea wa mwanzo, akaja mwingine akawapa sera za kumpinga wa mwanzo, naye wakamkubali!!
 
Hi inapokuwa Serikali tatu, kila nchi na Rais wake mwenye Mamlaka kamili, huyo Rais wa Muungano atakuwa hana maana ya kuwepo, labda kama hawa Marais wawili watakuwa Magavana au Mawaziri Wakuu.

Serikali 3! Ama suala la muundo wa kiutawala uweje, hiyo ndo inapaswa iwe kazi ya Bunge Maalum la Katiba kuboresha yale maoni ya Wananchi!
 
mpaka sasa zanzibar sio nchi mkuu, tuna tanzania pekee
Kama Katiba yao inasema Zanzibar ni nchi na ina Rais wake, bendera yake, wimbo wake wa Taifa, kwanini usiamini kuwa ni nchi!
 
wewe usiyecopy niambie hiyo nchi yenye serikali tatu ni ipi??
hakuna ndo maana tunataka sisi tuwe wa kwanza na hao waje wacopy kwetu, wabongo mnaogopa kuwa wa kwanza, mnatafuta reference na nyinyi ndo mfuate.
 
Mimi siungi mkono serikali tatu, ni gharama na mzigo zaidi kwa watanzania.
alafu mkiulizwa mseme hizo gharama ni zipi mnakimbia, swala hapa ni kuzuia matumizi ya sio na lazima na matumizi mabaya ya fedha za uma jambo ambalo serikali ya ccm imeshindwa kabisa
 
serikali tatu za kwenye vitabu za kusoma sawa hapa ni serikali moja tu hakuna jinsi kama ule mkoa wa kule visiwani unataka au hautaki msimamo ndo huo hawawezi kutuumiza vichwa
 
huo ni mtazamo wake, hakuna nchi duniani yenye serikali tatu, labda sisi tuwe wa kwanza..3 hazina tija yoyote kufurahishana wakati tunaingia hasara, siungi mkono, suluhisho ni serikali moja tu

Muungano wa serikali 2 kwa miaka hamsini imeshindwa kuondoa kero. Mchakato wa kuelekea serikali moja ambao ilikuwa uanze mara tu ya Muungano miaka hamsini iliyopita, hata agenda haijawekwa mezani. Bado wengine wanaamini kitu ambacho kwa uchambuzi wa kina muungano wa serikali moja haiwezekani. Ni heri tujaribu serikali tatu. Na hii ikishindikana basi tutengane kimoja na tubaki na ujirani mwema. Tugange linalowezekana sio nadharia.
 
Kumbe watanzania wengi ni wavivu wa kufikili yaani kwa kero hz tuu ambazo zinazungumzika leo tunakata tamaa na kuona mfumo uliopo wa serikali ndio tatizo? Nadilikikusema tumepotea na hoja hii inapaswa kupingwa kwa nguvu zote, hv hii tume inajuwa afya ya serikali tatu na mbili ipi bora? Au wamekurupuka tuu?.

Kero zipi unazosema zinazungumzika? Kwani wakati muungano umeundwa 1964 Zanzibar ilibaki kuwa nchi kama ilivyo sasa? Kama huwezi kutafakari nenda katafute hotuba ya warioba ya jana nawe usome labda utaambulia kitu then urudi hapa jukwaani. Tabia ya kukaa baa unapiga kilauli then unaingia JF inakuvua nguo bure.
 
huo ni mtazamo wake, hakuna nchi duniani yenye serikali tatu, labda sisi tuwe wa kwanza..3 hazina tija yoyote kufurahishana wakati tunaingia hasara, siungi mkono, suluhisho ni serikali moja tu

Tanzania ni Nchi inayojitegemea kutokana na aina wa Muungano wetu, hatuna haja ya kuiga hiyo miundo mingine ya "nchi nyingine duniani"
 
huo ni mtazamo wake, hakuna nchi duniani yenye serikali tatu, labda sisi tuwe wa kwanza..3 hazina tija yoyote kufurahishana wakati tunaingia hasara, siungi mkono, suluhisho ni serikali moja tu

Kumbuka pia hakuna nchi duniani yenye mfumo wa serekali mbili kama huu wetu, ni ajabu sana kwenye muungano wa serekali mbili yani tanganyika na zanzibar alafu tanganyika haipo ipo Zanzibar na muungano, yani rais wa muungano ndo anaiongoza tanganyika moja kwa moja ila haiongozi Zanzibar moja kwa moja, hii inamaanisha ata rais wa muungano akitoka nchi Ya zanzi anaiongoza tanganyika ila mtanganyika haruusiwi kwenda kutawala Zanzibar,
 
Kama Katiba yao inasema Zanzibar ni nchi na ina Rais wake, bendera yake, wimbo wake wa Taifa, kwanini usiamini kuwa ni nchi!

katiba ya Jamhuri ya MUUNGANO WA TANZANIA, haijasema hivyo, hivyo amendment hiyo ni BATILI ON THE EYES OF THE CONSTITUTION OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, 1977.
 
Back
Top Bottom