Zitto Kabwe aunga Mkono Serikali 3 baada ya Hotuba ya Jaji Warioba Dodoma

Tanzania ni Nchi inayojitegemea kutokana na aina wa Muungano wetu, hatuna haja ya kuiga hiyo miundo mingine ya "nchi nyingine duniani"

muundo wa serikali 3 haufai, ni kujiongezea gharama kwa kutaka kujifurahisha, furaha ambayo haitadumu, hapa tunaanza safari ya kuua muungano, warioba pia amekiri challenge kubwa ni gharama, kwanini kuwatesa wananchi kwa matakwa ya wanasiasa wenye UCHU?? Tuboreshe tulichonacho kuliko kuongeza matatizo..
 

matatizo yapo kwa wanasiasa wanaotaka kuchukua nafasi hii kuona muungano unakufa, kwanini muungano huo haukuwa tatizo 40 yrs ago?? tumeanza kuwa na kizazi kisichojali misingi bora tuliyowekewa na babu zetu, tumepotoka na tunakoelekea ni kuiua hii nchi, historia itatuhukumu kwa kuwa waroho wa mambo madogo na kuacha kuangalia faida za kuwa na serikali moja imara yenye amani na maelewano, wakati ni sasa wa kuacha faida binafsi za muda mfupi na kuangalia vizazi vijavyo vyenye muungano bora,
 
katiba ya Jamhuri ya MUUNGANO WA TANZANIA, haijasema hivyo, hivyo amendment hiyo ni BATILI ON THE EYES OF THE CONSTITUTION OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, 1977.

nibatili kivipi wakati tayari inatumika na katiba ya muungano inaifwata mfano kuchelewa kwa ukusanyaji maoni kulisubiri baraza la wawakilishi Zanzibar liizishe azimio toka bunge la jamhuri ubatili wake uko wapi Zanzibar sasa hivi ni sovereignty government ambayo haijazinishwa!!!!
 

mkuu panua kichwa chako hata hizo gari za gharama zinaongezea wananchi mzingo tatizo la ccm wanapenda ccm iendele kuwa state party baadala ya political party legitimate hiyo haipo mkuu wajipange upya
 
Kwanini serikali 3?? kama si ulafi wa wanasiasa wachache, nini cha ziada? tuvunje Muungano tu - ndio suluhisho. Zanzibar waende kivyao na Tanganyika/Tanzania twende kivyetu na nina uhakika majority kutoka pande zote watakuwa happy tu
 

hapo umenena mkuu.
 
uko sahihi mkuu maana umepata stroke, stroke huwa ni tatizo baya sana kiafya, linaweza kuathiri hata uwezo wa kufikiri. Kwa kuwa Tanganyika haupendi irudi katika enzi yake , bali unataka serikali mbili na nchi mbili na sio nchi moja, unaonaje sasa uwashawishi Wazanzibari wakubali kuvunja serikali yao na nchi yao, maana wameendesha serikali yao kwa kipindi cha miaka 50, sasa iwe zamu ya Tanganyika, nasi tuendeshe serikali ya Jamhuri ya Tanganyika kwa miaka hamsini, yaaani iwe ni kupokezana, Jamhuri hii ikifikisha miaka 50, iwe zamu ya Zanzibar tena kuendesha serikali yao, si itapendeza!!!
Ili hilo wazo likubaliwe patachimbika kama unadhani natania kawagise Wazenj na wazo hilo, uone moto wake!!! kajaribu!!

Kama hilo haliwezekani, basi Jamhuri ya Tanganyika, Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba waridhie maoni ya Watanganyika na wengine yaliyowasilishwa kwao na Jaji Mkuu Mstaafu,Waziri Mkuu Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu, Jaji Warioba kwa niaba ya Wananchi wote
 

Na mimi napendekeza kuwa sasa ni ZAMU ya Zanzibar kuwa kama Tanganyika! Kivipi? Iwepo Serikali 2 yaani Serikali ya Jamhuri ya Zanzibar itakayoshughulikia mambo ya Zanzibar na ya Muungano, halafu kuwepo na. Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika ambayo ni huru,itakayoshughulikia mambo ya Tanganyika tu, kwani ni Zamu ya Watanganyika nao kupumua! Hiyo ni kama muungano uwe wa serikali2, la sivyo serikali 3 haziepukiki!
 
AhAAAAAAAHHHaaaahhh!!!! yaani unamaanisha nao watulipie mishahara kama sisi tunavyochangia bajeti yao kiaina, watulipie bill za umeme kama sisi tunavyofanya, te te te te h!!! watakimbia nchi mkuu
 

Mtanzania yeyote mwenye akili timamu hawezi kupingana na maelekezo muhimu ya Jaji Warioba... kwa maana nyingine watanzania wamefika katika hatua muhimu ya historia ya nchi yao....Jaji Warioba na tume yake wamefichua mambo yaliyofichika takribani miaka 30 nyuma... utashi wa Tume hiyo kwa watanzania unabaraka tele kwa wa Tanzania walio wengi... Mungu atawabariki wajumbe wote walioamua kufunguka na kuacha unafiki ambao umezoeleka miongoni mwa viongozi walio wengi... wanaopenda sana kujaza matumbo yao na kuangalia ubinafsi ... kusahau taifa linataka nini .. viongozi waliopata nafasi kuwa madarakani wanajisahau na kuwasahau waTZ ...

 
pinga hoja za warioba kwa hoja cyo kwa nguvu, miaka yote hiyo kero zinazidi kuongezeka, mmlikuwa wapi kuzizungumzia hadi zanziba ikavunja katiba?
 
Serikali 3! Ama suala la muundo wa kiutawala uweje, hiyo ndo inapaswa iwe kazi ya Bunge Maalum la Katiba kuboresha yale maoni ya Wananchi!

Bahati mbaya ni kwamba hao wajumbe wote hakuna nayefikiria kuhusu muundo wa Muungano, bali wanawaza Serikali 3. Serikali tatu maana yake si ni kwamba kila Seriklai iwe na mamlaka yake ?
 
huo ni mtazamo wake, hakuna nchi duniani yenye serikali tatu, labda sisi tuwe wa kwanza..3 hazina tija yoyote kufurahishana wakati tunaingia hasara, siungi mkono, suluhisho ni serikali moja tu

Jenga hoja kiongozi, kikubwa ni hoja kama zina mashiko husije ukatuletea ooo gharama za kuendesha serikali 3 ni kubwa wakati pesa zinazo ibiwa kwa kila mwaka ni nyingi mara 4 ya kuendesha hizo serikali 3.
 

Magamba jasho hadi ktk visigino.wamezowea vya kunyonga
 
Lazima utakua unasumbuliwa na Maradhi Zittophobia...kama hujui mchango wake katika Taifa Hili..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…