Zitto Kabwe aunganishe nguvu na vile vyama 13 vya siasa vilivyopinga maandamano haramu ya Chadema yaliyopigwa marufuku na Polisi

Zitto Kabwe aunganishe nguvu na vile vyama 13 vya siasa vilivyopinga maandamano haramu ya Chadema yaliyopigwa marufuku na Polisi

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Hii italeta pumzi mpya, changamoto mpya kwa ccm, mageuzi, na uelekeo mpya wa upinzani nchini.

Hata hivyo,
Hatua hiyo muhimu itategemea sana, utashi na utayari wa uongozi wa vyama hivyo vya kisiasa nchini, kuweka maslahi ya Taifa mbele, na kuweka kando tofauti zao za kisiasa, usaliti, ubinafsi, tamaa na uchu wa madaraka na vyeo.

Wananchi wameshaikatia tamaa Chadema wameichoka na wamechoka kuburuzwa kwa style ile ile miaka nenda miaka rudi. Maelfu kwa maelfu ya wanachama wa Chadema hivi sasa maeneo mbalimbali nchini, wanajiunga ccm hivi sasa, na bilashaka yoyote maelfu wengine watajiunga vyama vingine vya upinzani, kuepuka kutolewa kafara na kuchukuliwa misukule na Chadema.

So,
Hiyo ni fursa ya kipekee sana kwa Zitto Kabwe kuitumia kuunganisha upinzani, na kuchangia mabadiliko na uelekeo wa Kidemokrasia kupitia muungano mpya wa upinzani nchini 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Hata wakiungana hawawezi kuitikisa CCM zaidi watakuwa kama wanajenga mnara wa Babeli kwa kuanza kutofautiana Lugha.
 
Hivyo vya 13 + CHADEMA havina wanachama zaidi ya viongozi hivyo hata vikiungana kuitoa CCM bado ni ndoto ya mchana!
 
Hivyo vya 13 + CHADEMA havina wanachama zaidi ya viongozi hivyo hata vikiungana kuitoa CCM bado ni ndoto ya mchana!
sio kwaajili ya kuitoa ccm kwenye hatamu ya kuongoza nchi bali ni tu kubadili pumzi na uelekeo wa upinzani nchini 🐒
 
Back
Top Bottom