Zitto Kabwe awa mbogo, awashukia vikali wanaodai Makamu wa Rais, Dkt. Mpango ni Mrundi

Kubaya kama sura yako??!!

Kama kubaya ulifuata nini??!!
Hahahahah nilikuwa kambi moja huko Kati iko kasulu pale[emoji1][emoji1]

Kunywa maji mwanangu[emoji1787][emoji1483]

Aisee kasulu kubayaaaaaaaa!!!! Bonge la tope
 
Kigogo ana chuki na Dr. Mpango toka alivyoteuliwa kuwa VP na mtu wake kuukosa huo u- VP, toka pale hata simuamini huyo jamaa na mambo yake, naamini kuna kundi la wanasiasa nyuma yake linamtumia kwa malengo yao binafsi.
 
Weka ukabila kando, weka siasa kando na ujibu hoja kwa ushahidi na na vielelezo.

Mimi binafsi ninajua kuwa eneo la mkoa wa Mwanza ni eneo ambalo lilikuwa ni malezi ya wakimbizi toka Rwanda, Burundi na Kongo na wanapokaa Mwanza kwa muda mrefu walikuwa wakijiita ni watanzania. Walihamia Tanzania miaka ya hamsini

Moja ya eneo ambalo wakimbizi wa Rwanda au Burundi waliishi kwa kwa muda mrefu mkoani Mwanza ni Mkuyuni. Na mwaka 1994 baada ya vita vya kimabari kuisha tulishudia wengi wakiondoka Tanzania kama wakimbizi na kurudi Rwanda au Burundi.

Hivyo usidhanie kuwa uraia wa mtu utakanushwa kwa porojo na maneno kama unavyodhania.

Kama mtu sio mtanzania acha ukweli uwekwe wazi.
 
Uhamiaji ni chombo pekee kisheria kina mamlaka ya kuhoji uraia wa mtu na siyo users wa twitter au Jamiiforums. Mkiwa na mashaka na urai wa mtu mnaenda kuripoti uhamiaji na una haki ya kufuatilia ripoti yako.
 
Zitto Kabwe anashupalia vitu vidogo vidogo sana.

Mbona mzee Mkapa rip kwao ni Lupaso kijijini tatizo ni nini?!!
 
kwahiyo hata wewe uliyeandika uzi huu unaamini 85% ya watu wa Kigoma sio WaTanzania, mbona hii nchi inavituko
 
mwenye uraia nchi hii na ulimwengu ni ADAMU na HAWA na walikuwa weupe sio waafrica
 
mbona kenya mambo haya hayapo mpaka waziri wa utalii mwarabu mkuu wa majeshi alikuwa msomali mkuu wa polisi alikuwa msomali
 
Hapana ifike mahali tujue chombo cha uhamiaji kipo kwa ajili ya mambo kama hayo ni jukumu la watu kuripoti uhamiaji na wao watoe majibu. Nadhani pia Watanzania ambao hawatoki mipakani hawaelewi jinsi wanavyowakera wenzao pale wanapohoji uraia wao. Kwanini mtu wa Dodoma, Singida, Kilimanjaro ajihisi raia kuliko mtu wa Kagera, Kigoma na Mtwara .Hata hivyo NIDA wanahitaji kufanya jitihada kutoa vitambulisho vya taifa kupunguza hii kero.
 
Kumbe homeboy ni homeboy tu. Kiongozi wa Act wazalendo amefura na amekuwa kama mbogo. Hii ni baada ya video iliyosambaa mitandoni ikimuonyesha Makamu wa Rais wa sasa akicheza ngoma inayofanana na ya kirundi.

View attachment 1742127
Kwa mtizamo wangu kadhia si ya kupuuza hata kidogo.
Tuliwahi kusikia kuwa Marehemu Mkapa hakuwa mzaliwa bali alikuja na baba yake.
Marehemu Magufuli naye tukasikia ya kuwa alikuja na mama yake toka Burundi.
Huu msiba wa Magufuli umekuwa wa kwanza kumuondoa Rais aliyepo madarakani na tayri akili inaanza kutujia kuwa makamu wa Rais ni lazima awe mtu aliye kamilika kwani anaweza kuwa Rais wakati wowote.
Dr.Philio Mpango,toka hadharani na sawazisha hili jambo mapema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…