Tatizo letu hasa upinzani ni kuchafuana. Mtu yeyote mwenye kujuwa historia ya TZ pamoja na makabila yake anatakiwa kujuwa kuwa watu wa mipakana wana makabila yanayoshahibiana. Waha kwa kifupi wana uhusiano na Warundi. Nafikiri siku hizi hata historia ya makabila hatujifunzi. Wale tuliyokuwa shule miaka ya 1950 tulijifunza juu ya makabila na asili zao. Ndiyo maana ukinitajia Mwami Ntare ninajuwa ni nani na alitawala wapi. Sasa hivi watu wanasikia Wahutu na Watusi, wakidhani hayo ni makabila kumbe siyo. Hata Waha, Wanyamwezi, na Wasukuma wana wahutu wao na watusi wao.
Hao wanamuita Mpango Mrundi ni CHADEMA waliokosa sera wamebaki kuchafuana. Hata kama angekuwa Mrundi, kwani Warundi wangapi wamechukuwa utaia wa TZ kutokana na migogoro yao. Je, akiwa na asili ya Kirundi lakimi ni Mtanzania utamnyima hiyo nafasi kwa sababu asili yake ni Burundi. TZ haibagui wananchi wao kwa dini, kabila, wala asili yao. Ukishakuwa Mtanzania ni Mtanzania tu, hata kama wewe ni mzungu. Hivi mliwa kuwaona mawaziri wa Nyerere ambapo kulikuwa na wazungu, waafrika, na wahindi. Hivi leo hii ikitokea hivyo, kelele za CHADEMA zitafika wapi? Au watanyamaza kwa sababu huko Ulaya ndipo alipo prpogandist wao mkubwa anti-pus Lissu.