Zitto Kabwe: Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa ambayo hamjawahi kuyaona, tusipoteze hii fursa jamani

Zitto Kabwe: Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa ambayo hamjawahi kuyaona, tusipoteze hii fursa jamani

Mkuu hebu weka hisia zako pembeni kaskilize nina hakika hujasikiliza alichosema ukimsikiliza utagundua ulikuwa umewaza tofauti. Hakuna sehemu aliposema bandari ijengwe kwa mkataba uliyopo maana hata yeye kasema hakuna aliyewahi kuona huo mkataba mbali na ikulu na angependa uwekwe wazi watu wajadili.
Hayo ya kusema meli kubwa ma bandari kuwa ya tatu kwa ukubwa duniani alionhelea presentation wao kama wabunge waliyooneshwa. Lakini mkataba serikali specifically ikulu mpaka leo haikuwahi kuuweka wazi.
Crap
 
Shida mnaochangia hamkumsikiliza. Kasema waliona plan ya huo mradi lakini mkataba haukueahi kupelekwa bungeni wala hawakuwahi uona uko ikulu tu, kaomba badala yake uwekwe wazi watu wajue kilichokuwemo kuliko tu mtu kusema tu kwanini usiwekwe wazi...
Wanasiasa waongo usiwaamini. Bagamoyo haiwezi kuwa bandari ya 3 kwa ukubwa duniani.

Na habari ya meli kubwa(Mega Ship) kuleta mizigo Kisha meli ndogo (Feeder vessel) kuja kuchukulia mzigo Bagamoyo hiyo itakuwa kawaida maana bandari tulizonazo karibu ni Berbera,Mombasa,Beira na Port Elizabeth.

Hapo wa kututegemea ni Mombasa na Beira, Port Elizabeth wao Wana uwezo wa kuhandle meli aina yoyote na ni cost kuja kufata mzigo huko. Hao Somali wao Transhipment hawana shida nayo wapo karibu na Arabuni ambapo meli kubwa zinaacha mizigo ambayo meli ndogo hufata.
 
Zitto siku zote ni mnafiki, Mwendazake sikuwai kukubaliana nae katika mambo mengi ila hapa kwenye huu Mradi wa bandari ya Bagamoyo alikuwa mzalendo, namuunga mkono.

Kama wanataka tuwaunge mkono waweke mkataba hadharani kwanza
 
KC wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kitu ambacho wabunge wengi hawakijui ni kwamba Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa makubwa kutoka huko duniani ambazo hatujawahi kuziona hapa Tanzania....
Kwani bandari ya Dar es Salaam imekwama nini kupokea hayo mameli makubwa au ina maji kama ya MTO?
 
Ni muda gani China anakuwa rafiki na ni muda gani anakuwa bepari😅😅😅 kuna muda mara anasifiwa na kuna muda mara anapondwa.
Anakuwa bepari pale anaponyonya nchi maskini kama Zambia kwa kutoa mikopo yenye masharti magumu.china ya mao ndo ilikua rafiki,lkn ya sasa waulize wakenya
 
Hilo la kuchukua mkopo na kujenga wenyewe lina risk kubwa mno! Huwezi kurudisha investment ya dola bil 10 kwa miaka 8. Hilo linawezekana kwenye mitambo siyo miundo mbinu ya bandari. Tunaweza kuangalia best practice na kunegotiate.

Kuhusu kuendesha wenyewe,sina uhakika kama tunaweza! Bandari ya Dar ilitushinda kuendesha. Kwa sasa,wanaoendesha ni TICTS siyo serikali.
Bora mkopo wa pesa kuliko masharti ya wao kukusanya mapato miaka wanayotaka.
Hao TICTS bandari ya Dar wanafanya kwenye gati chache ambazo ni za container tu. Kwenye Gati (Berth) nyingine hawahusiki.
 
Mchina kama ni ela kagawa za kutosha
Basi mtueleze na yale masharti 11 yamebadilishwa and you yale yale ya kipumbavu
 
Bongo Bahati Mbaya! Mh. ZZK akiwa na Spika Nancy Pelosi, jamaa siyo "mshamba" kabisa!
NancyPelosi-ZittoKabwe-DennisKucinich.JPG
 
Kwanini tusikopeshwe pesa ili tujenge sisi na kurejesha mkopo huo ili tuone hiyo mijimeli?
 
Details zinadai kwamba Wachina wangeleta management team yote kwa miaka 100 ijayo na pia mapato yote ya hiyo bandari kwa miaka 100 ni yao ili kurudisha mkopo wao, Tanzania haipati hata senti.
Mkuu BAK ,details za kutoka wapi!!?
Kama mkataba au makubaliano ya awali unao,tuwekee ili tujue mbivu ni zipi na mbichi ni zipi.
Vipi kama GNT wakakaa/wanakaa/wamekaa tena na China ili kutengeneza makubaliano/mkataba wenye maslahi zaidi kwa Tanzania halafu tukaambiwa ndio mkataba/makubaliano ambayo JPM aliyakataa!!?
 
KC wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kitu ambacho wabunge wengi hawakijui ni kwamba Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa makubwa kutoka huko duniani ambazo hatujawahi kuziona hapa Tanzania...
Bandari ya Tanzania au China.
 
KC wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kitu ambacho wabunge wengi hawakijui ni kwamba Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa makubwa kutoka huko duniani ambazo hatujawahi kuziona hapa Tanzania...
Ukubwa wa meli unatusaidia nini kama mnauza nchi yetu kwa vijirushwa uchwara? Toa faida za kisayansi badala ya upuuzi
 
China sio mwekezaji tu ni mnyonyaji kama wanyonyaji rasilimali wengine.

Mwekezaji gani hajengi viwanda badala yake anachukua tu tenda za kujenga kila kitu hapa barani Africa na kuchota rasilimali zetu?
Ni kwa sababu tenda ni deal making za viongozi wa Afrika kuibia waafrika wenzao pesa hivyo mchina hana hiyana maana nae anataka pesa sasa why aforce kujenga viwonder kama viongozi wa afrika wanataka kuneemesha mitumbo yao kupitia 50%? za rushwa
 
Huu mkataba hawawezi kukuwepa hadharani haraka mpaka wau edit kwanza
 
Eeenh Heeee!

Sasa Zitto anataka kushindanisha Bagamoyo na Lamu?

Haya mameli makubwa yapo mangapi dunia hii yapigane vikumbo kuja kwenye ukanda huohuo kiasi hicho. Biashara yote ya dunia itakuwa imehamia kwenye eneo hili?

Yaani tujenge kwa sababu ya ushindani tu na hao majirani zetu ambao wao tayari wamekwisha anza kazi kwenye bandari yao?
 
Tunajua kilichotokea Zambia na Sri Lanka, na tunajua itafuatia Kenya, Djibout muda sio mrefu
Chinese goverment are Mafia like state, hizo kampuni na contractors zote ni mali ya serikali tukiiangia tumekwisha............

 
Back
Top Bottom