Zitto Kabwe: IPTL ni dude linalofufuliwa kila Awamu

Zitto Kabwe: IPTL ni dude linalofufuliwa kila Awamu

Sasa mbona huyo anaesema anadaiwa kamwambia hilo deni mahakama ilishaamua (umesikiliza hata clip ya dakika mbili iliyowekwa humu JF).

Kwa akili zako mtu anaekwambia deni ambalo mahakama limeamua, litakuwa bado kwenye orodha yake ya madeni?

Hata hao TRA watakubali uweke deni ambalo mahakama ilishaamua kwenye hesabu zako, halafu ulitumie kama debt interest kukwepa kodi.

Zitto atakuwa keshaongea na rafiki yake Makamba na Chande kujiridhisha zaidi hilo deni halipo kwenye vitabu vya TANESCO na ata uongozi wa leo hawalitambui.
Sasa anayalifufua ni Tanesco na wanaoshindwa kulifuta maana wanaweka matakataka ambayo hayastahili hata kidogo
 
Mbona mwaka jana , mwaka juzi huyu CAG hakutaja hilo deni la IPTL kwenye ripoti zake, mbona CAG aliyepita pia hakutaja hilo deni la IPTL kwenye kaguzi zake

je hilo deni la iptl ni jipya limejulikana mwaka huu?

Huyu CAG kasetiwa na watu wenye IPTL makusudi hili wapate sababu ya kupiga hela
Kivipi kaka nipe fact
 
Hiki dude linaondoka mpaka hapo siku CCM itaondoka madarakani.

Ni dudu ( toto) la CCM
 
Yalivyo ya ajabu ccm eti yako busy majukwaani kuomba kura, what for? Kila mahali kumeoza, mbona wasi shughulikie na kusafisha nyumba kabla ya kupanda jukwaani?, tuna hitaji kuwa ondoa hawa mchwa , tunatakiwa ku declare ccm ni janga la taifa, kila kitu kisimame kwa muda ili watanzania wote tujadili kuhusu hili janga.
 
Tukisema tuchukue hiyo logic yako deni ni jipya ina maana interest ya deni ni over 100% ndani ya mwaka mmoja?

Unashindwa hata kuelewa simple concept, madeni ya muda mrefu ya shirika yanawekwa kwenye N.L na TANESCO watakuwa na orodha.

Madeni yao ya muda mrefu serikali iliyachukua yote, sasa hilo deni la IPTL atakama lingekuweko limerudi vipi tena TANESCO.

Mbaya zaidi TANESCO wenyewe washamwambia CAG kwa maneno yake mwenyewe jana wao hawalitambui.

Sasa na CAG labda ueleze hilo deni umeliona kwenye vitabu gani, kama kwenye vitabu vya TANESCO halipo.
Umesoma ripoti ya CAG ujue amelitoa wapi? Nachopinga ni speculation zako kabla haujasomq
 
Kuona logic ya swali langu, inabidi kwanza ukajifunze ni vitu gani vinawekwa hapo kwenye non current liabilities, vinginevyo tutakuwa tunazunguka tu.

Shirika halina deni kwenye vitabu vyake, wewe unazungumza IPTL ni kama mkataba wa 2023-2024
Labda nikuulize, serikali kuu ikilichukua deni kutoka TANESCO balance sheet inasomaje na wakisema lirudishwe Tanesco balance sheet mpya itasomaje? Na pia dispute settlement ikitoa award kuwa ni deni halali na mkakubali kulipa hakuna changes kwenye hiyo statement of financial position?
 
Balance sheet niliyokupa ni hiyo kabla deni alijafutwa.

Nani anadai kwenye non-current liabilities zao, pembeni ya aina ya deni kuna number labda (29) or whatever hiyo inakwambia maelezo zaidi ya deni lote yapo kwenye notes (29).

Sasa angalia Current liabilities na Non-Current liabilities; chagua deni moja nenda kwenye notes, soma wadeni wote ukiona IPTL njoo utuonyeshe na sisi.

Vinginevyo hilo deni halikuwepo kwenye vitabu vya TANESCO muda mrefu sana, labda wawe wamelirudisha upya.
 
Balance sheet kabla ya deni niliyokupa ni hiyo kabla deni alijafutwa.

Nani anadai kwenye non-current liabilities zao, pembeni ya aina ya deni kuna number labda (29) or whatever hiyo inakwambia maelezo zaidi ya deni lote yapo kwenye notes (29).

Sasa angalia Current liabilities na Non-Current liabilities; chagua deni moja nenda kwenye notes, soma wadeni wote ukiona IPTL njoo utuonyeshe na sisi.

Vinginevyo hilo deni halikuwepo kwenye vitabu vya TANESCO muda mrefu sana, labda wawe wamelirudisha upya.
Naomba ni save hii comment yako mpaka ripoti ya CAG ikiwekwa public ndio tutarudi kuona NAO walitoa wapi hilo deni.
 
IPTL ni mitanzania ya hapa bongo, na hiyo mijitu ndio yenye sumu zote za kuuwa wenye viherehere nchini haijarishi hata kiongozi wa nchi

Kama ilishaamriwa na Mahakama za Rufaa ikaisha, kwa nini liibuke kwenye serikali inayoongozwa na mtu mpoole mama wa watu?
Wekeni hukumu hapa ili wadau waione.
 
Back
Top Bottom