Zitto Kabwe: Iundwe Tume kwa ajili ya ukiukwaji mkubwa wa Haki za Kibinadamu awamu ya 5

Zitto Kabwe: Iundwe Tume kwa ajili ya ukiukwaji mkubwa wa Haki za Kibinadamu awamu ya 5

Halafu utadhani maisha yalianza 2015 wakati wakina Dr Ulimboka walitekwa na kung'olewa kucha awamu ya nne.Kuna watu walimwagiwa tindikali,kulishawahi kuwa tuhuma za wanasiasa kulawitiwa katika kampeni za chaguzi ndogo.Kuna watanzania waliofukiwa katika machimbo ya madini.

Hiyo tume ianze kufanya kazi kuanzia mwaka 1985.Wakina Pinocchet walitenda makosa miaka mingi sana iliyopita wakala mshahara wao.

Huyu Zitto Kabwe anatumika na baadhi ya watu ndani ya CCM.Hatutokubali pesa za walipa kodi zitumike kwa mizaa na malengo ya wapumbavu wachache wa nchi hii.
Wacha tume ya majaji wastaafu iundwe ili ukweli ujulikane na Kusiwe na kumsingizia Hayati mambo ambaya hayamhusu au unasemaje?
 
Mimi nilivunjiwa nyumba mbili na Utawala wa Magu, pale kibamba.
Hatukupewa hata kiwanja , bali vitu vuetu vilisagwa na kalandinga .
Lilingilia mlango wa mbele na kutokea mlango wa nyuma.
Mpaka mita ya umeme ilisagwa sagwa,,hatukuweza kutowa chochote ila ilikuwa taka taka tuu.
Mungu amlipe Jahanamu ya chini kabisa huko aliko, alijiona mwamba asiyeshindwa.
Nimeshuhudia kumuona Mamayangu Mzazi akilia kama mtoto mdogo,
Dada yangu mkubw alipigwa na stroke ,
na hivi sasa tunatanga tanga kwenye majumba ya jamaa wa karibu.
MUNGU HAKIMU
 
Omwami Zitto Kabwe Ruyagwa bado anazidi kutufumbua macho juu ya maovu yaliyofanywa na Magufuli.

Ameomba iundwe tume maalum ya majaji ili kuchunguza maovu waliyofanyiwa binadamu wenzetu.

.https://www.instagram.com/p/CckuHiEIodY/?igshid=YmMyMTA2M2Y=
 
Pumbafu kabisa. Mlisoma shule gani nyie wajinga. Unajua tofauti kati ya ''Hayashauri'' na ''Ashauri''? Hujui heading yako inamaanisha kitu kingine kabisa tofauti na Zitto alivyosema!
Mkuu, Hiyo “Hayashauri” umeitoa wapi au ndio muda wa kubadilisha miwani yako?!
 
Kuna haja kubwa ya kuundwa kwa Tume ya Majaji kwa ajili ya kuwapa nafasi waathirika wa vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binaadam vilivyofanyila wakati wa utawala wa Rais Magufuli kupata Haki zao. Watu ambao wamepoteza ndugu zao, waliotekwa, waliobambikiwa Kesi nk. MUHIMU

I repeat a call for a commission of inquiry, to headed by a retired Judge of Court of Appeal, on atrocities committed during the tenure of J P Magufuli administration. All Killings, abductions, disappearance of people, trumped up charges of money laundering MUST be investigated


Hiyo tume ya kijaji ianze kwanza kuchunguza chanzo cha kifo cha mpendwa wetu JPM. Kwa yanayoendelea sasa na kauli hizi za ZZK, kuna namna anahusika au anawafahamu wahusika wakuu
 
Uanzishwe uzi wa matukio awamu ya 4 vs 5 tuone hiyo tume ilipaswa kuliliwa toka lini! Wanasiasa ni wanafiki sana, hawa hawa ndio walitufanya wengine tutende dhambi ya kumchukia EL kuwa hafai kwa ufisadi wa kutisha na chanzo cha chain za ufisadi nchi hii alafu wakaja kumsafisha!

Naunga mkono tume ya kuchunguza uhalifu toka awamu ya 4 tusigeuzane watoto wadogo hapa.
 
Umoja Party, Walipo tupo,

Huku ndio kuzikwa pembeni mwa JPM, zitto aipate hii

Na afahamu, waliompenda JPM na hata sasa wanaomkubali JPM ni wengi Mara mia kuliko wanachama na chama chake kwa ujumla!
 
Zzk ni mnafki mbona hakusema chochote wkt wa Jk walivyoumizwa akina Absalom Kibanda, Dr Ulimboka, mauaji ya Mtwara wkt wakipinga uvunaji wa gesi?
 
Ni jambo jema. Ndivyo ilivyofanyika pia kwa Stallin.

Marehemu hahukumiwi, lakini washirika wake walio hai, wafikishwe mahakamani na kuhukumiwa.

Tukifanya hivyo, kila mtawala atakayrkuja siku za mbeleni, ataweza kuwaheshimu wanachi, tofauti na ilivyokuwa wakati wa utawala wa awamu ya 5 ambapo watawala walifanya mambo mengi ya hovyo dhidi ya wananvhi.e
 
Back
Top Bottom