Kama ndege sita zipo grounded, hilo haliwezi kuwa kosa la Magufuli, tatizo la Zitto amekariri kila siku kutupa lawama kwa mtu mmoja ambaye kwa sasa hayupo, na kumlinda yule aliyepo, akidhani wote hatuna akili.
Hizo ndege kama zimekosa matunzo, na sasa Magufuli amefariki karibia miaka miwili iliyopita, Zitto anatakiwa ajue wakuwalaumu ni hawa waliopo kwa matunzo mabovu ya hizo ndege, na sio yule aliyezinunua.
Anachofanya ni kama ujinga wa watoto kumlaumu baba yao kwa ubovu wa nyumba aliyowajengea baba yao aliyefariki, wakati wao ndio waangalizi wa nyumba hiyo, ujinga wake ni kutumia kigezo cha wingi wa ndege kama sababu ya hizo ndege sita kuwa grounded, hoja ya kijinga kabisa.