Usizungumzie hisia, zungumzia facts.
Ndege 6 zimekuwa grounded, ni fact.
Ndege hazifanyiwi service ni hisia.
Ndege ni mitumba ni possibility, kwa sababu si kawaida ndege mpya 6 kwa wakati mmoja ziharibike, na si jambo linaloingia akilini kuwa shirika limeshindwa kuzifanyia service ya kawaida ndege 6.
Inatakiwa itolewe taarifa kamili juu ya ukweli wa kila jambo kama ilivyokuwa kwenye mabehewa ya treni tuliyoambiwa ni mapya, baadaye ikagundulika ni mitumba. Rais na Waziri walikuwa waungwana katika kulikiri hilo, lakini kuna wapamve wajinga, waliojifanya ni watetezi wa Serikali, ni watetezi wa Rais Samia, walikuwa wakiropoka tena kwa nguvu kweli kuwa mavehewa ni mapya. Hana hata access ya kujua manunuzi yalivyofanyika, halafu anabakia na ubishi wa kijinga.
Kama huna uhakika, changia hoja, toa mawazo yako, lakini usiwe mbishi.