Zitto Kabwe kulamba Ubunge wa kuteuliwa na Unaibu Waziri.. Salum Mwalimu anaamini Samia hatamtupa

K

Kwani Halima ni chama gani vile?
Alikuwa Chadema. Sasa hivi si mwanachama wa chama chochote.
Wanaohangaika ni CHAUMA kuliko chadema kwa CHAUMA. Lengo la CHAUMA ni kukidhoofisha chadema kwa kufadhiliwa na ccm.
Msiwe kama mtoto anayeapa hajalamba sukari wakati mdomo wake umejaa sukari. Humu ndani pamejaa mabandiko yakikiandama Chaumma. Makamu Mwenyekiti wa Chadema amemtukana Suzan Kiwanga ambae ni kiongozi wa Chaumma hadharani bila kujibiwa. Mwanachama pekee wa Chaumma anayewaandama Chadema ni Yericko. Waliokuwa Chaumma wangetaka kukidhoofisha Chadema wasingeondoka Chadema. Toeni ushahidi wa ufadhili wa CCM kwa Chaumma. Hamna tofauti na wale wanaosema Heche ni fisadi bila ushahidi wowote.
Asilimia kubwa ya waliohamia chauma kutoka Chadema walijifukuzisha wenyewe baada ya uchaguzi wa viongozi wa chama ndio hadi leo chuki hazijaisha na miongoni mwao wanaomba viongozi wa chadema wauwawe au wakamatwe na kufungwa.
Uongo ni kitu kibaya. Sehemu kubwa ya viongozi waliohamia Chaumma kutoka Chadema waliondoka wenyewe na hawakufukuzwa na mtu. Wala haikuwa kwa sababu ya uchaguzi. Walijiondoa baada ya kuona kuwa hawakubaliani na mtazamo wa uongozi wa sasa wa chama chao. Badala ya kubaki kinafik wakaamua kuondoka na kukiacha kiendelee na mikakati yake bila pingamizi lolote. Wengi wao hawana chuki na Chadema na wanakitakia mafanikio. Mwanachama pekee ambae ana uhasama na Chadema ni Yericko. Yericko sio msemaji wa Chaumma kama ambavyo Hilda sio msemaji wa Chadema. Hata hivyo ana haki ya kuwa na mawazo yanayo tofautiana na ya wenzake. Hiki ni kitu ambacho Chadema imesahau ingawa inajiita Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Achaneni na Chaumma. Mbaya wenu ni CCM.

Amandla...
 
Golugwa je?
Nani anamjua Galugwa? Hana charisma ya wakina Heche. Itamchukua muda kujijenga kuwafikia. Hata yule kiongozi wa Bavicha. Huwezi kumlinganisha na waliomtangulia. Bawacha nao wako kimya. Brenda anajitahidi lakini nae bado. Chadema ina kazi kubwa ya kuwajenga.

Amandla...
 
Imepwaya ila cha ajabu haipewi uhuru wa kufanya mikutano ya siasa
Chadema ya Mbowe ilizuiwa kufanya mikutano ya siasa na maandamano, kwa viongozi wake rumande kulikuwa nyumbani. Wanachama na wafuasi wao walipotezwa, waliawa na wengine kufunguliwa kesi za ajabu.

Yote haya hayakuwafanya waache mpambano. Waliita maandamano hata pale jeshi lilipotangaza siku ya usafi. Waligoma kushusha bendera za chama vyao pamoja na kushambuliwa na wapinzani wao.

Walifanya jogging huku wamevaa sare za Chadema, walijazana makanisani wakiwa na sare za Chadema, walijigalagala nje ya balozi, walijazana Mahakamani wakati wa kesi ya Mwenyekiti wao. Hawakungoja kibali cha serikali kama ambavyo warithi wao wanavyo subiri.

Chadema ya leo inaogopa hata kupandisha bendera yao baada ya kukatazwa na wapinzani wao! Ni aibu kusema kuwa wanashindwa kufanya siasa kwa sababu hawana kibali. Huko ndio kupwaya.

Amandla...
 
Amteue tu si muislamu mwenzie. Hatujali vyeo wanapeana kama peremende!
 
Kwenye Orodha ya watu nimeapa kutowaamini kwenye haya maisha ni pamoja na hao wanasiasa

Wanabadirika kama mawimbi ya bahari
Kubadilika badilika ndiyo mwendo wa siasa.
Siasa ni kazi ya ovyo, kama huwezi unafiki kaa mbali nazo bro.
 
Wamechelewa hata hivyo! 😊
Zitto ni wa kushindwa ubunge with a big margin... kwao mwandiga na comedian baba levo!! 😊
Angeshinda asingewapigia magoti, kwa kuaibishwa kwake imebidi awe mpole, alidhani akisema wa mboga mboga tosha basi atamshinda diwani std VII kumbe wenzake wanamchora tu na hata maamuzi ya mahakama ilikuwa ni kumdhalilisha tu ili wenyewe waweze kummudu kirahisi .Kwa sasa Zitto mbele ya mboga mboga clan ni sawa na boflo kwenye urojo!
 
Chadema ya Mbowe ilizuiwa kufanya mikutano ya siasa na maandamano, kwa viongozi wake rumande kulikuwa nyumbani. Wanachama na wafuasi wao walipotezwa, waliawa na wengine kufunguliwa kesi za ajabu.

Yote haya hayakuwafanya waache mpambano. Waliita maandamano hata pale jeshi lilipotangaza siku ya usafi. Waligoma kushusha bendera za chama vyao pamoja na kushambuliwa na wapinzani wao.

Walifanya jogging huku wamevaa sare za Chadema, walijazana makanisani wakiwa na sare za Chadema, walijigalagala nje ya balozi, walijazana Mahakamani wakati wa kesi ya Mwenyekiti wao. Hawakungoja kibali cha serikali kama ambavyo warithi wao wanavyo subiri.

Chadema ya leo inaogopa hata kupandisha bendera yao baada ya kukatazwa na wapinzani wao! Ni aibu kusema kuwa wanashindwa kufanya siasa kwa sababu hawana kibali. Huko ndio kupwaya.

Amandla...
mbona sasa hao hao chadema walimuondoa mbowe kwa uchaguzi ambao kila kura ilihesabiwa waziwazi na tuliona

Na chama cha siasa lengo lake sio kufanya jogging,
Mazingira ya siasa ya sahivi kila mtu anajua yalivyo sasa kama na hili linahitaji ligi basi ntakuita hamnazo
 
Wamechelewa hata hivyo! 😊
Zitto ni wa kushindwa ubunge with a big margin... kwao mwandiga na comedian baba levo!! 😊
Ukiwa ndumilakuwili a.k.a msaliti laazima utapotea tu kwenye ulimwengu wa siasa kwa sababu wananchi watakutema na gharama ya kurudi tena kwenye umaarufu inakuwa ni ngumu
 
mbona sasa hao hao chadema walimuondoa mbowe kwa uchaguzi ambao kila kura ilihesabiwa waziwazi na tuliona
Na aliyesimamia huo uchaguzi ni Mbowe. Kukubali matokeo ni dalili ya ukomavu kisiasa.
Na chama cha siasa lengo lake sio kufanya jogging,
Chama cha siasa lengo lake ni kufanya siasa. Chama makini cha siasa kinatafuta njia mbadala kuendelea kufanya siasa pale ambapo njia za kawaida zimezuiwa. Jogging ni moja wapo ya hizo njia. Na serikali ilijua hilo ndio maana wakina Ruge walikuwa wanakamatwa kila wakifanya jogging. Walikuwa wanakaidi agizo la serikali kwa kutaa kuzuiwa kufanya siasa. Chadema ya sasa hivi haina huo ujasiri. Wanangojea wapewe kibali kufanya siasa.
Mazingira ya siasa ya sahivi kila mtu anajua yalivyo sasa kama na hili linahitaji ligi basi ntakuita hamnazo
Ukiniita hamnazo nakuweka kwenye ignore list. Mazingira yalivyo sasa hayana tofauti na yaliyokuwepo wakati wa JPM. Tofauti ni kuwa Chadema ya wakati ule ilipambana mtaani wakati ya sasa ujasiri wake ni mtandaoni.

Amandla...
 
Alikuwa Chadema. Sasa hivi si mwanachama wa chama chochote.

Msiwe kama mtoto anayeapa hajalamba sukari wakati mdomo wake umejaa sukari. Humu ndani pamejaa mabandiko yakikiandama Chaumma. Makamu Mwenyekiti wa Chadema amemtukana Suzan Kiwanga ambae ni kiongozi wa Chaumma hadharani bila kujibiwa. Mwanachama pekee wa Chaumma anayewaandama Chadema ni Yericko. Waliokuwa Chaumma wangetaka kukidhoofisha Chadema wasingeondoka Chadema. Toeni ushahidi wa ufadhili wa CCM kwa Chaumma. Hamna tofauti na wale wanaosema Heche ni fisadi bila ushahidi wowote.

Uongo ni kitu kibaya. Sehemu kubwa ya viongozi waliohamia Chaumma kutoka Chadema waliondoka wenyewe na hawakufukuzwa na mtu. Wala haikuwa kwa sababu ya uchaguzi. Walijiondoa baada ya kuona kuwa hawakubaliani na mtazamo wa uongozi wa sasa wa chama chao. Badala ya kubaki kinafik wakaamua kuondoka na kukiacha kiendelee na mikakati yake bila pingamizi lolote. Wengi wao hawana chuki na Chadema na wanakitakia mafanikio. Mwanachama pekee ambae ana uhasama na Chadema ni Yericko. Yericko sio msemaji wa Chaumma kama ambavyo Hilda sio msemaji wa Chadema. Hata hivyo ana haki ya kuwa na mawazo yanayo tofautiana na ya wenzake. Hiki ni kitu ambacho Chadema imesahau ingawa inajiita Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Achaneni na Chaumma. Mbaya wenu ni CCM.

Amandla...
Ni wapi niliposema walifukuzwa?
Umekuja pale pale ya kwamba miongoni mwao walijifukuzisha chamani baada ya uongozi uliokuwepo kushindwa.
 
Viongozi wangapi wa Chaumma wamerudi Chadema? Tuliambiwa Halima Mdee atarudi Chadema, yuko wapi?
Mimi kila siku huwa nawashangaa Chadema kuhangaika na Chaumma. Inaelekea wameanza kujutia uamuzi wao wa kukataa kuwasikiliza walipokuwa Chadema. Chadema ya sasa hivi imepwaya. Ukiwaondoa Lissu, Heche, Mnyika nani mwingine ana mvuto nchi nzima? Sugu na Boni wana nguvu katika majimbo yao tu. Nani mwingine? Labda Msigwa.

Amandla...

Na ambao wamewapoteza, wenye mvuto, walioenda Chaumma ni nani ?
 
Viongozi wangapi wa Chaumma wamerudi Chadema? Tuliambiwa Halima Mdee atarudi Chadema, yuko wapi?
Mimi kila siku huwa nawashangaa Chadema kuhangaika na Chaumma. Inaelekea wameanza kujutia uamuzi wao wa kukataa kuwasikiliza walipokuwa Chadema. Chadema ya sasa hivi imepwaya. Ukiwaondoa Lissu, Heche, Mnyika nani mwingine ana mvuto nchi nzima? Sugu na Boni wana nguvu katika majimbo yao tu. Nani mwingine? Labda Msigwa.

Amandla...
Zamani nilikuwa nakuona una akili, unamfunga mtu mikono na miguu halafu unamwambia mbona hutembei, akili za kijiko hizi.
 
Na aliyesimamia huo uchaguzi ni Mbowe. Kukubali matokeo ni dalili ya ukomavu kisiasa.

Chama cha siasa lengo lake ni kufanya siasa. Chama makini cha siasa kinatafuta njia mbadala kuendelea kufanya siasa pale ambapo njia za kawaida zimezuiwa. Jogging ni moja wapo ya hizo njia. Na serikali ilijua hilo ndio maana wakina Ruge walikuwa wanakamatwa kila wakifanya jogging. Walikuwa wanakaidi agizo la serikali kwa kutaa kuzuiwa kufanya siasa. Chadema ya sasa hivi haina huo ujasiri. Wanangojea wapewe kibali kufanya siasa.

Ukiniita hamnazo nakuweka kwenye ignore list. Mazingira yalivyo sasa hayana tofauti na yaliyokuwepo wakati wa JPM. Tofauti ni kuwa Chadema ya wakati ule ilipambana mtaani wakati ya sasa ujasiri wake ni mtandaoni.

Amandla...
Wewe niweke kwenye ignore list ila ukweli ni kwamba mtu akisoma post zako lazima akubaliane na mimi kwamba hamnazo

Ukomavu wa kisiasa my foot yaan makamu wako anapata matatizo ya kisiasa hata kwenda kumuangalia au kuhudhuria kesi hutaki alafu unasema ni ukomavu wa kisiasa wewe kweli hamnazo
 
Benki ya dunia na IMF mwaka 2019 viliitangaza Tanzania kuingia uchumi wa kati baada ya maboresho makubwa ya kiuchumi yaliyofanywa na serikali ya awamu ya tano iliyokuwa ikiongozwa na hayati Magufuli na Makamu wake Samia.

Serikali ya awamu ya tano ilifikia hayo mafanikio ya kuingiza nchi uchumi wa kati baada ya kubana matumizi, kudhibiti ufisadi, kujenga viwanda na kuhimiza wananchi kuchapa kazi kwa nguvu zao zote.

Hali ilibadilika ghafla baada ya Rais Samia kuapishwa serikali yake ya awamu ya sita ikaacha kuhubiri viwanda wala wananchi wake kuchapa kazi na akatangaza sera mpya ya kula kulingana na urefu wa kamba yako! Matokeo yake ni kuuzwa kwa sekta muhimu za kuingizia nchi kipato kama bandari zote na makaa ya mawe.

Kutokana na kuzorota huku kwa usimamizi wa rasilimali za taifa Tanzania imeshushwa kutoka uchumi wa kati na sasa haieleweki iko uchumi gani! Hivyo Rais ajaye baada ya Samia atakuwa na kazi kubwa ya kubana matumizi, kudhibiti ufisadi serikali, kulinda rasilimali za taifa na kuirudisha nchi uchumi wa kati tena.

Kuna kila aina ya ushahidi kuwa Rais Samia amekata tamaa na haumizi kichwa tena kuhusiana na shida za watanzania ila inaonekana awamu yake hii ya pili alijipanga kula raha na kusafiri sana duniani ila mauwaji ya oktoba 29 yamempunguza speed baada ya kupigwa marufuku kusafiri ndani ya nchi za Ulaya.
Pale mjane wa marehemu Shetani la Chato anapohaha huku akimkumbuka na kuomboleza kifo cha Shetani lake.
 
Ila ukileta stori jaribu kwanza kuhakiki hata sheria, nafasi za Rais kuteua wabunge kwa wanaume zilishaisha maana wabunge wakuteuliwa na Rais ni 10 na angalau nusu wawe wanawake hivyo wanaume watano wameshafika hakuna namna Zitto anaweza kuteuliwa labda kama mmoja anyang'anywe nafasi.
 
Ni wapi niliposema walifukuzwa?
Umekuja pale pale ya kwamba miongoni mwao walijifukuzisha chamani baada ya uongozi uliokuwepo kushindwa.
Kujifukuzisha ina maana walifanya kitu wakafukuzwa. Hawa hawakufukuzwa kwa tafsiri yeyote. Walitangaza wenyewe hadharani kujitoa Chadema.

Na uongo mwingine ni kuhusisha kuondoka kwao na Mbowe kushindwa uchaguzi. Ingekuwa hivyo, wasingesubiri na wangejitoa baada tu ya Lissu kutangazwa kuwa mshindi. Waliondoka baada ya kutokubaliana na muelekeo wa Chadema ya Lissu. Ilikuwa haki yao na bado ni haki ya mwanachama wa chama chechote.

Amandla...
 
Kubadilika badilika ndiyo mwendo wa siasa.
Siasa ni kazi ya ovyo, kama huwezi unafiki kaa mbali nazo bro.
Kabisa Mkuu

Ukiwa mtu uliyenyooka huwezi kujihusisha na Siasa, maana zenyewe zinahitaji unafiki zaidi
 
Back
Top Bottom