Zitto Kabwe kulamba Ubunge wa kuteuliwa na Unaibu Waziri.. Salum Mwalimu anaamini Samia hatamtupa

Kubadilika badilika ndiyo mwendo wa siasa.
Siasa ni kazi ya ovyo, kama huwezi unafiki kaa mbali nazo bro.
Kabisa Mkuu

Ukiwa mtu uliyenyooka huwezi kujihusisha na Siasa, maana zenyewe zinahitaji unafiki zaidi
 
Halima ni kiongozi au ni Mwanachama wa CHAUMMA? Nahisi una lengo la kumchafua
Nimesema wapi kuwa Halima ni mwanachama wa Chaumma?

Halima Mdee hajawahi kuhamia chama chochote baada ya uanachama wake wa Chadema kufutwa. Watu wa Chadema ndio wamekuwa walimuombea arudi Chadema. Yeye mwenyewe hajawahi kusema kuwa ana nia hiyo.

Amandla...
 
Ni lini chadema walimuomba halima mdee kurudi chadema
Sababu unakaa nyuma ya keyboard unatunga uongo
 
Ni Makubaliano ya kile kinachoitwa nusu Mkate kati ya ACT Wazalendo na CCM.

Hii ni nafasi ambayo Mbowe alikuwa anaitamani, bahati mbaya chama chake kikasusia Uchaguzi.

Hata CHAUMMA wameshiindwa kufikia lengo. Kwani walisema wana nguvu ya kuisambaratisha CHADEMA, wakaomba wapewe Chopa za kuzunguka Nchi nzima na Magaei yenye uwezo.

Kazi iliwashinda CHAUMMA
Wenye Helkopta zao na Magari wakachukua. CHAUMMA kila mtu akaanza kufa na chake matokeo wakagombana. Wengine wanarudi CHADEMA huku Wengine wa huko Kigamboni Wakirudi kwa Mbowe awatete.

Sasa wana mpango wa kukusanya Tonetone kila mkoa.. Ili wapate nguvu ya kupambana na CHADEMA.

Baada ya viongozi wa CHAUMMA kugawana walopewa ya kuisambaratisha CHADEMA Je, CCM itawekeza tena hela kwa CHAUMMA?
Bila shaka wewe ni "akili kubwa" ya Chadema! Ahahahahaha!!
 
Ni lini chadema walimuomba halima mdee kurudi chadema
Sababu unakaa nyuma ya keyboard unatunga uongo
Ni wapi nimesema Chadema walimuomba Halima kurudi Chadema? Mimi nilichosema ni kuwa watu wa Chadema ( mashabiki wa Chadema) walitaka kutuaminisha kuwa Halima yuko njiani kurudi. Nakumbuka ilibidi Heche atoe tamko kuwa kama Halima anataka kurudi Chadema anajua utaratibu wa kufuata.

Ukiwa muongo usidhani kila mtu ni muongo kama wewe.

Aidha, kabla ya kurupuka jaribu kuelewa kilicho andikwa. Comprehension ni muhimu.

Amandla...
 
Viongozi wangapi wa Chaumma wamerudi Chadema? Tuliambiwa Halima Mdee atarudi Chadema, yuko wapi?
Mimi kila siku huwa nawashangaa Chadema kuhangaika na Chaumma. Inaelekea wameanza kujutia uamuzi wao wa kukataa kuwasikiliza walipokuwa Chadema. Chadema ya sasa hivi imepwaya. Ukiwaondoa Lissu, Heche, Mnyika nani mwingine ana mvuto nchi nzima? Sugu na Boni wana nguvu katika majimbo yao tu. Nani mwingine? Labda Msigwa.

Amandla...
Kwenye hii comment yako umesema tuliambiwa halima mdee atarudi chadema

Swali langu ni nani alikuambia halima mdee anarudi chadema
 
Catherine Ruge, Suzan Kiwanga, Kigaila, Devota Minja, Aisha Madoga n.k. Sasa niambie katika hao wangapi wamerudi Chadema?

Amandla...
Asha Madogo na Devita Minja ndio nani nchi hii kisiasa ???

Hayo majina mepesi sana kuliko ambayo CHADEMA imewahi kuwapoteza. Na ikabaki imara.

CHADEMA imepoteza Zitto , Kitila Mkumbo , Selasini, Mashinji, Msigwa, Mdee, Waitara, Wenje, Nassari, Juakali, na wengine kibao, na ikaendelea kusimama, sembuse Aisha Madogo na Kigaila ???

Chama kinatishiwa kufutwa, chama kinabembelezwa kifanye maridhiano unasema kiko dhaifu ?????? Hoja dhaifu!

Samia kasema wamekutana na vyama vyote wameelewana ila wanasubiri kimoja ndio wanakisikilizia. Chama dhaifu kitabembelezwa na Rais?? Kwa nn hawakuendelea kivyao bila hichob chama dhaifu ???
 
Hayo majina mepesi sana kuliko ambayo CHADEMA imewahi kuwapoteza. Aisha Madogo na Devita Minja ni nani hao ?

CHADEMA imepoteza kina Zitto na Selasini na Mashinji na Mdee na Kitila Mkumbo na ikaendelea kusimama, sembuse Aisha Madogo na Kigaila ???

Chama kinatishiwa kufutwa, chama kinabembelezwa kifanye maridhiano unasema kiko dhaifu ???

Samia kasema wamekutana na vyama vyote wameelewana ila wanasubiri kimoja ndio wanakisikilizia. Chama dhaifu kitabembelezwa na Rais?? Kwa nn hawakuendelea kivyao bila hichob chama dhaifu ???
Nimesema Chadema ya Lissu ni dhaifu kuliko ya Mbowe. Rais Samia amesema lini kuwa wanakisubiri Chadema? Ni kama wakati mmekataa kujaza fomu za Tume ya Uchaguzi, mkandani mtabembelezwa! CCM wameisha wajulia. Wanawapaka mafuta kwa mgongo wa chupa wakati wanaendelea na mambo yao.

Mashinji alikuwa light weight. Na wote uliowataja waliondoka wakati Mbowe alikuwa Mwenyekiti wa Chadema.

Mbowe alijenga watu wa kuchukua nafasi zao. Hata wakina Halima waliponyang'anywa uanachama, Bawacha ya Sharifa na Ruge iliziba pengo lao vizuri sana.

Mbowe ana kipaji cha kutambua na kuwajenga viongozi. Hata Heche anakiri kuwa Mbowe ndie alimjenga kwenye siasa. Mnyika, Halima na wengine wengi tu nao walijengwa na Mbowe.

Chama dhaifu kinasubiriwa kwa hamu sana kwenye meza ya maridhiano
 
Viongozi wangapi wa Chaumma wamerudi Chadema? Tuliambiwa Halima Mdee atarudi Chadema, yuko wapi?
Mimi kila siku huwa nawashangaa Chadema kuhangaika na Chaumma. Inaelekea wameanza kujutia uamuzi wao wa kukataa kuwasikiliza walipokuwa Chadema. Chadema ya sasa hivi imepwaya. Ukiwaondoa Lissu, Heche, Mnyika nani mwingine ana mvuto nchi nzima? Sugu na Boni wana nguvu katika majimbo yao tu. Nani mwingine? Labda Msigwa.

Amandla...
CDM ya sasa ina ushawishi na nguvu kuliko miaka yote tangu kuanzishwa kwake.

Hata waliokuwa hawana vyama sasa hivi wanavutiwa na kufikiria kujiunga CDM.

Lissu amejijengea imani kubwa kwa umma kwa misimamo yake isiyoyumba.
 
Nimesema Chadema ya Lissu ni dhaifu kuliko ya Mbowe. Rais Samia amesema lini kuwa wanakisubiri Chadema? Ni kama wakati mmekataa kujaza fomu za Tume ya Uchaguzi, mkandani mtabembelezwa! CCM wameisha wajulia. Wanawapaka mafuta kwa mgongo wa chupa wakati wanaendelea na mambo yao.

Mashinji alikuwa light weight. Na wote uliowataja waliondoka wakati Mbowe alikuwa Mwenyekiti wa Chadema.

Mbowe alijenga watu wa kuchukua nafasi zao. Hata wakina Halima waliponyang'anywa uanachama, Bawacha ya Sharifa na Ruge iliziba pengo lao vizuri sana.

Mbowe ana kipaji cha kutambua na kuwajenga viongozi. Hata Heche anakiri kuwa Mbowe ndie alimjenga kwenye siasa. Mnyika, Halima na wengine wengi tu nao walijengwa na Mbowe.

Amandla...
Unaongea kikada, kama shabiki tu lenye mapenzi na CCM

Who in their right mind nchini leo anasema kwamba CCM walikuwa na response nzuri ( wameshawajulia chadema) pale CHADEMA walipogoma na CCM wakaendelea na mipango ya uchaguzi uliokuwa hauna upinzani..... Matokeo yake ilikuwaje, uchaguzi ulifanyika ?

Samia aliposema "kuna wenzetu... chama kimoja ... wamegoma tunawazungumza nao..." Kwa hiyo we hujui alikuwa anaongelea kina nani?

Chama kinachotishiwa kufutwa kila uchwao, kulimwa mabarua, wanachama wake kutekwa na kuuliwa kutwa kucha, kufunguliwa makesi ya ugaidi na uhaini unasemaje ni dhaifu kuliko kile cha Mbowe? Acha kuongea kikada, acha kujizima data

Halafu, hata kama chama kile moderate and acquiescent cha Mbowe kilikuwa ndo bora zaidi KILI ACHIEVE NINI ???, CHADEMA YA MBOWE, SOFTCORE OPPOSITION POLITICS ZILIWAFIKISHA WAPI ?????

Wanachadema walishaamua, tunataka hardcore opposition politics. Tunataka Siasa Ngumu.
 
Na wewe hauongei kishabiki? Shabiki lenye mapenzi na Chadema ya siasa ngumu! Hebu nipe mfano wa hizo siasa ngumu na mafanikio yake. Kitu pekee tunacho kiona ni simulizi za Lissu kukataa kutoka mahabusu kwa sharti la kuunga mkono maridhiano. Hakuna hata mmoja wenu aliyediriki kuandamana kudai kiongozi wenu aachiwe. Mmepigwa stop kufanya siasa na kweli mkaufyata.

Hayo yote ya kulimwa mabarua, kutekwa, kufunguliwa kesi za ajabu yalifanyika wakati wa Mbowe.

Mbowe amekaa rumande mara kadhaa, amehukumiwa kifungo na alikitumikia kabla ya kulipiwa faini, Makamu wake alipigwa risasi na akahakikisha anakimbizwa nje ya nchi n.k. Mbowe biashara zake zilifilisiwa na kuhujumiwa. Kwa taarifa yako Mbowe na wenzake walilipiwa faini ya Shilingi milioni 300 na wananchi ndani ya siku mbili. Nyinyi mnaojifanya mnataka siasa ngumu shilingi milioni 300 na ushee zinawatoa kamasi baada ya mchango kutangazwa miezi kadhaa iliyopita. Sasa hivi hamtaki hata kuzungumzia mchango huo.

Niambie nani katika viongozi wa Chadema ya sasa ambae mali na biashara zake zimehujumiwa kama za Mbowe?

Mbowe aliitisha maandamano kadhaa na alijitokeza hata pale yalipokatazwa. Mashujaa wenu karibu wote waliingia mitini. Lissu alilala nyumbani wakati alijua thika kuwa nyumba yake itazingirwa ili kumzuia kutoka. Lema kaja na ndege kutoka Arusha, nae akijua kuwa atapokelewa vizuri na vyombo vya usalama. Mnyika hakuonekana. Heche nae hakuonekana. Hilda alifika lakini akajificha asionekane. Waliojitokeza ni Mbowe na binti yake.

Mbowe alikipokea chama kikiwa na wabunge wasiozidi kumi. Chini ya uongozi wake, Chadema iliwahi kuwa na wabunge zaidi ya 70. Hapo haujazungumzia madiwani.

Mbowe huyo huyo aliweza kuishinikiza serikali iwahakikishie usalama viongozi wa Chadema waandamizi waliokuwa wamekimbia nchi ili waweze kurudi na kuendelea na siasa. Aliwezesha wafuasi na wanachama wa Chadema waliokuwa na kesi za ajabu kufutiwa kesi hizo. Aliwezesha mikutano ya hadhara ya vyama vyote vya siasa kuruhusiwa.

Mtu aliyewafanyia yote hayo leo unamuita mdhaifu! Watu wa ajabu sana.

Amandla...
 
Back
Top Bottom