Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Nijuavyo mimi aombaye maridhiano ni aliyeshindwa, kwa maana hiyo Mbowe anaomba maridhiano kwa kutomtambua Magufuli kama Rais pamoja na serikali yake? Kwa kususia chaguzi za serikali za mitaa zilizofanyika hivi karibuni?Kwa kuzuiwa kufanya mikutano hata ya ndani ya chama? Kwa kesi zinazowakabili mahakamani?n.k
Ni kipi hasa kilichompelekea yeye kuomba maridhiano baada ya madhila yote waliyofanyiwa ikiwemo Mwanasheria wake mkuu wa chama anayeishi uhamishoni mpaka sasa baada ya shambulizi la kikatili?
Sawa,baada ya kuomba maridhiano wamefikia makubaliano yepi?

Mbowe katuvunja sana moyo tuliowaamini, ilikuwa move ya hovyo kabisa kufanywa na tuliyemuamini kama kiongozi shupavu kwenda kupiga goti kuomba poo kwa waliyetuaminisha ni mtesi wao.
Unless atuambie waliyokubaliana katika maridhiano hayo na tuone kwa vitendo vinginevyo tutachukulia kama maridhiano yatakayomnufaisha yeye binafsi na viongozi wenzie chamani mwake.
Wakati huu ambao majibu ya waliomdhuru Lisu hayajapatikana haikuwa wakati wa maridhiano, je Lisu anaonaje? Je anakubaliana na Mbowe kuomba maridhiano ikiwa kila siku anasema hawezi kurejea nchini kwasababu ya usalama wake kutokuwa wa kuaminika? Mbowe amefanya mambo ya hovyo sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iko wazi Mbowe anajaribu kuukwepa mlango wa kuingia jela kupitia kesi ya akwilina ikiwa ni pamoja na kukilindaa kibarua chake.
Iweje Leo aombe maridhiano kwa mtu asiyemtambua kama Rais wa Nchi hii?

Kama walisusia Uchaguzi Serikali za mitaa halafu Leo hii anataka yeye awepo bungeni term ijayo? Je huo sio ubinafsi? Je shutuma zilizokuwa zikitolewa kwa muda mrefu kwamba Serikali inatesa na kuau watu Leo kumebadilika nini? Nimekuwa shabiki na kupigia kura wapinzani kwa term nne tofauti lakini kwa kitendo cha Mbowe kuomba poo nimemshusha vyeo vyote.

Kwangu Mbowe namuona kama wasaliti wengine tu, iweje aombe poo kwa mtu aliyemshtumu kumdhuru Lisu? Sio Mbowe aliyebariki safari za Lisu nje ya Nchi kuipaka matope Tanzania na Serikali yake?

Mwisho kabisa swala la watazania kupigana vita kwasababu ya Siasa zisizo na kichwa wala miguu liondoe kichwani kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ngoja nikuulize swali dogo tu, hivi unadhani Mbowe ndiye aliyefyaua ile risasi iliyomwua Akwilina akiwa ndani ya basi la daladala??

Hebu wewe nieleze sababu zipi zilizofanya yule askari aliyefyattua kizembe bunduki yake hadi kusababisha kifo cha mwanafunzi yule asiye na hatia, auawe ambaye wala hakuwa miongoni ya waandamanaji, asifunguliwe mashtaka ya mauajI??

Hicho ndiyo kitu tunachoweza kukiita "kujimwambafai" na kuweza kuwabambikia kesi akina Mbowe, wakati mhalifu halisi yule Polisi akiachiwa huru mitaani!
 
Ngoja nikuulize swali dogo tu, hivi unadhani Mbowe ndiye aliyefyaua ile risasi iliyomwua Akwilina akiwa ndani ya basi la daladala??

Hebu wewe nieleze sababu zipi zilizofanya yule askari aliyefyatua kizembe bunduki yake hadi kusababisha kifo cha mwanafunzi yule asiye na hatua, ambaye wala hakuwa miongoni ya waandamanaji??

Hicho ndiyo kitu tunachiweza kukiita "kujimwambafai" na kuweza kuwabambikia kesi akina Mbowe, wakati mhalifu halisi akiachiwa huru mitaani!
Ninafahamu Mbowe hakufyatua lisasi na hakuua, na ndio maana nikasema anawezaje kuomba maridhiano ikiwa yeye tu amegeuziwa kibao kwenye kesi kama ile? Anaombaje maridhiano ikiwa wenzake wanaandamwa na kesi mahakamani? Je vipi Lisu anaunga mkono maridhiano? Je Mbowe amehakiiisha usalama wa Lisu ili aweze kurejea nyumbani kuendelea na maisha yako? Kama sivyo basi naamini Mbowe analinda kibarua chake na huo nitauita ubinafsi uliokubuhu! Hivi familia ya Lisu inajisikiaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I mean Lisu kuendelea na maisha yake

..Zitto yuko sahihi.

..cdm pia wako sahihi.

..maridhiano yakishindikana, then hatua anazopendekeza Zitto zitakuwa muafaka.
Zitto yupo sahihi kwa namna nyingi sana, Chadema wamekosea

1. Mbowe, kiongozi wa CDM ndiye kiongozi wa kambi ya Upinzani.
Upinzani unahusisha ACT Wazalendo, tofauti ni kuwa CDM wana Wabunge wengi

Zitto hata kama ni mmoja, ieleweke ana chama na kundi kubwa nyuma yake
Kundi hilo ndilo linaunda upinzani dhidi ya CCM.

Chadema na Mbowe walipaswa kumshirikisha katika maamuzi na sikuchukua hatua peke yao

2. Zitto kama wapinzani wa CDM wanaonja madhila yale yale kutoka serikali na chama tawala
Haiwezekani kumweka pembeni katika wakati wa maamuzi ambayo yanamwathiri pia.

3. Chadema wanaonja machungu ya serikali na CCM si kwasababu wamefanya makosa, bali ubabe tu uliokithiri. Wanapokwa haki zao na ni halali kusema, Wapinzani wananyima haki zao

Chadema na Wapinzani hawajawahi kuwa na tatizo na serikali. Wanachodai ni haki yao ya kikatiba ya kujumuika katika shughuli za kisiasa na za nchi kwa ujumla

Mbowe anapokwenda kuomba maridhiano ni kama vile CDM na Upinzani ulifanya makosa
Maridhiano gani mbele ya haki?
Kwamba unanyimwa haki halafu unataka maridhiano!Haki haiombwi, haki inadaiwa

Hakuna sababu zozote za msingi wala za maana kwa kitendo cha Mbowe

Kwangu ni political stunt kuelekea uchaguzi wa chama ambao ukiuangalia una tatizo

Behind matatizo hayo yupo Mbowe na kundi la 'mwamba tuvushe''.
Hili linahitaji mjadala mwingine, ni kubwa na pana na kama halitaangaliwa CDM inapotea

Pascal Mayalla
 
Wewe hivi hujaona tatizo linaanzia wapi??

Ni kutokana na kitendo cha "kujimwambafai" kwa mkuu wetu, kwa kuamini kuwa yeye ndiye anayelimiliki Jeshi la Polisi nchini na kwa yeyote anayempinga yeye, hata kama ni kwa "constructive criticism" basi ataliamrisha Jeshi *lake" limshughulikie mtu huyo!

Na kwa namna Jeshi letu lilivyopoteza kufanya kazi yake kwa weledi, litatii amri hiyo Ingawa linajua kuwa siyo amri halali!
Kwa maana hiyo sasa tusalimu amri? Hivi unafikiri huyo kiongozi anayejimwambafai atatoa masharti gani baada ya sisi kuomba suluhu (maridhiano)? Atapiga marufuku kukosolewa,jaribio lolote la maandamano ya kudai haki n.k
Ndio, si tumeomba maridhiano? kama vile sisi tulivyoumizwa nae tunajua anaumizwa na kukosolewa au namna yoyote ya kupingana nae na maridhiano ni pande zote mbili kukubaliana. Tutakuwa na upinzani wa aina gani?

Kwa hoja yako unataka kujiaminisha kuwa baada ya kuomba maridhiano ndio vyombo vyetu vya usalama vitafanya kazi kwa weledi? Tena upinzani ndio walioomba maridhiano? You cant be serious.
 
Nifah, Na swali kubwa kwa Mbowe. Hivi kulikuwa na ugomvi gani kati ya CDM na Serikali kiasi cha kuomba maridhiano?
Wanaoteseka ni Wapinzani kwa kupigwa, kufungwa n.k. kwasababu moja tu ya kutumia haki zao za kikatiba. Je, hili ndilo Mbowe analiona tatizo linalohitaji maridhiano?

Yaani watu wananyimwa haki zao za kikatiba na kibinadam halafu wanaomba maridhiano!

Kuna msemo unaosema kuwa , silaha kubwa si ile yenye makali bali silaha ya kumtia mpinzani wako unyonge. Ukishamfanya mnyonge utamshinda bila kurusha ujiti au njiti.

Mbowe kuomba maridhiano ni dalili njema sana ya unyonge! Hilo amevurunda bila mjadala

Sioni utetezi wala sababu zozote zinazoshawishi maridhiano! sioni hata kidogo
Ninachokiona ni unyonge! mbaya sana
 
Ningependa kuona watu wanaomkosoa Zitto waje na hoja na si personal attack

1. Maridhiano kutokana na kitu gani? Kuna tatizo gani lililohitaji maridhiano?

2. Uchaguzi wa serikali za mitaa umefanyika kihuni, umemamlizika kihuni.
Mbowe anataka maridhiano gani katika mazingira kama hayo?

3. Kwanini Mbowe akiwa KUB hakushirikisha Wapinzani wengine ambao walishiriki vyema katika kupinga uchaguzi wa serikali za mitaa, kama ACT?

4. Mbowe anataka maridhiano kama Kiongozi wa Chadema au kiongozi wa kambi ya Upinzani?

Someni hoja za Zitto kwa upana na utulivu, kuna makosa makubwa sana ya Mbowe na CDM

Kwa wanaofuatilia duru za siasa, Mbowe anataka kuondoa pressure ndani ya chama chake kuelekea uchaguzi. Presha hiyo imejengwa na mazingira ya kutatanisha sana

Kuna malalamiko kwamba uchaguzi mkuu utaishia, mtu vs giza, template ya CCM
Huu kama siyo ujima ni maridhiano!

Ili kubadili mwenendo, Mbowe anataka maridhiano ya kudai haki!

Yaani anataka haki katika silver plate, tena haki yake. Ni mbaya kuliko

Ninyi CDM kuna tatizo, hili la maridhiano ni dalili tu. Kuna tatizo la uongozi, kwenu huenda ni jipya kwa wengine si jipya.
 
Mkuu Kennedy upo sahihi kwa asilimia 100

Wengi wa wachangiaji wanauchukulia ule kuwa ni mpambano mathalani wa watani wa jadi kati ya Yanga na Simba, wakati kiuhalisia alichofanya Mbowe, ni kuiepusha nchi yetu isiingie kwenye machafuko ya kupigana sisi wenyewe kwa wenyewe
Hakuna Asiyejua Hali Zamani Kule Zanzibar Ilivyokuwa Hata Salaam Ikawa Watu Wengi Sana Hawasalimiani
Hawasaidiani Kwenye Masuala Yetu Ya Jamii
Kwaujumla Meza Ya Duara Na Sisi Wananchi
Tutaifanya Tanzania Iwe Nzuri
 
Mkuu maisha ya siasa hayaishii tu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa tu.

Bado tunahitaji kupatiwa uwanja safi na huru wa kufanya siasa kwa kukutana na wananchi ili kusikikiza kero zao.

Tunahitaji kuimarisha vyama vyetu kwa kufungua matawi na kuongeza wanachama.

Tunahitaji kujinadi kwa wapiga kura wetu kabla ya uchaguzi mkuu unao kuja kuliko kubakia sandukuni kama ilivyo sasa.

Tunahitaji taifa lenye upendo na umoja na mshikamano bila kubaguana kama ilivyo sasa.

Tunahitaji kuheshimika kwa jamii na kupewa nafasi ya kushiriki kwenye mambo ya kitaifa kama ilivyo tokea juzi kwenye maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa nchi yetu maana sote ni wana [emoji1241] tanzania.

Wewe unafarijika kitu gani ukiwaona viongozi wa vyama vya upinzani nchini wakishinda mahakamani kila wiki?

Unapataje huo ujasili wa kupinga hatua angalau ya mh Mbowe kupata nafasi ya kumuelezea mh rais wa nchi na taifa kwa ujumla juu ya jambo hili muhimu kwa mustakabali mwema wa taifa letu?
Ningependa kuona watu wanaomkosoa Zitto waje na hoja na si personal attack

1. Maridhiano kutokana na kitu gani? Kuna tatizo gani lililohitaji maridhiano?

2. Uchaguzi wa serikali za mitaa umefanyika kihuni, umemamlizika kihuni.
Mbowe anataka maridhiano gani katika mazingira kama hayo?

3. Kwanini Mbowe akiwa KUB hakushirikisha Wapinzani wengine ambao walishiriki vyema katika kupinga uchaguzi wa serikali za mitaa, kama ACT?

4. Mbowe anataka maridhiano kama Kiongozi wa Chadema au kiongozi wa kambi ya Upinzani?

Someni hoja za Zitto kwa upana na utulivu, kuna makosa makubwa sana ya Mbowe na CDM

Kwa wanaofuatilia duru za siasa, Mbowe anataka kuondoa pressure ndani ya chama chake kuelekea uchaguzi. Presha hiyo imejengwa na mazingira ya kutatanisha sana

Kuna malalamiko kwamba uchaguzi mkuu utaishia, mtu vs giza, template ya CCM
Huu kama siyo ujima ni maridhiano!

Ili kubadili mwenendo, Mbowe anataka maridhiano ya kudai haki!

Yaani anataka haki katika silver plate, tena haki yake. Ni mbaya kuliko

Ninyi CDM kuna tatizo, hili la maridhiano ni dalili tu. Kuna tatizo la uongozi, kwenu huenda ni jipya kwa wengine si jipya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wale wanaosoma madesa ya mwalimu halafu mtihani wa Taifa unafeli,.je,utaendelea kusoma hayohayo,MADESA YA NGUNGURI NA NGANGARI YA ZANZIBAR YAMEZAA MATOKEO GANI HADI SASA,
Kafanya vizuri Hekima MARIDHIANO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo aliyokuwa anafanya Zitto kipindi cha Kikwete na haya wanayofanya wakina Mbowe yakuomba waonewe huruma yanatofauti gani mkuu?.

Yaani siasa alizofanya Zitto tukaziona zakijinga ndio hizohizo wanakujanazo wakina Mbowe.
Tofauti ipo kubwa sana, wakati CDM walikubaliana ndani ya kamati kuu waende kwenye sherehe za uhuru wa Tanzania, na wakasema walichokisema mbele ya halaiki ya watu, Zitto alikuwa anatoroka usiku, anaenda kufichwa chumbani, hata hatujui alikuwa anamwaambia nini babake!. af akitoka huko anakuja anasema nataka uenyekiti CDM!, hahaaa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1576129760387.png
 
Unaomba maridhiano upewe haki zako kwenye sahani na anae anaekupora haki?.
 
Move waliyoifanya Chadema inaonyesha uchovu wa akili za viongozi wao.Waachie demokrasia ndani ya chama chao kwanza kabla hatujawapa nchi.Hii cream ya uongozi wao wa sasa yote haipaswi kuwepo pale.Hata mwizi ana demokrasia lakini wao hawana.Mtu unaposema kwa mazingira magumu ya sasa hakuna awezaye kuivusha Chadema zaidi ya Mbowe,na wale wa kijani wakisema kwa mazingira ya sasa hakuna awezaye kuivusha Tz zaidi ya Jiwe,hivyo hakuna uchaguzi,utalalamika?Tunaipenda Chadema,Mbowe tunakushukuru sana,umefanya mengi,ni wakati wa kuwaachia wengine.Usiniambie hakuna,maana kama wewe ni kiongozi mzuri kwa muda uliokaa madarakani ulipaswa kuwa umeshawaandaa akina Mbowe wengine.Akina Mtei walikuachia chama salama,then pass it on to somebody else katika njia zinazoeleweka kidemokrasia.Practice what you preach!
 
Ningependa kuona watu wanaomkosoa Zitto waje na hoja na si personal attack

1. Maridhiano kutokana na kitu gani? Kuna tatizo gani lililohitaji maridhiano?

2. Uchaguzi wa serikali za mitaa umefanyika kihuni, umemamlizika kihuni.
Mbowe anataka maridhiano gani katika mazingira kama hayo?

3. Kwanini Mbowe akiwa KUB hakushirikisha Wapinzani wengine ambao walishiriki vyema katika kupinga uchaguzi wa serikali za mitaa, kama ACT?

4. Mbowe anataka maridhiano kama Kiongozi wa Chadema au kiongozi wa kambi ya Upinzani?

Someni hoja za Zitto kwa upana na utulivu, kuna makosa makubwa sana ya Mbowe na CDM

Kwa wanaofuatilia duru za siasa, Mbowe anataka kuondoa pressure ndani ya chama chake kuelekea uchaguzi. Presha hiyo imejengwa na mazingira ya kutatanisha sana

Kuna malalamiko kwamba uchaguzi mkuu utaishia, mtu vs giza, template ya CCM
Huu kama siyo ujima ni maridhiano!

Ili kubadili mwenendo, Mbowe anataka maridhiano ya kudai haki!

Yaani anataka haki katika silver plate, tena haki yake. Ni mbaya kuliko

Ninyi CDM kuna tatizo, hili la maridhiano ni dalili tu. Kuna tatizo la uongozi, kwenu huenda ni jipya kwa wengine si jipya.

..Mzee mwenzangu umesahau kwamba TANGANYIKA ilipata UHURU bila kumwaga damu, kupitia MARIDHIANO.

..binafsi kuomba maridhiano siyo unyonge bali ni ishara ya kukataa kulipa unyama kwa unyama, ukatili kwa ukatili, na dhuluma kwa dhuluma.

..alternative ya maridhiano ni CDM / wapinzani kulipa kisasi, na wakifanya hivyo hawatakuwa na tofauti na CCM.

..Nchi hii tuliaminishwa kuwa wapinzani wana vurugu na watasababisha vita, lakini utawala wa awamu ya 5 umedhihirisha kwamba watawala / CCM ndiyo wapenda shari, na wavunja amani na wenye kutishia mshikamano wa waTz.
 
Zitto kapanic kwa lile walilofanya CHADEMA jana, kashtukizwa hakutegemea, anatamani ile nafasi ingekuwa yake kwa tabia zake za ki_opportunist, toka jana ni twitter, insta habanduki huko, eti leo Zitto anataka siasa za mapambano anawafundisha CHADEMA!, wonders shall never end, wakati ule anaenda kukutana na JK watu wanamuuliza kulikoni anasema JK ni sawa na babake, vipi leo Magufuli sio sawa na babake pia?!
Zitto huyuhuyu kwenye uzinduzi wa bunge aliamua kubaki na kusikiliza hotuba ya Magufuli akitofautiana na wabunge wengine wa upinzani walioamua kususia na hakuna aliyemehutumu. Katika siasa watu hutumia mbinu tofauti kufanikisha malengo yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom