Zitto kabwe: Mradi wa NSSF wa kiwanda cha kuzalisha sukari Mkulanzi kilichogharimu Tsh bilioni 130 hakijazalisha hata tani moja mpaka sasa

Zitto kabwe: Mradi wa NSSF wa kiwanda cha kuzalisha sukari Mkulanzi kilichogharimu Tsh bilioni 130 hakijazalisha hata tani moja mpaka sasa

Mradi wa ujenzi wa kiwanda hiki unakadiriwa kutumia sh bilioni 130 mpaka sasa na mtaji wake sh bilioni 250.

Uwezo wake wa kuzalisha sukari ni tani 250,000/= lakini hakijazalisha hata tani 1.

Shamba la miwa lina miwa ya hekta 800 imechomwa moto, mradi umekufa.
Kwa hiyo aliyechoma moto miwa ni serikari aubni watu waliotumwa na zito ili aje kulalamika hpa?

Je miwa hiyo haitalimwa tena?
 
Haiwezekani kuzalisha tani 250,000 kwa kulima hekta 800 (Narudia haiwezekani, hiyo ilikuwa lugha ya kutapeli pesa za wafanyanyakazi tu)

TPC inalima hekta hazizidi 8000 lakini hawajawahi kuzalisha kuzidi tani 120,000

Kilombero Sukari (ILLOVO) iwanalima sio pungufu ya hekta 16,000 jumlisha wakulima wa nje (Outgrowers) lakini haijawahi kuzalisha kuzidi tani 250,000

Sasa muujiza wa kiwanda cha MVUHA kinatokea wapi?

Zitto's observation is right and he has spoken minds of many voiceless.
Nadhani kuna zaidi ila hizo 800 ndizo walilima
 
Sekta ya umma na biashara ya viwanda wapi na wapi?

Yule jamaa alikuwa wa ajabu sana
 
Ila hii nchi tunapigwa, ila na tulivyo wajinga na mafala tunaishia kushangilia, huu ujinga wetu utatuisha lini?

Kwa nini tuna kiwango hiki cha ujinga?

Ni lini utambuzi utatuijia?
Simply....ukijuwa kusoma na kuandika unakuwa MP/MBUNGE,halafu unaongea maneno ya ajabu.
 
Hata kile kiwanda cha mabuti cha magereza lazima kitajifia.

Ushauri hawa watu wakijenga na kuweka mtaji kwenye hii miradi wauze sekta binafsi iendeshe au wafanye kwa ubia.

Mtu anaepokea salary ya serikali na biashara wapi na wapi?
 
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inapoacha kazi zake za msingi na kuingizwa mkenge na wanasiasa uchwara.Wastaafu wanakosa mafao yao huku fedha zao zikiingizwa katika biashara ,ujenzi na viwanda uchwara.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] biashara pekee yenye risks ndogo ni real estate ndio maana walikuwa huko lakini Magu aliharibu kila kitu
 
Upo sahihi lakini ni kweli tunatakiwa tuwe na upungufu wa sukari kila mwaka Tanzania na kwa nini hicho kitu Nchi zingine majirani zetu hakuna na wana bei pungufu kuliko sisi na ni hao hao Ilovo...
Bei ilikuwa 2000-2500 ,muulizeni mwendazake alifanyaje hadi bei kuwa. 3000-3500?
 
Mradi wa ujenzi wa kiwanda hiki unakadiriwa kutumia sh bilioni 130 mpaka sasa na mtaji wake sh bilioni 250.

Uwezo wake wa kuzalisha sukari ni tani 250,000/= lakini hakijazalisha hata tani 1.

Shamba la miwa lina miwa ya hekta 800 imechomwa moto, mradi umekufa.
Hiyo ndiyo kazi ya awamu ya 5. Ndiyo Legacy tuliachiwa. Nina hasira mno na hiyo awamu. Tulidanganywa mno kama watoto wadogo. Ndiyo maana uhuru wa Habari ulibinywa ili wale investigative Journalists wasifukue madudu. Nguvu kubwa ilitumika kificha maovu. Sasa yanawekwa hadharani. Hiyo ndiyo Legacy. Narudia hiyo ndiyo legacy.
 
Hayo mapagale wkati yanajengwa si ndo hao akina Zitto na shoga yake Dau walikuwa wanakula pesa za NSSF. Yeye anakuja na hili la kiwanda, mara mashamba yamechomwa mara pesa bhla! bhla!
Mazingira ya uchumi yalikuwa yanaruhusu ila yalivurugwa na marehemu ndio maana miradi imejifia
 
Waswana ka Nchi kadogo tuu huwa wanazalisha mpaka ziada na hiyo ziada muda mwingine wanakosa soko mpaka zinapita siku za matumizi wanachoma Moto bongo kila kukicha sukari ni big ishu ili wapewe wachache vibali wapige pesa...
Ukiweka business minded staff ambao wamefanya Kazi nje au ndani ndio waendeshe haya mashirika kibiashara yatafaulu ila sio hao wajinga mliwaokota kwenye Utumishi wa umma
 
Hivi ni nani alituloga? Akahamisha Ubungo wenye akili akatuwekea hewa?. Tunaliwa tu na tunakubali kuliwa.
 
Mradi wa ujenzi wa kiwanda hiki unakadiriwa kutumia sh bilioni 130 mpaka sasa na mtaji wake sh bilioni 250.

Uwezo wake wa kuzalisha sukari ni tani 250,000/= lakini hakijazalisha hata tani 1.

Shamba la miwa lina miwa ya hekta 800 imechomwa moto, mradi umekufa.
Kwani NSSF wanyewe wanasemaje?
 
NSSF wana miradi mingi ya ajabu
Sana bila wa kusahau na ule mradi wa jimboni kwake wa kununua viwania kwa heka milioni 200.
Inabidi upelekwe mswada wa kulinda hela za wastaafu kwani watu wanajichotea tu.
 
Anti Magufuli wanapenda sana nyuzi za aina hii zenye maudhui ya kuweka doa, na kuleta siasa za paka na panya, yaani CCM vs Chadema, upande ule ni mbaya si tuliwaambia....! Tuchagueni sisi.

Sasa nyie kwa akili zenu hizo za kudemka mmepata stori kamili ya kinachoendelea behind the scene kuhusu hicho kiwanda kilichojengea na NSSF zaidi ya hayo maneno ya Zitto? Mmesikiliza upande wa pili wanajiteteaje au wana maelezo gani? Au je idea ya kujenga kiwanda ni mbaya? Kama hakijaweza kuzalisha kifanyeje kianze kuzalisha? Naona watu wanakimbilia kumlalamikia JPM as if idea ya uhamasishaji viwanda ilikuwa ni idea ya hovyo kwa kutumia mfano wa NSSF. Hiyo inaitwa nitpicking na ni logical falacy iliyojengwa kwenye misingi ya chuki tu.

Matatizo ya NSSF na mifuko yote ya kijamii ni mtambuka na yashughulikiwe bila kuingiza suala la chuki juu ya mtu mmoja fulani.
 
Hata kile kiwanda cha mabuti cha magereza lazima kitajifia.

Ushauri hawa watu wakijenga na kuweka mtaji kwenye hii miradi wauze sekta binafsi iendeshe au wafanye kwa ubia.

Mtu anaepokea salary ya serikali na biashara wapi na wapi?
Well said my friend!!!!

Duniani kote hauwezi kukuta Serikali inafanya biashara. Kazi ya Serikali inatakiwa itengeneze sera nzuri za kuziwezesha hizo biashara kukua na kushamiri na SIO kujiingiza kwenye biashara na kushindana na private sectors. Serikali iweke sera nzuri ili iweze kupata kodi ya kutosha kutoka kwa private sector.

Kwa nchi zinazojitambua hapa duniani huwezi kukuta Serikali inajiingiza moja kwa moja kwenye biashara. Nchi haiwezi kutunga sera and at the same time ifanye biashara, ikifanya hivyo yafuatayo yatajitokeza;

1. Sector binafsi ita-perish completely

2. Public Enterprises zita-collapse in long run due to lack of seriousness

3. Hakutakuwa na mzunguko wa pesa wa kutosha

4. Ukosefu wa ajira

5. Hakutakuwa na checks and balance kwasababu Serikali yenyewe ndo inatunga sera na yenyewe kufanya biashara

6. Tutakuwa tunarudi nyuma tulikotoka na kwenda kinyume na dunia

7. N.k
 
Back
Top Bottom