Zitto Kabwe: Mwaka 2016-2019, wakati wa utawala wa Hayati Magufuli, watanzania milioni nne waliingia katika kundi la umasikini mkali

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Akitoa mada yake katika mazungumzo ya miaka 30 ya vyama vingi vya siasa, Zuberi Zitto Kabwe, alieleza kwamba kwa miaka mitatu tu, utawala wa JPM ulitengeneza masikini milioni nne, ambao,hapo awali, walikuwa wanajimudu kimaisha.

Hii maana yake JPM angetawala miaka 10 basi robo tatu ya watanzania wangekuwa masikini na wanyonge wa kutupwa, hivyo kumpa mtaji wa kura na kisiasa kwa kuwa alikuwa Rais wa masikini na wanyonge.

Kwa maana hiyo, alikuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa Rais wa maisha kwa kuwa angekuwa na uhakika wa kura.
 
Akitoa mada yake katika mazungumzo ya miaka 30 ya vyama vingi vya siasa, Zuberi Zitto Kabwe, alieleza kwamba kwa miaka mitatu tu, utawala wa JPM ulitengeneza masikini milioni nne, ambao,hapo awali, walikuwa wanajimudu kimaisha...

Magufuli hakuwahi kutegemea kura kupata madaraka toka alipokuwa mbunge. Wangalau ubunge wake wa kwanza ndio alipata kwa kura halali, lakini toka amekuwa mbunge, hakuwahi kuwa muumini wa ushindani wa haki.

Alipokuwa rais kutokana na udhaifu wa katiba hii, akanajisi uchaguzi waziwazi. Hivyo bila kujali hali ya wananchi kimaisha, yeye angefia madarakani kama sio Mungu kuchukua hatua.
 
Mko kupambana na marehemu na bado anawagaragaza tu!!

Apumzike kwa Amani, katufanya tujue maana ya uongozi ni nini!!

Kwa sasa tuendeleeni kuramba asali huku tukipiga mapambio " Mama ana upiga mwingi"[emoji3525]
 
Naona umebadili id kutoka kinembe hadi kiembe!

Ok.. Huyo Zito wako amesema hao watu walikuwa wanafanya kazi zipi zilizokuwa zinawapa utajili kisha wakawa masikini?

Zitto aendelee kuramba asali tu hakuna mtu atamlaumu
 
Nasikia Mbowe akaanda mazingira 2025 mtashinda kwa kishindo kikuu
 
Naona umebadili id kutoka kinembe hadi kiembe!

Ok.. Huyo Zito wako amesema hao watu walikuwa wanafanya kazi zipi zilizokuwa zinawapa utajili kisha wakawa masikini?

Zitto aendelee kuramba asali tu hakuna mtu atamlaumu
Wakulima wa korosho, wavuvi waliofilisiwa na Mpina na wafugaji ambao ng'ombe zao hazijulikani ziko wapi baada ya JPM na Mpina kuzikamata. Kariakoo iligeuka "mahame" mwanza ikafa kibiashara, Arusha na mbeya kwisha kazi

Sijabadili ID
 
Kwahiyo Mungu kamuwahi hahaha
 
Naona umebadili id kutoka kinembe hadi kiembe!

Ok.. Huyo Zito wako amesema hao watu walikuwa wanafanya kazi zipi zilizokuwa zinawapa utajili kisha wakawa masikini?

Zitto aendelee kuramba asali tu hakuna mtu atamlaumu

Huyo chawa uchwara hiyo ID wamemlazimisha Mods kubadilisha,yeye kwa akilizake alikuwa anaona sawatu.

Wana jaribu kumchafua Magu sababu Magu hakutaka urafiki wakijinga kwamba uwerafikiyake alafu ukikwepa kodi akuchekee.

Ndio maana aliwaparua mbaka untouchables.
 
Mbowe kafikia mwisho wa siasa, ataandaa mazingira gani ya 2025 boss? Bado unaoongelea habari za uchaguzi, kwani nchi hii kuna uchaguzi? Watu tuna mahesabu tofauti kabisa, sio hayo ya kwenda kupoteza muda kwenye mstari wa kura.
Kwa hiyo hamtaki kwenda ikulu kabisa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…