Zitto Kabwe vs Prof. Kitila Mkumbo juu ya ujenzi wa SGR

Zitto Kabwe vs Prof. Kitila Mkumbo juu ya ujenzi wa SGR

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Zitto Kabwe:
Uharibifu wa Uchumi unaofanywa na Serikali yaMagufuli ni mkubwa sana. Itachukua miaka 10 kurudi Hali ya mwaka 2015 ( ambayo nayo haikuwa nzuri) iwapo ataondolewa madarakani mwaka huu. Akipata miaka 5 mingine itachukua miongo 2 ( miaka 20, two decades) na Marais 2 kurudi 2015

Zitto Kabwe:

Uchumi unaanguka kwa sababu ya viongozi kukosa MAARIFA. Tunapaswa kuikoa nchi yetu sasa sio kesho. Mwagapombe2020.

Zitto Kabwe:

SGR kipande cha Dar-Moro kilikuwa kiishe Novemba, sasa kipo 70%. Kuisha mwaka kesho. Sasa mkopo wa Biashara wa Fedha za kigeni umechukuliwa. Riba 9%. Serikali ipo kwenye panic. Gharama za Ujenzi zinaongezeka ( costs over run ). Mbia mmoja wa Ujenzi ( Mreno) kabwaga manyanga

Zitto Kabwe:

Akaanza kujenga. Hela zikatoka kwenye mzunguko. Hali ya maisha ya wananchi ikawa mbaya, ukuaji wa mzunguko wa Fedha ( M3- money supply ukawa NEGATIVE). Serikali ikaanza kushindwa kulipa invoices za Mkandarasi, wakandarasi wadogo wakakimbia. Ujenzi ukasimama! Moro-Dom ikakwama

Zitto Kabwe:

Mradi wa Reli ya Kati ya SGR USD Bilioni 7.5 - Fedha UWEKEZAJI WA UBIA ( PPP ) kutoka Benki ya Exim ya China ulikataliwa na Rais Magufuli akiamini kuwa ni dili la mtangulizi wake. Akasema tutajenga wenyewe kwa kutumia Kodi. Tukamwambia haiwezekani (Assets-Liabilities Match )

zitto Kabwe:

Niongeze kidogo kuwa, Standard Chartered Bank inaunganisha Deni la $1.4bn halafu anasaini CEO wa Dar? Largest single foreign currency denominated loan by Tanzania? Backed by export credit agencies of Sweden and Denmark? Isainiwe vile? Riba ndio 9%? Desperation au nini?

Kitila Mkumbo:
Hoja ya msingi ni hizo hela zinakwenda wapi. Tunajua kwa dhati kabisa fedha inayokopwa inakwenda kwenye miradi ya maendeleo na inaonekana. Ni wewe uliyeshauri kwa bidii kuwa tusijenge miradi hii kwa hela za ndani.

Zitto Kabwe:

Ni kweli nilishauri mwaka 2016 kuwa hamwezi kujenga Mradi mkubwa wa Reli SGR kwa Kodi za wauza nyanya. Imewachukua miaka 4 kuelewa hilo na baada ya Reli kuishia Morogoro, Wakandarasi kutolipwa na kuahirisha uzinduzi mara 7. Kuendesha Nchi ni MAARIFA sio maguvu na Ukatili

Kitila Mkumbo:
Hoja ya msingi ni hizo hela zinakwenda wapi. Tunajua kwa dhati kabisa fedha inayokopwa inakwenda kwenye miradi ya maendeleo na inaonekana. Ni wewe uliyeshauri kwa bidii kuwa tusijenge miradi hii kwa hela za ndani.

Zitto Kabwe:
Mimi sijasema lolote. Nimemwaga data tu kutoka Benki Kuu kuhusu Deni la Taifa. Kwamba wakati Uchumi unakua kwa 4-5% kwa mwaka, Deni la Nje ( Foreign currency denominated) linakua kwa zaidi ya 18% kwa mwaka. Katika miaka 4, Serikali ya Magufuli imekopa zaidi ya miaka 10 ya Kikwete

Kitila Mkumbo:
Replying to Zitto Kabwe
Hoja ya msingi ni hizo hela zinakwenda wapi. Tunajua kwa dhati kabisa fedha inayokopwa inakwenda kwenye miradi ya maendeleo na inaonekana. Ni wewe uliyeshauri kwa bidii kuwa tusijenge miradi hii kwa hela za ndani.
 
Kitila Mkumbo ,

..angetueleza huu mkopo ni wa MUDA gani na RIBA yake ni kiasi gani.

..pia labda Prof angetuelimisha zaidi kuhusu UNAFUU wa mkopo huo akilinganisha mikopo mingine ambayo Tz imechukua, au nchi nyingine ambazo zimechukua mikopo mikubwa kwa ajili ya miundombinu.
 
Sio kama itatokea wasaliti kushinda uchaguzi lakini ukisema itakuchukua miaka 20 kuweka nchi sawa, inamaanisha unajiwekea kinga kama ukitenda mabaya usilaumiwe. That's not leadership.
 
February 5, 2020
Kilosa, Tanzania

Wahandisi : SGR kuchukua miaka 15 kuikamilisha pia Reli ya kati ihamishwe toka eneo la mafuriko

Wakati wa ukaguzi wa uharibifu wa njia ya reli ya kati sehemu za Gulwe na Kilosa, wataalamu wa ujenzi wa reli wamebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuitumia reli ya mkoloni kwa miaka zaidi ya 10 ijayo.

Pia Reli mpya ya SGR itachukua takriban miaka 15 kumalizwa kujengwa hilo limebainishwa ktk eneo la reli ya kati lililokumbwa na mafuriko yasiyo ya kawaida wakati jopo la wahandisi na mkurugenzi mkuu walipokuwa wanajadili athari za mafuriko na changamoto za reli ya mkoloni na reli mpya ya SGR.

TRC inapoteza zaidi ya milioni 100 kwa siku kutokana na kusitisha safari reli ya kati. Na ili kukabiliana na mafuriko inabidi reli ya kati ihamishiwe mlimani na mlima huo unahitaji kuchongwa pia .

Uharibifu ktk eneo la mto Mkondoa ni mkubwa sana na ingawa eneo hilo la Gulwe Kilosa hakuna mvua lakini mvua kubwa zinazonyesha mikoa ya Iringa na Dodoma inaingiza kiasi kikubwa cha maji mto Mkondoa.

Source: TRC Reli
 
Hiyo miaka kumi na tano inaweza kuwa kweli, hao wakandarasi wanaogopa kumwambia kwasababu hataki kusikiliza ushauri wa mtu, alishakosea kwenye mengine kama la korosho hakujifunza, anakosea sasa kwenye hiyo reli bado hataki kujifunza, na atakosea mengine mbele ya safari, sijui Kikwete alimtoa wapi huyu mtu, bora angempa mwanamke tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SGR reli kuisha yote ndani ya Miaka 15 hao wahandisi wamejaribu sana kuitetea serikali ya CCM Mpya. Kiuhalisia ni 2020 + 15 = 2035
 
Kitila mkumbo ni profesa wa education, zitto ni mchumi,
Siyo hivyo tu. Prof Kitila Mkumbo ni mpinzani wa kiukweli kweli ila kwa maadili ya kuwa yuko Serikalini hawezi kusema anachokiamini.

Ndiyo maana jibu lake ni la mkato kuwa pesa inakwenda kwenye miradi ya maendeleo. Kwenye moyo wake anajua kuwa hii SGR ni uharibifu wa fedha za umma. Miradi hii haiwezi kulipika. Soon tunarudi kwenye status ya 1995 tulipokuwa tunaitwa ni nchi ya HIPC (Highly Indebted Poor Countries)
 
Zito Kabwe siyo smart kichwani, ni mradi Dunia hii ambao haongezeki gharama ukilinganisha na gharama ya awali? Hiyo ni kawaida sana kwenye miradi yote hata nyumba yako binafsi tu.

Na kwa kuwa huyu jamaa siyo intelligent hakuna mahali ataenda kisiasa, 2020
wanamwaga Ubunge halafu kwisha habari yake.
 
Hiyo miaka kumi na tano inaweza kuwa kweli, hao wakandarasi wanaogopa kumwambia kwasababu hataki kusikiliza ushauri wa mtu, alishakosea kwenye mengine kama la korosho hakujifunza, anakosea sasa kwenye hiyo reli bado hataki kujifunza, na atakosea mengine mbele ya safari, sijui Kikwete alimtoa wapi huyu mtu, bora angempa mwanamke tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo SGR ya kwenda Rwanda hata ingekamilika mwaka 2019 bado haina tija mpaka ukamilishe unavyokwenda Mwanza na Kigoma.

Ya kwenda Rwanda imelenga mzigo wa tani 800,000 kwa mwaka ndiyo throughput ya nchi nzima. Mzigo wa maana uko Kivu/ Goma kwa kupitia Kigoma na mzigo wa Uganda kwa kupitia Mwanza.

Ila Jiwe kwa kukurukpuka na kufanya kazi za misifa na huku anadanganywa ma Muuaji Paul Kagame yeye kapeleka Rwanda. Ni wendawazimu mtupu
 
Back
Top Bottom